Agosti 27. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Kwamba Najua Mwili Wangu Ni Zawadi Takatifu kutoka kwa Mungu? 1 Wakorintho 1–7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023 (2022)
“Agosti 27. Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Kwamba Najua Mwili Wangu Ni Zawadi Takatifu kutoka kwa Mungu?,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Akidi za Ukuhani wa Haruni na Madarasa ya Wasichana: Mada za Mafundisho 2023
Agosti 27
Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuonyesha Kwamba Najua Mwili Wangu Ni Zawadi Takatifu kutoka kwa Mungu?
Shaurianeni kwa Pamoja
Ikiongozwa na mshiriki wa urais wa darasa au akidi; takribani kwa dakika 10–20
Mwanzoni mwa mkutano, rudieni kwa pamoja Dhima ya Wasichana au Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni. Kisha ongoza mjadala kuhusu kazi ya wokovu na kuinuliwa ukitumia swali moja ua mengi ya yale yaliyopo hapo chini au yako mwenyewe (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 10.2, 11.2). Panga njia za kutenda juu ya kile mnachojadili.
-
Ishi injili. Ni uzoefu gani wa karibuni uliotuleta karibu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
-
Kuwajali wenye mahitaji. Je, Kuna mtu amehamia kwenye kata yetu au kujiunga na Kanisa? Tunawezaje kuwasaidia wao wajisikie kukaribishwa?
-
Waalike wote kuipokea injili. Je, kuna shughuli zozote zinazokuja ambazo tunaweza kuwaalika marafiki zetu kuhudhuria?
-
Unganisha familia milele. Je, Ni juhudi gani tunaweza kufanya kuandika historia yetu binafsi?
Mwishoni mwa somo, kama inafaa, fanya yafuatayo:
-
Shuhudia juu ya kanuni zilizofundishwa.
-
Wakumbushe washiriki wa darasa au akidi kuhusu mipango na mialiko iliyotolewa wakati wa mkutano.
Fundisha Mafundisho
Mkiongozwa na kiongozi mtu mzima au kijana; takribani kwa dakika 25–35
Jiandae Binafsi Kiroho
Kwa uzuri au ubaya, Watakatifu wa Siku za Mwisho yaonekana wanajulikana sana kwa kile tusichofanya. Nyingi ya hizi “usifanye” zina uhusiano na jinsi tunavyoitendea miili yetu. Nyuma ya kila moja ya chaguo hizo kuhusu kufanya ni baadhi ya kweli za milele—kile sisi tunachojua. Wakati kweli za milele zinaongoza chaguo zetu, chaguo hizo zinakuwa rahisi kufanya, zenye furaha zaidi, na za kudumu zaidi. Kweli za milele pia hutusaida sisi kuelezea chaguo zetu kwa marafiki zetu. Pengine kama nyongeza ya kujulikana kwa kile tusichofanya, tungeweza kuwa wazuri kujulikana kwa kile tunachojua.
Fikiria kuhusu kweli za milele unazojua kuhusu miili yetu—kwa nini tunazo, jinsi Mungu anahisi kuzihusu, na jinsi Yeye hututaka sisi kuhisi kuzihusu. NI kwa jinsi gani kujua kweli hizi kumekubariki na kushawishi chaguo zako? Ni kwa jinsi gani elimu hii hubariki washiriki wa darasa lako au akidi yako? Unapotafakari hili, soma Mwanzo 1:27; 1 Wakorintho 6:19–20; na makala ya Rais Russell M. Nelson “Mwili Wako: Kipawa Kikuu cha Kutunzwa” (Liahona, Agosti 2019, 50–55).
Jifunzeni Pamoja
Washiriki wa darasa lako au akidi yako walipoijifunza maandiko wiki hii, wanaweza kuwa walikuwa na mawazo juu ya mafundisho ya Paulo kuhusu miili yao katika 1 Wakorintho 6. Njia moja ya kuwaalika wao kushiriki mawazo haya ni kumpa kila mmoja wao kipande cha karatasi na kuwaomba wao kuandika angalao majibu matatu yamkini kwa swali “ Ni kwa jinsi gani miili yetu ni kama mahekalu? Wahimize wao wasome 1 Wakorintho 6:19–20 wanapotafakari swali hili. Wao wangeweza kisha kushiriki majibu yao mmoja kwa mwingine. Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Mwokozi kuhusu miili yetu hushawishi chaguo tunazofanya? Hapa kuna baadhi ya shughuli za ziada juu ya mada hii; chagua kutoka kwa hizo, au panga moja yako mwenyewe.
