Njoo, Unifuate 2024
Desemba 9–15: “Kristo Akuinue Juu.” Moroni 7–9


Desemba 9–15: ‘Kristo Akuinue Juu.’ Moroni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Desemba 9–15. Moroni 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Moroni akiandika kwenye mabamba ya dhahabu

Minerva Teichert (1888–1976), Moroni: Mnefi wa Mwisho, 1949–1951, mafuta juu ya ubao, 34 3/4 × 47 inchi. Jumba la Makumbusho la sanaa la Chuo kikuu cha Brigham Young, 1969

Desemba 9–15: “Kristo Akuinue Juu”

Moroni 7–9

Kabla ya Moroni kuhitimisha kumbukumbu tunayoijua leo kama Kitabu cha Mormoni kwa maneno yake ya mwisho, alishiriki jumbe tatu kutoka kwa baba yake, Mormoni: waraka kwa “wafuasi wa imani ya Kristo ” (Moroni 7:3) na nyaraka mbili ambazo Mormoni alikuwa amemuandikia Moroni. Pengine Moroni alizijumuisha jumbe hizi katika Kitabu cha Mormoni kwa sababu aliona kabla mifanano baina ya hatari za siku zake na zetu. Wakati maneno haya yalipoandikwa, Wanefi walikuwa wakigeuka mbali na Mwokozi. Wengi wao walikuwa “wamepoteza upendo wao, mmoja kwa mwingine” na walifurahia “kila kitu isipokuwa kile ambacho ni chema” (Moroni 9:5, 19). Na bado Mormoni alipata sababu ya kuwa na tumaini, akitufundisha kwamba tumaini haimaanishi kupuuza au kuwa mshamba kuhusu matatizo ya ulimwengu. Tumaini inamaanisha kuwa na imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, ambao uwezo wao ni mkubwa na wa milele zaidi kuliko matatizo haya. Inamaanisha “[kushikilia] kila kitu kizuri” (Moroni 7:19). Inamaanisha kuruhusu Upatanisho wa Yesu Kristo “na matumaini ya utukufu wake na uzima wa milele, viwe katika akili yako” (Moroni 9:25).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Moroni 7:12–20

Nuru ya Kristo inanisaidia nijue kati ya ukweli na kosa.

Watu wengi walijiuliza, “Ni kwa jinsi gani ninaweza kujua kama msukumo unatoka kwa Mungu au unatokana na mawazo yangu mwenyewe?” au “Kwa udanganyifu mwingi wa leo, ni kwa jinsi gani ninaweza kujua ni kipi kilicho sahihi au kosa?” Maneno ya Mormoni katika Moroni 7 yanatupatia kanuni kadhaa tunazoweza kutumia kujibu maswali haya. Zitafute hususani katika mistari 12–20. Ungeweza kutumia kweli hizi zikusaidie kutathmini jumbe unazokutana nazo na uzoefu ulio nao wiki hii.

Ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Light, Light of Christ,” Maktaba ya Injili; “Patterns of Light: Discerning Light” (video) Maktaba ya Injili.

Moroni 7:20–48

Kwa sababu ya Yesu Kristo, ninaweza “kushikilia kila kitu kizuri.”

Mormoni aliuliza swali ambalo linaonekana kuwa muhimu sana leo hii: “Inawezekanaje [kushikilia] kila kitu kizuri?” (Moroni 7:20). Kisha yeye alifundisha kuhusu imani katika Yesu Kristo, tumaini na hisani. Unaposoma mistari 20–48, tafuta jinsi kila sifa inavyokusaidia upate na “ushikilie” uzuri ambao huja kutoka kwa Yesu Kristo. Kwa nini sifa hizi ni muhimu kwa mfuasi wa Yesu Kristo?

Ona pia “Mormon’s Teachings about Faith, Hope, and Charity” (video), Maktaba ya Injili.

Moroni 7:44–48

Picha
ikoni ya seminari
“Hisani ni upendo msafi wa Kristo.”

Mormoni aliona kwamba imani na tumaini katika Yesu Kristo hutuongoza kuwa na hisani. Lakini hisani ni nini? Ungeweza kuandika Hisani ni … na kisha usome Moroni 7:44–48, ukitafuta maneno au virai ambavyo vingeweza kukamilisha sentensi. Unapokamilisha, fikiria kubadilisha neno Hisani kwa jina Yesu Kristo. Je, hii inakufundisha nini juu ya Mwokozi? Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ameonesha upendo Wake safi? Fikiria mifano kutoka kwenye maandiko na maisha yako mwenyewe.

