Njoo, Unifuate 2024
Februari 5–11: “Huru Kuchagua Uhuru na Uzima wa Milele, kupitia yule Mpatanishi Mkuu.” 2 Nefi 1–2


“Februari 5–11: ‘Huru Kuchagua Uhuru na Uzima wa Milele, kupitia yule Mpatanishi Mkuu.’ 2 Nefi 1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)

“Februari 5–11. 2 Nefi 1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)

Picha
Adamu na Hawa wakiondoka katika Bustani ya Edeni

Adamu na Hawa, na Douglas Fryer

“Huru Kuchagua Uhuru na Uzima wa Milele, kupitia yule Mpatanishi Mkuu”

2 Nefi 1–2

Kama ungelijua kwamba maisha yako yapo karibu na mwisho, ni jumbe zipi za mwisho ungetaka kushiriki na wale unaowapenda zaidi? Wakati nabii Lehi alipohisi alikuwa akikaribia mwisho wa maisha yake, aliikusanya familia yake pamoja kwa mara ya mwisho. Alishiriki pamoja nao kile ambacho Baba wa Mbinguni alikuwa amemfunulia. Alitoa ushuhuda wake juu ya Masiya. Alifundisha kweli za injili alizozithamini kwa watu aliowathamini. Alizungumza juu ya uhuru, utii, anguko la Adamu na Hawa, ukombozi kupitia Yesu Kristo na shangwe. Siyo watoto wake wote walichagua kuishi kwa kile alichofundisha—hakuna kati yetu anayeweza kufanya chaguzi hizi kwa ajili ya wapendwa wetu. Lakini tunaweza kufundisha na kushuhudia juu ya Mkombozi, anayetufanya tuwe “huru kuchagua uhuru na uzima wa milele” (ona 2 Nefi 2:26–27).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Kanisani na Nyumbani

2 Nefi 1:13–29

Ninaweza “Kuzinduka! na kuinuka kutoka mavumbini.”

Katika 2 Nefi 1:13–29, zingatia maneno aliyoyatumia Lehi kuelezea hali za kiroho za Lamani na Lemueli. Je, kipi hukusaidia wewe uzinduke kutoka kwenye “usingizi mzito” wa kiroho? Je, ni kipi hukusaidia ujifungue “minyororo” ya kiroho katika maisha yako? Fikiria kuhusu ushuhuda wa Lehi katika mstari wa 15 na mwaliko wake katika mstari wa 23. Je, Baba wa Mbinguni ana ujumbe upi kwa ajili yako kwenye mistari hii?

Tumia vielelezo vya kufundishia. Kutumia vielelezo vya kufundishia kutawasidia wanafunzi waelewe kweli za injili na kuzikumbuka kwa muda mrefu. Unapojiandaa kufundisha kutoka katika muhtasari huu, fikiria ni vielelezo vipi vya kufundishia ungeweza kutumia. Kwa mfano, yawezekana mnyororo wa karatasi ungeweza kuwasaidia wanafunzi waelewe maneno ya Lehi katika 2 Nefi 1:13 au 2 Nefi 2:27.

Picha
ikoni ya seminari

2 Nefi 2

Kwa sababu ya Yesu Kristo “niko huru kuchagua uhuru na uzima wa milele.”

Familia ya Lehi ilikuwa sasa katika nchi mpya, iliyojaa mategemeo mengi mapya. Chaguzi walizozifanya katika sehemu hii mpya zingekuwa muhimu kwa ajili ya furaha na mafanikio yao. Pengine hii ndiyo sababu Lehi alimfundisha Yakobo, mtoto wake kuhusu haki ya kujiamulia au uwezo wa kufanya chaguzi, katika 2 Nefi 2:25. Unapojifunza mistari 11–30, andika majibu yanayoweza kupatikana ya maswali haya:

  • Je, kwa nini haki ya kujiamulia ni muhimu sana kwa Baba wa Mbinguni, ingawa baadhi ya watu wanaitumia kwa njia za kuumiza?

  • Je, ni kwa namna gani adui hujaribu kudhoofisha au kuharibu haki yetu ya kujiamulia?

  • Je, ni kwa namna gani Mwokozi anakusaidia “uchague uhuru na uzima wa milele” (mstari wa 27)?

Hapa kuna njia nyingine ya kujifunza kuhusu haki ya kujiamulia katika 2 Nefi 2: Tafuta vitu ambavyo ni muhimu kwa ajili yetu ili tuwe na haki ya kujiamulia na kufikia uwezekano wetu wa kiungu. Kwa mfano:

Je, kungetokea nini kwenye haki yetu ya kujiamulia kama moja au zaidi ya mambo haya yangekosekana?

Kila moja ya vipengele sita vya Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana: Mwongozo wa Kufanya Chaguzi hubeba “Mialiko” na “Baraka Zilizoahidiwa.” Angalia kwenye moja au zaidi ya vipengele hivi na chagua baraka iliyoahidiwa unayoitumainia katika maisha yako. Je, ni mwaliko upi unahitaji kuufanyia kazi ili upokee baraka hii? Fikiria kushiriki na mtu mwingine baraka ambazo umepokea kutokana na kufuata mialiko hii.

Ona pia Mada za Injili, “Haki ya Kujiamulia na Uwajibikaji,” Gospel Library; “Tuko Huru Kuchagua,” Nyimbo za Dini, na. 134.

2 Nefi 2:1–4, 6–25

Mungu anaweza kugeuza majaribu yangu yawe baraka.

