Njoo, Unifuate
Mikutano ya Baraza Jumapili ya Kwanza


Jumapili ya Kwanza Mikutano ya Baraza

Kwenye Jumapili ya kwanza ya kila mwezi, mikutano ya akidi ya wazee, na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama haijumuishi somo linalofundishwa na mwalimu. Badala yake, urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama unaongoza mikutano ya baraza. Katika mikutano hii ya baraza ya Jumapili ya kwanza, kila akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama wanashauriana pamoja kuhusu wajibu wa mahali pao, fursa na changamoto; kujifunza kutokana na utambuzi na uzoefu wa kila mmoja wao; na kupanga njia za kufanya juu ya misukumo iliyopokewa kutoka kwa Roho. Majadiliano haya yanapaswa yatokane na maandiko husika na mafundisho ya manabii wanaoishi.

Siyo mikutano yote ya baraza itafanana. Hii hapa ni baadhi ya miongozo ili kusaidia urais kuongoza baraza lenye mafanikio.

Kabla ya mkutano wa baraza

Fanya:

  • Tafuta shida za eneo husika, fursa, na changamoto

  • Kwa maombi chagua mada ya kujadiliana.

  • Waalike washiriki wa akidi au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama waje wakiwa wamejitayarisha kutoa mawazo na uzoefu wao.

Usifanye:

  • Kutayarisha Somo.

  • Kuja na suluhisho maalumu au mpango wa utendaji akilini.

Wakati wa mkutano wa Baraza

Fanya:

  • Waalike washiriki kushiriki uzoefu waliopata wakati wakifanyia kazi misukumo na mipango iliyotokana na mikutano ya awali.

  • Wasilisha mada ya mkutano na wahimize washiriki kushauriana pamoja juu ya mada hiyo, mkitafuta suluhisho na mwongozo kutoka kwenye maandiko, maneno ya manabii, na Roho Mtakatifu.

  • Panga kutenda juu ya kile kilichojadiliwa. Hii inaweza kujumuisha mipango ya kikundi au mipango ambayo watu binafsi wanaifanya wao wenyewe.

Usi:

  • Usitawale mazungumzo.

  • Kujaribu kuwashawishi wengine juu ya mawazo yako.

  • Kujadili maswala nyeti au ya siri.

  • Kufundisha Somo.

  • Kumshinikiza yoyote kushiriki.

Baada ya mkutano wa baraza

Fanya:

  • Ufuatiliaji juu ya mipango na kazi zilizopangwa wakati wa mkutano wa baraza

  • Tafuta njia za kuwajumuisha wale ambao hawakuweza kuhudhuria mkutano kwa sababu ya miito yao au sababu zingine zozote. Wajulishe kuhusu mipango ambayo ilifanywa.

  • Wape fursa washiriki kuelezea uzoefu wao katika mikutano ijayo.

Mada kwa ajili ya Mikutano ya Baraza la Jumapili ya Kwanza.

Mawazo kwa ajili ya mada za kujadili katika mikutano ya baraza yanaweza kutoka kwenye mikutano ya urais, mikutano ya baraza la kata, mpango wa eneo, mawazo ambayo viongozi wanayapokea wanapowahudumia waumini, na ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mada hizi hapo chini ni mapendekezo tu. Viongozi wanaweza kufahamu kuhusu shida nyinginezo ambazo wanahisi wamepata mwongozo wa kiungu wa kuzishughulikia.

  • Je, tunaweza kufanya nini ili kuwatumikia wale wanaotuzunguka? (Ona Mosia 23:18).

  • Je, tunawezaje kuyawekea kipaumbele majukumu yetu tofauti ?

  • Je, ni kwa jinsi gani tutaweza kushiriki injili pamoja na marafiki na majirani zetu? (ona Alma 17).

  • Je, tunawezaje kujilinda wenyewe pamoja na familia zetu dhidi ya mitandao isiyo mizuri ya mawasiliano na ponografia?

  • Je, tutafanya nini kusaidia kuwanasihi na kuwaimarisha watoto na vijana wetu katika kata yetu?

  • Je, ni kwa namna gani tunaweza kushiriki katika kazi ya historia ya familia na ibada ya hekaluni?

  • Je, ni kwa namna gani tunaweza kuomba usaidizi wa Bwana kutafuta majibu kwa maswali yetu ya injili na kuelewa kwa kina injili?

  • Je, tunawezaje kuimarisha ushuhuda wetu juu ya Bwana na Injili Yake na kusaidia familia zetu kujitegemea kiroho?

Chapisha