Njoo, Unifuate
Mikutano ya Jumapili ya Pili na ya Tatu


Mikutano ya Jumapili ya Pili na ya Tatu

Jumapili ya pili na ya tatu ya kila mwezi, akidi za wazee na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama watajifunza kutoka katika mafundisho ya viongozi wa Kanisa kutoka kwenye Mkutano Mkuu wa hivi karibuni. Msisitizo unapaswa kutolewa kwenye ujumbe kutoka kwa washiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Hata hivyo, kutokana na shida za mahali husika na mwongozo wa kiungu kutoka kwa Roho, ujumbe wowote kutoka kwenye mkutano mkuu wa hivi karibuni unaweza kujadiliwa.

Mara nyingi, akidi ya wazee au Urais wa Usaidizi wa Wakina Mama watachagua ujumbe wa mkutano mkuu wa kujifunza kutokana na mahitaji ya waumini, ingawa askofu au rais wa kigingi anaweza kuchangia. Viongozi wanaweza kuchagua ujumbe unaoshabihiana na mada iliyojadiliwa kwenye Jumapili ya kwanza ya baraza, au wanaweza kuchagua ujumbe juu ya mada tofauti, kutokana na mwongozo wa kiungu kutoka kwa Roho.

Viongozi na walimu wanapaswa kutafuta njia za kuwahimiza waumini kusoma ujumbe teule mapema, na kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki ukweli wa injili na mawazo kuhusu jinsi ya kuzifanyia kazi. Shughuli za kujifunza zilizopendekezwa hapo chini, ambazo zimetokana na kanuni zilizomo katika Kufundisha katika njia ya Mwokozi, zinaweza kusaidia waumini kujifunza kutoka kwenye ujumbe wa Mkutanao Mkuu

Picha
President M. Russell Ballard

M. Russell Ballard, “Karama kuu kutoka kwa Mungu,” 9–11

Ujumbe wa Rais Ballard unaelezea mada mbalimbali—ikijumuisha manabii, imani katika Kristo, sakramenti, na washiriki wa akidi yako au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama wanaweza kupata mada tofauti hususani zenye maana. Waalike waumini kushiriki kitu fulani kutoka kwenye ujumbe huu ambacho kiliwavutia. Ni mialiko au baraka gani zilizoahidiwa tunazozipata katika ujumbe wa Rais Ballard? Fikiria kuwaalika waumini kutafakari kwa dakika chache kile wanachohisi kimewavutia kufanya kama matokeo ya majadiliano haya.

Picha
Elder Gary E. Stevenson

Gary E. Stevenson, “Moyo wa Nabii,” 17–20

Ili kuwasaidia waumini “kuelewa uzito” wa wito wa nabii mpya, unaweza kuwaalika waumini kutafuta katika ujumbe wa Mzee Stevenson, wakitafuta ukweli na umaizi ambao unawasaidia wao kuelewa umuhimu na utukufu wa mchakato huu. Fikiria kuwaalika waumini kuelezea jinsi walivyohisi wakati wa kusanyiko takatifu ambapo Rais Nelson alikubalika kama Rais wa Kanisa. Unaweza pia kuchora moyo ubaoni na kuwaomba waumini waandike ndani yake maneno au virai ambayo vinauelezea moyo na tabia ya Rais Nelson. Je, yeye amefundisha kitu gani ambacho kimetubariki sisi?

