Njoo, Unifuate 2024
Desemba 2–8: “Kuwaweka katika Njia Nzuri.” Moroni 1–6


“Desemba 2–8: ‘Kuwaweka katika Njia Nzuri’ Moroni 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Desemba 2–8. Moroni 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Alma akibatiza watu katika Maji ya Mormoni

Minerva Teichert (1888–1976), Alma Anabatiza katika Maji ya Mormoni, 1949–1951, mafuta juu ya ubao, 35 7/8 × 48 inchi. Jumba la Makumbusho la sanaa la Chuo kikuu cha Brigham Young, 1969

Desemba 2–8: “Kuwaweka katika Njia Nzuri”

Moroni 1–6

Baada ya kumaliza kumbukumbu ya baba yake juu ya Wanefi na ufupisho wa kumbukumbu ya Wayaredi, Moroni alidhani kwamba kazi yake ya kutunza kumbukumbu ilikuwa imekamilika (ona Moroni 1:1). Kulikuwa na nini cha ziada cha kusema kuhusu mataifa mawili yaliyokuwa yameangamizwa kabisa? Lakini Moroni alikuwa ameona siku zetu (ona Mormoni 8:35), na alitiwa msukumo “kuandika vitu vingine vichache, kwamba pengine vingekuwa vya manufaa … katika siku zijazo” (Moroni 1:4). Alijua kwamba ukengeufu uliotapakaa ulikuwa unakaribia, ukija na machafuko kuhusu ibada za ukuhani na kuhusu dini kwa ujumla. Hii yaweza kuwa sababu ya yeye kutoa maelezo bayana kuhusu sakramenti, ubatizo, kutunukia kipawa cha Roho Mtakatifu, na baraka za kukusanyika pamoja na waumini wenzetu “kuwaweka [kila mmoja] katika njia nzuri, … wakitegemea tu katika nguvu ya wokovu ya Kristo, ambaye alikuwa mwanzilishi na mtimizaji wa imani [yetu]” (Moroni 6:4). Utambuzi wa thamani kama huu unatupatia sababu ya kuwa na shukrani kwamba Bwana alihifadhi uhai wa Moroni ili aweze “kuandika vitu zaidi” (Moroni 1:4).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Moroni 1

Ninaweza kumfuata Yesu Kristo licha ya upinzani.

Unaposoma Moroni 1, ni kipi kinachokutia msukumo kuhusu uaminifu wa Moroni kwa Bwana na wito wake? Ni zipi baadhi ya njia mtu angeweza “kumkana Kristo”? (Moroni 1:2–3). Tafakari jinsi unavyoweza kuwa mwaminifu kwa Yesu Kristo, hata wakati unapopitia majaribu na upinzani.

Moroni 2–6

Ibada za ukuhani lazima zisimamiwe kulingana na Bwana anavyoamuru.

Moroni alikuwa akikimbia kuokoa maisha yake wakati alipokuwa akiandika sura hizi. Kwa nini yeye alijisumbua kuandika kuhusu maelezo ya kina kama vile jinsi ya kufanya ibada? Tafakari kuhusu hili unaposoma Moroni 2–6. Je, ni kwa nini unadhani maelezo haya ya kina ni muhimu kwa Bwana? Hapa kuna baadhi ya maswali ambayo yangeweza kuongoza kujifunza kwako:

Uthibitisho (Moroni 2; 6:4).Ni kipi maelekezo ya Mwokozi katika Moroni 2:2 yanakufundisha kuhusu ibada ya uthibitisho? Ni kwa jinsi gani ungeweza kueleza kile inachomaanisha “kupokelewa na kusafishwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”? (Moroni 6:4).

Kutawazwa kwenye ukuhani (Moroni 3).Ni kipi unakipata katika sura hii ambacho kinaweza kumsaidia mtu ajiandae kutawazwa kwenye ukuhani? Je, ni kipi unakipata ambacho kinaweza kumsaidia mtu ajiandae kufanya utawazo?

Sakramenti (Moroni 4–5; 6:6).Unaweza kufanya nini ili kuifanya sakramenti kuwa tukio muhimu la kiroho la wiki yako?

Ubatizo (Moroni 6:1–3).Unafanya nini ili kuendelea kukidhi vigezo vya ubatizo?

Picha
msichana akipokea baraka

Yesu alifundisha jinsi ambavyo ibada zinapaswa kufanyika

Kulingana na kile ulichojifunza, ni jinsi gani utabadili jinsi unavyofikiri kuhusu, kushiriki katika, au kuwaandaa wengine kwa ajili ya ibada hizi?

Ona pia Mafundisho na Maagano 84:20.

Fanya-Igizo. Njia moja kuu ya kukumbuka kile unachojifunza ni kukielezea kwa wengine. Kwa mfano, jaribu matukio ya kuigiza nafasi kama haya: Rafiki hana uhakika kama yuko tayari kubatizwa. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia Moroni 6 ili umsaidie?

Moroni 4–5

Kupokea sakramenti hunisaidia nisogee karibu zaidi na Yesu Kristo.

Kuna uwezekano umesikia sala za sakramenti mara nyingi, lakini Je, ni mara ngapi unatafakari kwa makini kuhusu maneno yanamaanisha nini? Pengine ungeweza kujaribu kuandika sala mbili za sakramenti kutoka kwenye kumbukumbu yako. Kisha linganisha kile ulichoandika na Moroni 4:3 na 5:2. Je, umegundua chochote kuhusu sala hizi ambacho hukuwa umekigundua hapo awali?