Lehi alijua kwamba Yakobo, mwanaye mdogo alikuwa amepitia “mateso” na “huzuni nyingi” wakati wa utoto wake (2 Nefi 2:1). Je, unadhani ushuhuda wa Lehi katika 2 Nefi 2:1–3, 6–25 ungewezaje kuwa wa thamani kwa Yakobo. Kwa nini ni wa thamani kwako? Tafuta maneno au virai ambavyo unaviona vina nguvu maalumu. Je, ni kwa namna gani Mungu ameyafanya majaribu yako yawe faida kwako? (Ona 2 Nefi 2:2.)

Ona pia Warumi 8:28; Dale G. Renlund, “Kukosa Haki Kunakokasirisha,” Liahona, Mei 2021, 41–45.

2 Nephi 2:15–29

Anguko na Upatanisho wa Yesu Kristo ni sehemu muhimu za mpango wa Baba wa Mbinguni.

Watu wengi huamini kwamba lile Anguko lilikuwa ni janga tu na kwamba Adamu na Hawa walifanya kosa la kudumu wakati walipochagua kula tunda. Katika 2 Nefi 2:15–28, Lehi anafundisha kweli za ziada kuhusu Anguko—na kuhusu ukombozi kupitia Kristo. Unapochunguza mistari hii, tengeneza orodha ya kweli zinazohusu kile kilichotokea katika Bustani ya Edeni. Maswali kama haya yangeweza kusaidia:

  • Je, ni kwa nini Anguko lilikuwa muhimu?

  • Je, ni jukumu lipi Yesu Kristo alilifanya ili kushinda matokeo ya Anguko?

  • Je, ni kwa jinsi gani uelewa sahihi wa Anguko hutusaidia tuelewe vyema uhitaji wetu wa Yesu Kristo?

Ona pia Dallin H. Oaks, “The Great Plan of Happiness,” Ensign, Nov. 1993, 72–75.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Picha
Yesu Kristo

Msifadhaike Mioyoni Mwenu, na Howard Lyon

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

2 Nefi 1:13, 15, 23

Yesu Kristo ananisaidia nishinde matokeo ya dhambi.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe mwaliko wa Lehi wa “kujifungua minyororo” ya dhambi, pengine mngeweza kufanya kazi pamoja kutengeneza mnyororo wa vipande vya karatasi. Kwenye vipande, watoto wako wangeweza kukusaidia kuandika baadhi ya vitu ambavyo Shetani hutujaribu tuvifanye. Kisha mngeweza kusoma pamoja 2 Nefi 1:13, 15, 23 wakati wakiigiza baadhi ya virai kwenye mistari hii—ikijumuisha kujifungua kutoka kwenye mnyororo wa karatasi. Ni kwa jinsi gani dhambi ni kama mnyororo? Je, ni kwa jinsi gani Yesu hutusaidia sisi “tujifungue minyororo” ya dhambi?

2 Nefi 1:20

Ninabarikiwa pale ninapotii amri za Mungu.

  • Je, ingeweza kuwa ya msaada kwa watoto wako kulinganisha amri za Mungu na viatu, kofia, glavu au kitu kingine chochote ambacho kinatulinda? Pengine ungeweza kuwaruhusu wajaribu baadhi ya hivyo vitu wakati ukizungumza kuhusu jinsi gani amri zinatulinda. Kisha ungeweza kusoma 2 Nefi 1:20, na kusisitiza kwamba “tutafanikiwa au (kubarikiwa au kulindwa) pale tunapotii amri. Shiriki uzoefu wakati ulipobarikiwa au kulindwa kwa kufuata amri.

  • Ili kuonesha tofauti kati ya kufanikiwa na kutengwa kutoka kwenye uwepo wa Mungu (ona 2 Nefi 1:20), wewe pamoja na watoto wako mngeweza kuangalia mmea wenye afya na jani au tawi ambalo limekatwa kutoka kwenye mmea. Kisha watoto wako wangeweza kupitia chaguzi ambazo Nefi na kaka zake walizifanya (ona 1 Nefi 2:11–16; 3:5–7; 18:9–11). Ni yapi yalikuwa matokeo ya chaguzi hizi? Ni chaguzi zipi hutusaidia sisi tubaki tukiwa tumeunganika na Mungu?

2 Nefi 2:11, 16:27

Mungu amenipa haki ya kujiamulia.

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe kile ambacho Lehi alikifundisha kuhusu upinzani na kufanya chaguzi, mngeweza kucheza mchezo ambapo wewe unasema neno (kama vile nuru) na watoto wako wanasema kinyume chake (giza). Wasaidie wajifunze kwa nini upinzani ni sehemu ya mpango wa Mungu wakati mkisoma pamoja 2 Nefi 2:11, 16. Kisha ungeweza kushiriki hadithi ya mtoto ambaye anajaribiwa kufanya uchaguzi usio sahihi. Watoto wako wangeweza kushiriki kinyume cha uchaguzi usio sahihi ni nini na waigize.

  • Ili wajifunze kuhusu tofauti kati ya “uhuru” na “utumwa” (2 Nefi 2:27) watoto wako wangeweza kuchora picha za mnyama kwenye uzio na mnyawa kwenye mazingira yake halisi. Je, ni mnyama yupi yuko huru? Waalike watoto waoneshe picha sahihi wakati unaposoma neno “huru” katika 2 Nefi 2:27. Shuhudia kwamba Yesu Kristo hutuweka huru.

  • Imbeni pamoja wimbo kama “Chagua Jema” (Nyimbo za Dini, na. 135). Je, tunajifunza nini kutokana na wimbo huu kuhusu kufanya chaguzi?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Familia ya Lehi ikiwa imepiga magoti ufukoni

Lehi na Watu Wake Wanawasili katika Ulimwengu Mpya, na Clark Kelley Price

Chapisha