“Februari 12–18: ‘Tuliishi kwa Furaha.’ 2 Nefi 3–5,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)
“Februari 12–18. 2 Nefi 3–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)
Februari 12–18: “Tuliishi kwa Furaha”
2 Nefi 3–5
Kwa kusoma 1 Nefi, ungeweza kupata msukumo kwamba Nefi kwa namna fulani alikuwa mkubwa kuliko maisha. “Mkubwa kiumbo” vyote kimwili na kiroho (1 Nefi 2:16), alionekana kutoyumbishwa na majaribu aliyokabiliana nayo. Au angalau hivyo ndivyo tunavyoweza kudhani. Wakati imani ya Nefi ilikuwa ya kustaajabisha, maneno yake ya upole katika 2 Nefi 4 yanafunua kwamba hata watu waaminifu sana wakati mwingine wanahisi “kuhuzunishwa” na “kuzongwa kirahisi” na majaribu. Hapa tunamwona mtu fulani anayejaribu, anayetaka kuwa mwenye furaha, lakini ambaye “moyo wake una maumivu kwa sababu ya dhambi [zake].” Tunaweza kujifananisha na hayo na kwenye msimamo wenye tumaini ambao unafuata: “Walakini, ninajua ni nani ninayemwamini” (ona 2 Nefi 4:15–19).
Wakati Nefi na watu wake walipojifunza kuishi “kwa furaha” (2 Nefi 5:27), walijifunza pia kwamba furaha haiji kirahisi au pasipo vipindi vya huzuni. Hatimaye inakuja kutokana na kumtumaini Bwana, “mwamba wa haki [yetu]” (2 Nefi 4:35)
Mawazo kwa ajili ya kujifunza Nyumbani na Kanisani
Joseph Smith aliteuliwa na Mungu kurejesha injili.
Lehi alishiriki na Yusufu, mtoto wake unabii ulitolewa na Yusufu wa Misri. Unabii ulikuwa juu ya “mwonaji mteule” wa baadaye, Joseph Smith. Ni kipi mistari 6–24 inakisema kwamba Joseph Smith, angekifanya ili kuwabariki watu wa Mungu? Fikiria jinsi ambavyo kazi ya Joseph Smith imekuwa “ya thamani kuu” kwako. Ungeweza kupata baadhi ya mawazo kutoka kwenye video kuhusu Joseph Smith kwenye “Prophets of the Restoration” mkusanyiko katika Gospel Library. Fikiria kuhusu maswali kama haya, na zingatia kuandika majibu yako:
-
Je, unajua nini kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa sababu ya kile Joseph Smith alichokifundisha?
-
Ni kwa namna gani maisha yako ni tofauti kwa sababu ya kile ambacho Bwana amekirejesha kupitia Joseph Smith?
-
Je, Maisha yako yangekuwa ya namna gani kama Urejesho usingefanyika?
Sehemu moja muhimu ya misheni ya Joseph Smith ilikuwa ni kukileta Kitabu cha Mormoni. Je, unajifunza nini kutoka kwenye mlango huu kuhusu kwa nini Kitabu cha Mormoni ni cha muhimu? Hususani, ungeweza kutafuta sababu kutoka mistari 7, 11–13, 18–24.
Ona pia Tafsiri ya Joseph Smith ya, Mwanzo 50:24–38 (katika kiambatisho cha Biblia); Mada za Injili, “Joseph Smith,” Gospel Library.; “Sifa kwa Aliyenena na Bwana,” Nyimbo za Dini, na. 17.
“Ewe Bwana, nimekuamini.”
Nefi alisema kwamba yeye “angeandika mambo ya nafsi yake” (mstari wa 15). Unaposoma kile alichokiandika katika 2 Nefi 4:15–35, jiulize, “Vitu vya nafsi yangu ni vipi?” Fikiria kuviandika, kama Nefi alivyofanya na uvishiriki na watu uwapendao.
Kwa kuona jinsi Nefi alivyopata faraja wakati alipohisi kuzidiwa na woga kunaweza kukusaidia wewe wakati unapokuwa na hisia sawa na hizo. Tafuta katika mistari 15–35 kwa ajili ya aya zinazokuletea faraja. Je, unamjua mtu yeyote ambaye angepokea faraja kwenye aya hizi?
Ona pia Ronald A. Rasband, “Vitu vya Nafsi Yangu,” Liahona, Nov. 2021, 39–41.
Ninaweza kupata furaha kwa kuishi Injili ya Yesu Kristo.
Unadhani inamaanisha nini kuwa na furaha? Nefi aliandika kwamba watu wake “waliishi kwa furaha” (2 Nefi 5:27). Ungeweza kutafuta chaguzi ambazo Nefi na watu wake walizifanya ambazo ziliwasaidia wawe na furaha (ona, kwa mfano 2 Nefi 5:6, 10–17). Je, ni kitu gani kinaweza kukusaidia ujenge maisha ya furaha kama watu wa Nefi?