Picha
Elder Neil L. Andersen

Neil L. Andersen, “Nabii wa Mungu,” 24–27

Kujadiliana ujumbe wa Mzee Andersen kunaweza kuimarisha imani za waumini katika manabii wanaoishi. Unaweza kuwaalika kutafuta katika ujumbe huu kitu fulani ambacho kinawasaidia wao kuelewa kwa nini Mungu ana manabii duniani na kwa nini tunawafuata. Je, ni kwa namna gani sisi tumebarikiwa kwa sababu ya kuwa na nabii? Waumini wanaweza kuelezea jinsi walivyopata ushuhuda kwamba Rais Russell M. Nelson ni nabii wa Bwana na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Picha
Elder David A. Bednar

David A. Bednar, “Mnyenyekevu na Mnyofu wa Moyo,” 30–33

Ili kuhamasisha mjadala kuhusu ujumbe wa Mzee Bednar, unaweza kuandika ubaoni Unyenyekevu ni … Na Unyenyekevu sio … Waumini kisha wanaweza kuuchambua ujumbe wa Mzee Bednar na kuandika ubaoni virai wanavyopata ambavyo vinakamilisha kauli hizi. Tunajifunza nini kutoka kwenye ujumbe huu ambacho kinatupa mwongozo wa kuwa wanyenyekevu zaidi? Ni mifano gani ya unyenyekevu tunaweza kuifikiria? Tunawezaje kutumia ushauri wa Mzee Bednar wa kuwa wanyenyekevu zaidi?

Picha
Sister Bonnie L. Oscarson

Bonnie L. Oscarson, “Wasichana katika Kazi,” 36–38

Maswali ni njia mojawapo ya kushawishi watu kutafakari. Fikiria kuandika ubaoni maswali machache ambayo ujumbe wa Dada Oscarson unajibu, kama vile Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwahusisha wasichana katika kazi ya Bwana? Waalike waumini kupekua ujumbe wake kwa ajili ya majibu kwa maswali haya na kujadili kile wanachojifunza. Je, ni baraka gani zinakuja wakati wasichana wanapohusishwa katika utumishi? Pengine washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu walioupata wakitumikia sambamba na wasichana. Kutokana na majadiliano yetu, tunahisi tumepata mwongozo wa kufanya nini?

Picha
Elder Dale G. Renlund

Dale G. Renlund, “Historia ya Familia na Kazi ya Hekalu: Kuunganishwa na Uponyaji,” 46–49

Mzee Renlund alizungumzia juu ya ono la Ezekieli la hekalu na maji yakibubujika kutoka ndani yake (ona Ezekieli 47:8–9). Pengine mshiriki wa akidi au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama anaweza kuchora picha ya ono hili ubaoni. Ni kwa jinsi gani baraka za hekalu na historia ya familia hufanya kazi kama maji katika ono la Ezekieli? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki na wengine uzoefu wao wa baraka za hekalu na kazi ya historia ya familia. Je, tunaweza kufanya nini ili kufanya historia ya familia na kazi ya hekalu kuwa sehemu ya kawaida zaidi ya maisha yetu?

Picha
Elder D. Todd Christofferson

D. Todd Christofferson, “Akidi ya Wazee,” 55–58

Katika Akidi ya Wazee, unaweza kuwaomba washiriki wa akidi wasome sehemu ya ujumbe wa Mzee Christofferson wenye kichwa cha “Madhumuni ya Mabadiliko Haya,” Je, tunaweza kufanya nini ili kuhakikisha kwamba tunatimiza madhumumi haya? Katika Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, unaweza kumwomba mtu mmoja kufanya muhtasari wa mabadiliko kwa akidi za Ukuhani wa Melkizedeki ambayo Mzee Christofferson anaelezea. Wakina dada kisha wanaweza kutambua kanuni zilizodokezwa katika mabadiliko haya ambazo zinaweza kutumika kwenye kazi yako ya Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama. Katika akidi ya wazee au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, washiriki wanaweza kujadili kile wanachojifunza kutokana na hadithi ya Kaka Goates na jinsi inavyotumika kwenye kazi yao.