Fikiria kujumuisha wimbo wa sakramenti katika kujifunza kwako, kama vile “Kwa Ukumbusho wa Kristo” (Nyimbo za Dini, na. 105).

Moroni 6:4–9

Picha
ikoni ya seminari
Wafuasi wa Yesu Kristo hujali ustawi wa nafsi za wengine.

Uchaguzi wa kumfuata Kristo ni wa mtu binafsi, lakini waaminio wenzetu wanaweza kutusaidia tuwe “katika njia nzuri” (Moroni 6:4–5). Ni kipi waumini wa Kanisa katika nyakati za Moroni walifanya ili kuimarishana? Unaposoma Moroni 6:4–9, tafakari baraka ambazo zinakuja kutokana na “kuhesabiwa miongoni mwa watu wa kanisa la Kristo” (Moroni 6:4).

Ungeweza pia kuwafikiria watu ambao wanahudhuria katika kata yako au tawi lako. Je, una mtu yeyote ambaye ana mahitaji maalumu ya upendo wako—pengine mtu mpya au yule aliyeanza kurudi hivi karibuni? Ni kwa jinsi gani wewe ungesaidia kufanya uzoefu wao kanisani uwe kama ule Moroni alioueleza? (Kwa mawazo, ona My Covenant Path au “Strengthening New Members” video katika Maktaba ya Injili). Ungeweza kupata baadhi ya miongozo katika sehemu ya I ya ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Hitaji la Kanisa” (Liahona, Nov. 2021, 24–25).

Unapotafakari kile inachomaanisha “kulishwa na neno zuri la Mungu” (Moroni 6:4), ingesaidia kufikiria kuhusu lishe ambayo mimea au mtoto mchanga huhitaji—na nini hutokea kama ikipuuzwa. Chunguza Moroni 6:4–9 kwa ajili ya mawazo kuhusu jinsi unavyoweza kusaidia “kuwalisha” wengine kiroho. Ni kwa jinsi gani wafuasi wenzako wamesaidia kukulisha?

Inawezekana isiwe wazi kwa kila mtu kwa nini ni muhimu “kuhesabiwa miongoni mwa watu wa kanisa la Kristo” na “kukutana pamoja kila mara” katika mikutano ya Kanisa. Ni kwa jinsi gani ungeweza kufafanua kwa nini unashukuru kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo? (ona sehemu zingine za ujumbe wa Rais Oaks “Hitaji la Kanisa).

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Moroni 2–6

Roho Mtakatifu ni zawadi takatifu.

  • Roho Mtakatifu au Roho ametajwa mara kadhaa katika Moroni 2–6. Pengine ungeweza kuwaomba watoto wako watafute kila mstari ambao umemtaja Roho, wasome mistari hii, na waorodheshe mambo ambayo wanajifunza kuhusu Roho Mtakatifu. Mngeweza pia kushiriki ninyi kwa ninyi baadhi ya uzoefu wakati ambapo mlihisi ushawishi wa Roho.

Moroni 4–5

Ninapokea sakramenti kuonesha kwamba daima nitamkumbuka Yesu Kristo.

  • Kusoma sala za sakramenti pamoja na watoto wako kungeweza kuongoza kwenye mjadala kuhusu jinsi ya kuwa na uzoefu ulio wa maana zaidi kwenye sakramenti. Ungeweza kuwasaidia wafikirie kwamba rafiki anakuja kwenye mkutano wa sakramenti kwa mara ya kwanza. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumueleza rafiki sakramenti ni nini na kwa nini ni takatifu? Wahimize watoto wako watumie chochote kutoka Moroni 4 au 5 katika maelezo yao. Watoto wadogo wangeweza kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii au Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 108.

  • Fikiria kuimba wimbo kwa pamoja ambao unawasaidia watoto wako wafikirie kuhusu Mwokozi (kama vile “Reverently, Quietly, Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 26). Ungeweza pia kufanya zoezi la kuketi kwa staha wakati wa sakramenti.

Moroni 6:1–3

Ninaweza kujiandaa kwa ajili ya kubatizwa.

  • Ni yupi anaweza kubatizwa? Wasaidie watoto wako wapate majibu kwa swali hili katika Moroni 6:1–3. Inamaanisha nini kuwa na “moyo uliovunjika na roho iliyopondeka”? (Moroni 6:2). Ni kwa jinsi gani hii hutusaidia tujiandae kwa ajili ya ubatizo? Fikiria kuwaambia watoto wako jinsi gani wewe ulijiandaa kubatizwa.

Moroni 6:4–6, 9

Tunakwenda kanisani kupokea sakramenti na kusaidiana sisi kwa sisi.

  • Je, watoto wako wanajua kwa nini wewe unapenda kwenda kanisani? Kusoma Moroni 6:4–6, 9 kunaweza kukupa fursa ya kujadili pamoja baadhi ya mambo tunayofanya kanisani. Pengine wangeweza kuchora picha zao wenyewe wakifanya mambo hayo (kama vile kusali, kufundisha, kuimba, na kupokea sakramenti).

  • Baada ya kusoma Moroni 6:4 pamoja, wewe na watoto wako mngeweza kutazama picha au mifano ya vyakula vya lishe na kulinganisha kuilisha miili yetu kwa “kulishwa na neno zuri la Mungu.” Pia mnaweza kutazama video “Children Sharing the Gospel” (Maktaba ya Injili).

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Moroni akijificha pangoni

Moroni ndani ya Pango, na Jorge Cocco

Chapisha