Njoo, Unifuate
Kwa nini Tuna Mikutano ya Akidi na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama?


Kwa nini Tuna Mikutano ya Akidi na Muungano wa Usaidizi wa Wakina mama?

Katika hizi siku za mwisho, Mungu amerejesha ukuhani na kupanga akidi za ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama ili kumsaidia kutimiza kazi Yake ya wokovu. Kwa sababu hii, kila Jumapili wakati tunapokutana katika mikutano ya Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, tunajadiliana na kupanga nini tutakachofanya ili kusaidia kutimiza kazi ya Mungu. Ili iwe na matokeo yanayotarajiwa, mikutano hii inatakiwa kuwa zaidi ya madarasa. Kuna fursa za kushauriana kuhusu kazi ya wokovu, kujifunza pamoja kuhusu kazi ile kutoka mafundisho ya viongozi wa Kanisa, na kupanga na kujiandaa sisi wenyewe kuitimiza.

Chapisha