Picha
Elder Ronald A. Rasband

Ronald A. Rasband, “Tazama! Jeshi la Kifalme,” 58–61

Pengine kuimba, kusikiliza, au kusoma maneno ya “Tazama! Jeshi la Kifalme” (Wimbo, na. 251) pamoja unaweza kutia hamasa mjadala kuhusu ujumbe wa Mzee Rasband. Je, ni kwa jinsi gani akidi za ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama ni kama jeshi la kifalme? Waumini pia wanaweza kutafuta na kujadili “wingi wa baraka” Mzee Rasband anazitaja zitakuja kutokana na muundo mpya wa akidi za ukuhani. Ni baraka gani zingine tulizozipokea—au tunazotegemea kuzipokea—kutokana na kutekeleza mabadiliko haya? Je, ni kwa jinsi gani Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama pia kwa ukamilifu zaidi utapokea baraka kama vile “karama tofauti” na “kunasihi”?

Picha
President Henry B. Eyring

Henry B. Eyring, “Utumishi wenye Mwongozo wa Kiungu

Rais Eyring anaelezea kuhusu mahubiri ya mikutano miwili ya sakramenti ambayo ilimfurahisha. Pengine unaweza kuwauliza nusu ya akidi au washiriki wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama kurejea maneno ya kijana wa umri wa miaka 14 na nusu ingine kurejea hadithi kuhusu mwalimu wa nyumbani. Wanaposoma, waumini wanaweza kufikiria juu ya ushauri wanaoweza kumpa kijana au msichana ambaye ndio kwanza amepangiwa kumtumikia mtu fulani. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza “kuwa na mwongozo wa kiungu zaidi na wenye hisani katika… huduma za utumishi wetu”?

Picha
President Dallin H. Oaks

Dallin H. Oaks, “Nguvu za Ukuhani,” 65–68

Ili kuanza mjadala, unaweza kuandika vichwa vya sehemu nne za ujumbe wa Rais Oaks ubaoni. Kisha mwalike kila mmoja wa washiriki kusoma sehemu moja kimya kimya na kisha kuandika ubaoni sentensi moja ambayo inatoa muhtasari wa ujumbe kamili wa sehemu ile. Washiriki kisha wanaweza kushiriki kile ambacho wanahisi kushawishika kufanya kwa sababu ya kile walichosoma. Je, ni kwa jinsi gani huduma zetu kama wenye ukuhani au wakina dada wa muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama tutaziendeleza tunapotumia mafundisho katika ujumbe wa Rais Oaks?

Picha
President Russell M. Nelson

Russell M. Nelson, “Kutumikia kwa Nguvu na Mamlaka ya Mungu,” 68–75

Rais Nelson anawataka wenye ukuhani “kuinuka juu” na kutumia ukuhani ili kuwabariki watoto wa Baba wa Mbinguni. Waalike washiriki wa akidi yako au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama kupekua mifano anayotoa na kujadili jinsi gani inavyotusaidia kuelewa jinsi ukuhani unavyoweza kutumika kubariki familia zao na wengine. Ni uzoefu gani tunaweza kushiriki na wengine wakati tumekwisha barikiwa na nguvu ya ukuhani? Tunawezaje kuwasaidia wengine au sisi wenyewe kuwa na imani kutumia ukuhani wa Mungu ili “kutumikia katika jina Lake”?

Picha
Sister Reyna I. Aburto

Reyna I. Aburto, “Kwa Dhamira Moja,” 78–80

Ujumbe wa Dada Aburto unatoa fursa kwa akidi yako na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama kutathimini jinsi gani mnavyofanya kazi vizuri kwa umoja katika kufanya kazi ya Bwana. Ili kuwasaidia waumini kufanya hivi, unaweza kuonesha picha za vipepeo wakubwa, ziara ya Mwokozi kwa Wanefi (ona Kitabu cha Sanaa cha Injili, 82, 83, 84), na kazi ya hisani ya Kanisa (ona LDS.org). Waumini wanaweza kuchambua ujumbe na kugundua jinsi Dada Aburto alivyotumia mifano hii kufundisha kuhusu azma na baraka ya kufanya kazi kwa umoja. Tunaweza kufanya nini kufanya kazi “kwa nia moja”?