-
Kama ungetaka kuwa na mjadala zaidi kuhusu mfananisho wa Paulo kati ya mwili na hekalu, fikiria kuonyesha picha za mahekalu kadhaa tofauti. Unaweza kupata baadhi yake katika temples.ChurchofJesusChrist.org. Washiriki wa darasa au akidi wangeweza kujadili tofauti wanazoona katika mahekalu haya, pamoja na vitu walivyo sawa. Wangeweza pia kuongelea kuhusu jinsi wanavyohisi wakati wanapokuwa hekaluni. Ni nini ambacho hufanya hekalu kuwa mahali pa kiroho, na patakatifu? Kisha ungeweza kuhimiza darasa au akidi kulinganisha vitu walivyojadili kuhusu mahekalu na miili yetu. Ni kwa jinsi gani mafundisho kuhusu mahekalu katika Mafundisho na Maagano 97:15; 109:8, 12 yanavyohusiana na miili yetu?
-
Washiriki wa darasa lako au akidi yako wanaweza kuwa walipata—au watakuwa—na fursa za kuelezea kwa nini wanafuata mafundisho ya Mwokozi kuhusu kuitunza miili yetu. Ungeweza kuwauliza baadhi yao kile wangesema kama, kwa mfano, mtu angewauliza kwa nini hawanywi pombe, chai, au kahawa au kwa nini hawavalii aina fulani ya nguo. Ni zipi baadhi ya kweli kutoka katika injili ya Yesu Kristo ambazo uathiri jinsi tunavyoitendea miili yetu? Washiriki wa darasa lako au akidi yako wangeweza kupata baadhi ya kweli hizi chini ya “Nyenzo Saidizi.”
-
Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuwa na staha ya kina kwa ajili ya miili yao ya ajabu, ungeweza kuonyesha video “God’s Greatest Creation” (ona pia Russell M. Nelson, “Mwili Wako: Kipawa Kikuu cha Kutunzwa,” 50–55). Ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatutaka tuhisi kuhusu miili yetu. Ungeweza pia kujadili njia Shetani hujaribu kushawishi kuidunisha au hata kuichukia miili yetu. Tunaweza kufanya nini ili kushinda ulaghai wake na majaribu? Ni kweli gani zitatusaidia sisi? Baadhi ya nyenzo katika “Nyenzo Saidizi” zinaweza kusaidia.
Tenda kwa Imani
Watie moyo washiriki wa darasa au akidi kutafakari na kuandika kile watakachofanya juu misukumo waliyoipokea leo. Kama wangependa, wangeweza kushiriki mawazo yao. Waalike wafikirie kuhusu jinsi kutenda juu ya misukumo yao kutaimarisha mahusiano yao na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.
Nyenzo Saidizi
-
Mwanzo 1:27; 1 Wakorintho 6:19–20; Alma 11:42–44; 40:23; Mafundisho na Maagano 89; 130:22
-
“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” hasa aya tatu za kwanza
-
“The Lord Gave Me a Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 153
-
Makala kuhusu miili yetu katika New Era ya Agosti au Liahona
-
Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Katika kutupatia zawadi ya mwili, Mungu ameturuhusu kuchukua hatua muhimu kuelekea kuwa zaidi kama Yeye. Shetani anaelewa hili. … Hivyo mengi, kama si yote, ya majaribu anayoweka katika njia yetu hutusababisha kutumia vibaya miili yetu au miili ya wengine. … Mwili wako ni hekalu lako binafsi, lililojengwa kuipa hifadhi roho yako ya milele [ona 1 Wakorintho 3:16–17; 6:18–20] Utunzaji wako wa hekalu hilo ni muhimu. Sasa, ninawauliza, … je, mnavutiwa zaidi katika kuvisha na kuiweka nadhifu miili yenu ili kuvutia ulimwengu kuliko mnavyofanya kumpendeza Mungu? Jibu lenu la swali hili linatuma ujumbe wa moja kwa moja Kwake kuhusu hisia zenu kuhusiana na zawadi Yake kuu kwenu” (“Tunaweza Kufanya Vizuri Zaidi na Kuwa Wazuri Zaidi,” Liahona, Mei 2019, 68).
-
Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Wale ambao wanaamini kwamba miili yetu si kitu zaidi ya matokeo ya mageuko ya nasibu hawatahisi uwajibikaji wowote kwa Mungu au mtu yeyote kwa kile wanachofanya na au kwa miili yao. Sisi ambao ni mashahidi wa uhalisi mkuu wa maisha kabla ya kuzaliwa, maisha duniani, maisha ya milele, hata hivyo, ni lazima kutambua kwamba tuna wajibu kwa Mungu kuhusiana na mafanikio makuu ya uumbaji wa kimwili Wake. … Mwili wetu ni chombo cha roho yetu, ni muhimu kwamba tuutunze vyema tuwezavyo. Tunapaswa kuziweka wakfu nguvu zake kumtumikia na kueneza kazi ya Kristo” “Kuakisi juu ya Maisha Yaliyowekwa Wakfu,” Liahona, Nov. 2010, 17).