Agano Jipya 2023
Septemba 10. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Faraja katika Yesu Kristo Wakati Mpendwa Anapofariki? 1 Wakorintho 14–16


“Septemba 10. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Faraja katika Yesu Kristo Wakati Mpendwa Anapofariki? 1 Wakorintho 14-16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)

“Septemba 10. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Faraja katika Yesu Kristo Wakati Mpendwa Anapofariki?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023

wanawake wakitembea

Septemba 10

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kupata Faraja katika Yesu Kristo Wakati Mpendwa Anapofariki?

1 Wakorintho 14–16

ikoni ya kushauriana kwa pamoja

Shaurianeni kwa Pamoja

Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20

Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.

  • Ishi injili. Ni kwa jinsi gani kumgeukia Bwana hutusaidia kukabiliana changamoto zetu na majaribu yetu?

  • Kuwajali wenye mahitaji. Nani tunamjua ambaye anahitaji maombi yetu na urafiki wetu?

  • Waalike wote kuipokea injili. Ni mipango gani ya kushiriki injili iliyojadiliwa katika mikutano ya baraza la vijana la kata? Ni kwa jinsi gani darasa letu au akidi yetu inaweza kushiriki?

  • Unganisha familia milele. Ni kwa jinsi gani kazi ya historia ya familia imeimarisha mahusiano yetu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:

  • Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.

  • Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.

ikoni ya kufundisha mafundisho

Fundisha Mafundisho

Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35

Jiandae Binafsi Kiroho

Wakati mtu tunayempenda anapofariki, inaweza kuwa inaumiza. Utenganisho kutoka kwa mpendwa wetu huleta hisia za ghamu kubwa na huzuni. Lakini Paulo alifundisha kwamba hatimaye “mauti imemezwa kwa kushinda” (1 Wakorintho 15:54) kwa sababu ya Ufufuko wa Yesu Kristo. Kwa maneno mengine, “uchungu wa mauti”—maumivu na mahangaiko tunayohisi katika mwili unaokufa—”imemezwa katika Kristo” (Mosia 16:7–8); ona pia 1 Wakorintho15:54–57).

Wakati fulani, kila mtu atapata uzoefu wa kifo cha mpendwa wake. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata faraja katika nyakati hizi ngumu kupitia imani yao katika Yesu Kristo? Fikiria kuhusu swali hili unapojiandaa kufundisha kwa kusoma 1 Wakorintho 15; Mosia 16:7–9; Mafundisho na Maagano 42:44–46).

Jifunzeni Pamoja

Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa au akidi kushiriki wakati walihisi kitu ambacho hung’ata. Ungeweza kisha kuwauliza kwa nini unafikiri Paulo alitumia neno “uchungu” (ona 1 Wakorintho 15:54–56). Wapatie dakika chache kupitia tena 1 Wakorintho 15 na kushiriki kweli wanazopata kuhusu jinsi uchungu wa mauti ulishindwa. Kisha fikiria shughuli kama zile zilizopo hapo chini kuwasaidia vijana kuelewa vyema jinsi Mwokozi anaweza kutufariji wakati mtu tunayemjali unapokufa.

  • Unaweza kuwagawa washiriki wa darasa au akidi katika jozi na kuomba kila jozi kupitia tena pamoja baadhi ya vifungu vya maandiko katika “Nyenzo Saidizi.” Wangeweza kuandika majibu yao kwa swali kama “Ni kweli gani muhimu ninatarajia kukumbuka ninapompoteza mpendwa wangu? Waombe kujumuisha taarifa kutoka kwenye vifungu vya maandiko katika jibu lao. Kisha waalike kushiriki pamoja na darasa kweli ambazo zina maana kwao na kwa nini.

  • Fikiria kupitia tena pamoja tukio kutoka katika ujumbe wa mkutano mkuu ukionyesha jinsi mtu alivyopata tumaini katika Yesu Kristo wakati mtu waliyekuwa wanamjali alifariki. Mifano inajumuisha ujumbe wa Dada Reyna I. Aburto “Kaburi Halina Ushindi” (Liahona, May 2021, 85–86) na ujumbe wa Mzee S. Mark Palmer “Huzuni Yetu Itageuzwa kuwa Shangwe” (Liahona, May 2021, 88–89). Unaweza kupata msukumo kushiriki uzoefu wako mwenyewe au waalike vijana kushiriki jinsi walivyopata faraja na tumaini katika Yesu Kristo baada ya mpendwa wao kufa.

  • Baada ya kuzingatia mahitaji ya washiriki wa darasa lako au akidi yako, onyesha moja au zaidi ya video katika “Nyenzo Saidizi.” Waalike vijana kushiriki misukumo yao. Ni kwa jinsi gani kujua kwamba Yesu Kristo alifufuka kunaathiri jinsi wanavyoona kifo? Waalike washiriki wa darasa lako au akidi yako kushiriki ushuhuda wao kuhusu Mwokozi na Ufufuko Wake na jinsi elimu hii huwaletea tumaini.

  • Yohana 11 inaelezea uzoefu wa Mwokozi na kifo cha mpendwa mmoja—rafiki Yake Lazaro. Pengine darasa au akidi wangesoma mstari wa 1–45 pamoja, na wanaposoma, wangeweza kushiriki vitu wanavyojifunza kutokana na mfano wa Mwokozi. Je, tunajifunza nini kutokana na tukio hili ambacho kinaweza kutufariji wakati mtu tunayempenda anakufa? Ni kwa jinsi mfano wa Mwokozi wa “kuomboleza na wale wanaoomboleza … na kuwafariji wale ambao wanahitaji kufarijiwa”? (Mosia 18:9). Ni nini tunachojifunza katika Mafundisho na Maagano 42:45–46 ambacho kinaweza kutusaidia kufanya hivyo? Unaweza kutaka kuonyesha video “One-on-One (Ministering with Love)” (ChurchofJesusChrist.org).

kijana akitafakari

Ushuhuda wetu wa Ufufuko wa Yesu Kristo unatupatia tumaini wakati mpendwa anakufa.

Tenda kwa Imani

Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Nyenzo Saidizi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha hujumuisha kuhudumu kwa upendo na kuwasaidia wengine kupokea baraka za injili, na usaidizi huu mara nyingi ndio hasa kile washiriki wa darasa wasioshiriki kikamilifu wanahitaji. Sote tunahitaji kufanya kazi pamoja kuwasaidia wale ambao wanakabiliana na changamoto, na kama mwalimu unaweza kuwa katika nafasi ya kipekee kutoa usaidizi.