Picha
President Henry B. Eyring

Henry B. Eyring, “Roho Wake Apate kuwa pamoja Nawe,” 86–89

Kuongeza matamanio yetu na uwezo wa kumpokea Roho Mtakatifu, Rais Eyring anaelezea baadhi ya uzoefu wake binafsi na anatoa mwelekeo maalumu. Baada ya kutafakari uzoefu wake, kumbukumbu gani zinazofanana washiriki wako wa akidi au Muungano wa Usaidizi wa akina Mama wanaweza kushiriki wakati Roho Mtakatifu alipogusa mioyo yao au alipothibitisha ukweli? Pengine washiriki wanaweza kuorodhesha ubaoni mwongozo ambao Rais Eyring alioshiriki kusaidia “kufungua mioyo yetu ili kupokea huduma ya Roho.” Ni kwa jinsi gani kufuata mwelekeo wake kutatusaidia katika maisha yetu na katika familia zetu? Katika akidi zetu au Muungano wa Usaidizi wa akina Mama?

Picha
President Dallin H. Oaks

Dallin H. Oaks, “Vitu Vidogo na Rahisi,” 89–92

Ujumbe wa Rais Oaks una sitiari ambazo zinafundisha kiasi gani mambo madogo na rahisi yanavyoweza kuwa na matokeo yenye nguvu kwa wema au ubaya. Sitiari hizi ni pamoja na mizizi ya mti, timu ya wapiga kafia, nyuzi za kamba, na maji yanayotona. Waumini wanaweza kusoma sitiari hizi na kujadili kile zinachofundisha kuhusu nguvu ya kufanya mambo madogo na rahisi kwa uthabiti. Je, ni mambo gani madogo na rahisi ambayo yanaleta ushawishi wa Roho Mtakatifu ndani ya maisha yetu? Waalike waumini watakafari wanavutiwa kufanya nini ili kufuata ushauri wa Rais Oaks.

Picha
President Russell M. Nelson

Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” 93–96

Katika ujumbe huu, Rais Nelson anatusihi tuongeze “uwezo wetu wa kiroho ili kupokea ufunuo.” Kuwasaidia waumini kufuata mwelekeo wake, unaweza kuandika maswali kama yanayofuata ubaoni: Kwa nini tunahitaji ufunuo? Tunawezaje kuongeza uwezo wetu wa kupokea ufunuo—vyote kibinafsi na tunaposhauriana pamoja? Ni baraka gani Rais Nelson aliahidi kama tutatafuta ufunuo? Wagawe washiriki katika makundi, na alika kila kundi litafute na kuelezea majibu kwa mojawapo ya maswali.

Picha
Elder Gerrit W. Gong

Gerrit W. Gong, “Kristo Bwana Kafufuka Leo,” 97–98

Ni kwa namna gani washiriki wa akidi yako au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama wanaweza kujifunza kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Gong kuhusu maagano yetu na Upatanisho wa Yesu Kristo? Unaweza kuwaalika waumini kuchunguza ujumbe, wakitafuta baraka ambazo Upatanisho wa Mwokozi na maagano yetu—vikifanya kazi pamoja—zinatolewa kwetu. Kisha fikiria kuuliza maswali kama yafuatayo kuhusu nini walichokipata: Je, ni kwa jinsi gani maagano yetu na Upatanisho vinafanya kazi pamoja ili “kutuwezesha na kutuadilisha” sisi? Vinatusaidia kushikilia nini na kuachia nini?