Ni laana ipi ilikuja juu ya Walamani?
Katika siku ya Nefi laana ya Walamani ilikuwa kwamba “waliondolewa kutoka katika uwepo [wa Bwana] … kwa sababu ya uovu wao” (2 Nefi 5:20–21). Hii ilimaanisha kwamba Roho wa Bwana aliondolewa kutoka katika maisha yao. Wakati Walamani walipoikubali injili ya Yesu Kristo baadaye, “laana ya Mungu haikuwafuata tena” (Alma 23:18).
Kitabu cha Mormoni pia kinasema kwamba alama ya ngozi nyeusi ilikuja juu ya Walamani baada ya Wanefi kujitenga nao. Asili na mwonekano wa alama hii havijajulikana kikamilifu. Mwanzoni alama hiyo iliwatofautisha Walamani na Wanefi. Baadaye, kadiri Wanefi na Walamani walivyopitia vipindi vya uovu na utakatifu, alama ikawa haina maana.
Manabii wanathibitisha katika siku zetu kwamba ngozi nyeusi siyo ishara ya kutopendwa au laana. Rais Russell M. Nelson alitangaza: “Ninakuhakikishia kwamba kukubalika kwako mbele za Mungu hakuamuliwi kwa rangi ya ngozi yako. Kupendelewa au kutopendelewa na Mungu kunategemea kujitoa kwako kwa Mungu na amri Zake na siyo rangi ya ngozi yako” (“Acha Mungu Ashinde,” Liahona, Nov. 2020, 94).
Kama Nefi, Bwana “hamkatazi yeyote kuja kwake, weusi, na weupe, wafungwa na walio huru, waume kwa wake; … wote wako sawa mbele za Mungu” (2 Nefi 26:33).
Ona pia “Till We All Come in the Unity of the Faith” (video), Maktaba ya Injili.
Mawazo Kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Joseph Smith alikuwa nabii.
-
Fikiria namna utakavyowafundisha watoto wako kuhusu kazi kuu ambayo Mungu aliikamilisha kupitia Joseph Smith. Kwa kuanza, ungeweza kuwasaidia watoto watafute neno “mwonaji” katika 2 Nefi 3:6 na eleza kwamba manabii wanaitwa waonaji kwa sababu Baba wa Mbinguni huwasaidia waone mambo tusiyoweza kuyaona. Shiriki kwa nini wewe unayo shukrani kwa kuwa na mwonaji akiliongoza Kanisa.
-
Kitabu cha Sanaa za Injili kina picha kadhaa ambazo ungeweza kutumia kufundisha kuhusu kazi ya Mungu kupitia Joseph Smith (ona picha 89–95). Waruhusu watoto washiriki kile wanachokijua kuhusu picha hizi. Kwa nini Joseph Smith anaitwa “mwonaji bora”? Ni kitu gani Joseph Smith alikifanya kilicho “cha thamani kuu”? (mstari wa 7).
Ninapenda “vitu vya Bwana.”
-
Je, ni kitu gani kinatufanya sisi tuwe na furaha? Fikiria kusoma pamoja mistari kutoka 2 Nefi 4 ili kujua kilichompendeza Nefi au kilichomfanya awe na furaha (ona mistari 15–16, 20–25, 34–35). Katika ujumbe wake “Mambo ya Nafsi Yangu,” Mzee Ronald A. Rasband alishiriki “vitu saba vya Bwana” ambavyo ni vya thamani kwake (Liahona, Nov. 2021, 39–41). Pengine ungeweza kupitia orodha yake na kuzungumza kuhusu “vitu vya Bwana” ambavyo ni vya thamani kwako.
-
2 Nefi 5 inafafanua vitu ambavyo viliwasaidia Wanefi waishi “kwa furaha” (mstari wa 27). Ungeweza kutoa baadhi ya maneno au picha ambazo zinawakilisha vitu hivi na wasaidie watoto wako waoanishe mistari hii kwenye Mlango wa 5. Baadhi ya mifano hujumuisha familia (mstari wa 6), amri za Mungu (mstari wa 10), maandiko (mstari wa 12), kazi (mstari wa 15 na 17), mahekalu (mstari wa 16), na miito Kanisani (mstari wa 26). Ni kwa namna ipi vitu hivi hutuletea furaha?
Hekalu ni nyumba ya Bwana.
-
Wakati ukisoma 2 Nefi 5:15–16 kwa watoto wako, wangeweza kujifanya wanamsaidia Nefi kujenga hekalu. Ungeweza pia kuwaonesha picha za majengo tofauti tofauti, ikijumuisha hekalu. Je, mahekalu yana utofauti gani na majengo mengine? Ambianeni kwa nini hekalu ni muhimu kwenu (ona pia “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95).