Picha
Elder Ulisses Soares

Ulisses Soares, “Manabii Hunena kwa Uwezo wa Roho Mtakatifu,” 98–99

Ujumbe wa Mzee Soares unatupa mwongozo wa kiungu wa kutenda kwa imani wakati tunapojihisi upungufu katika kufanya mapenzi ya Bwana. Je, ni kwa jinsi gani Mzee Soares alipokea faraja na uhakika wakati alipopokea wito wake mpya kama Mtume? Je, alijifunza nini kutokana na tukio la kuitwa kwake kama rais wa misheni? Tunaweza kujifunza nini kutokana na huo uzoefu wake. Wape waumini muda wa kushiriki uzoefu wao wakati walipohisi kutokuwa na uhakika kuhusu kitu fulani ambacho Bwana aliwataka kukifanya. Walifanya nini ili kupata imani ya kusonga mbele?

Picha
Elder Jeffrey R. Holland

Jeffrey R. Holland,”Kuwa Pamoja na Kuwaimarisha,” 101–3

Kama washiriki wa akidi yako au Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama walijua kuhusu mabadiliko kwenye “dhana ya utumishi kwa ukuhani na Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama” ni maswali gani walikuwa nayo? Ujumbe wa Mzee Holland unaweza kutoa majibu. Waumini wanaweza kutafuta kanuni za injili ambazo Mzee Holland anafundisha ni msingi wa mabadiliko haya. Ni mialiko gani tunayoipata katika ujumbe huu? Je, ni baraka gani zimeahidiwa? Je, ni kwa jinsi gani njia hizi mpya za utumishi zinatusaidia kuwa “wafuasi wa kweli wa Kristo”?

Picha
Sister Jean B. Bingham

Jean B. Bingham, “Utumishi kama wa Mwokozi anavyofanya,” 104–7

Katika ujumbe wake, Dada Bingham anatutaka tujiulize wenyewe maswali ambayo yanaweza kuongoza jitihada zetu za utumishi. Waumini wanaweza kujadili jinsi maswali haya yanavyoweza kuongoza jitihada zao na kisha kutafuta majibu kwa swali la Dada Bingham, “Kwa hiyo [utumishi] unaonekana kama nini?” Unaweza kutumia muda kurejea baadhi ya mifano Dada Bingham anashiriki juu ya utumishi wa watu binafsi na waombe waumini kuelezea mifano yao wenyewe. Je, tunapata nini katika ujumbe wa Dada Bingham ambacho kinaongeza uelewa wetu wa kwa nini na jinsi gani tunatumikia?

Picha
Elder Dieter F. Uchtdorf

Dieter F. Urchtdorf, “Tazama Mtu!,” 107–10

Tunawezaje kumsaidia mtu fulani kuelewa kwamba dhabihu ya kulipia dhambi na Ufufuko wa Yesu Kristo ilikuwa ni matukio muhimu zaidi katika historia ya ulimwengu? Waalike waumini kutafakari swali hili wanaposoma sehemu za ujumbe wa Mzee Uchtdorf. Je, wanapata nini ambacho kitasaidia kuelezea kwa nini matukio haya ni muhimu sana kwao? Baada ya majadiliano haya, washiriki wa darasa wanaweza kuzungumza kuhusu inamaanisha nini kwao “kumtazama mtu.” Je, ni kwa jinsi gani umejifunza “kumtazama mtu”?

Picha
Elder Quentin L. Cook

Quentin L. Cook, “Jiandae Kukutana na Mungu,” 114–17

Unaweza kuanzisha majadiliano yenu ya ujumbe wa Mzee Cook kwa kumtaka mshiriki kutoa muhtasari juu ya urejesho wa funguo za ukuhani katika hekalu la Kirtland. Kulingana na ujumbe wa Mzee Cook, ni majukumu gani Kanisa linayo ambayo yana uhusiano na funguo hizi? Je, ni kwa jinsi gani majukumu haya yanajitokeza katika Kanisa leo? Andika maneno haki, umoja, na usawa ubaoni, na waombe waumini kushiriki umaizi wanaoupata kuhusu kila mojawapo ya kanuni hizi kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Cook. Je, ni kwa jinsi gani kanuni hizi zinatusaidia kutimiza majukumu matukufu ya Kanisa?

Chapisha