Rais Dallin H. Oaks alisema: “Sababu ya hisani kutokushindwa kamwe na sababu ya hisani kuwa kuu zaidi ya hata vitendo muhimu kabisa vya wema … ni kwamba hisani, ‘upendo msafi wa Kristo’ (Moroni 7:47), si kitendo bali ni hali au hali ya kuwa. … Hisani ni kitu ambacho mtu huwa” (“Changamoto ya Kuwa,” Ensign, Nov. 2000, 34). Ili kuunga mkono kauli hii, ungeweza kusoma ujumbe wa Mzee Massimo De Feo “Upendo Safi: Ishara Halisi ya Mfuasi wa Kweli wa Yesu Kristo” (Liahona, Mei 2018, 81–83) Je, ni kwa namna gani hisani inaathiri ufuasi wako? Ni kwa jinsi gani unaweza “kuambatana na hisani”? (mstari wa 46).

Ona pia 1 Wakorintho 13:1–13; Etheri 12:33–34; “Niwapendavyo,” Nyimbo za Dini, na. 185; “Charity: An Example of the Believers” (video), Maktaba ya Injili; Mada za Injili, “Hisani,” Maktaba ya Injili.

Tumia masomo kwa vitendo. Pengine kufikiria kigoda cha miguu mitatu kunaweza kukusaidia uelewe zaidi kuhusu uhusiano kati ya imani, tumaini, na hisani (ona Dieter F. Uchtdorf, “The Infinite Power of Hope,” Liahona, Nov, 2008, 21–24).

Moroni 9:3–5

Hasira inatuongoza kwenye huzuni na mateso.

Kinyume na ujumbe wa Mormoni wa upendo katika Moroni 7:44–48, waraka wa pili wa Mormoni kwa Moroni ulijumuisha maonyo dhidi ya kitu ambacho watu wengi wanataabika nacho leo—hasira. Kulingana na Moroni 9:3–5, ni yapi baadhi ya matokeo ya hasira za Wanefi? Ni maonyo yapi tunapata katika mistari 3–5, 18– 20, 23?

Ona pia Gordon B. Hinckley, “Slow to Anger,” Liahona, Nov. 2007, 62–66.

Moroni 9:25–26

Ninaweza kuwa na tumaini kwa Kristo bila kujali hali yangu.

Baada ya kueleza uovu ambao alikuwa ameuona, Mormoni alimwambia mwanaye asihuzunike. Ni kipi kinakuvutia kuhusu ujumbe wa Mormoni wa tumaini? Inamaanisha nini kwako kwa Kristo “kukuinua [wewe] juu? Ni sifa zipi za Kristo na kanuni zipi za injili Yake “ziko katika akili yako” na hukupa tumaini? (Moroni 9:25).

Ona pia Russell M. Nelson, “Shangwe na Kunusurika KirohoLiahona, Nov. 2016, 81–84.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Moroni 7:33

Nikiwa na imani katika Yesu Kristo, ninaweza kufanya chochote Yeye anachohitaji mimi nifanye.

  • Fikiria kuangalia pamoja picha chache ambazo zinaonesha mtu kutoka kwenye maandiko akitimiza kitu muhimu (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa za Injili, na.19, 70, 78,81). Ni kwa jinsi gani kuwa na imani katika Kristo kunaleta tofauti katika mifano hii? Wewe na watoto wako kisha mngeweza kusoma Moroni 7:33, mkitafuta kile tunachoweza kufanya wakati tunapokuwa na imani katika Yesu Kristo. Mngeweza pia kushiriki ninyi kwa ninyi baadhi ya uzoefu wakati ambapo Mungu aliwabariki kwa kuwa na nguvu za kufanya mapenzi Yake.

Moroni 7:41

Kuamini katika Yesu Kristo kunaweza kunipa tumaini.

  • Unapowasomea watoto Moroni 7:41, pengine wangenyanyua mikono yao wakati wanaposikia jambo ambalo Mormoni alisema tunapaswa kulitumainia. Waambie kuhusu tumaini ulilonalo kwa sababu ya Yesu Kristo.

  • Wewe na watoto mngeweza kumfikiria mtu ambaye anaweza kuwa ana wakati mgumu kwenye kitu fulani. Pengine watoto wako wangechora picha kwa ajili ya mtu yule ambayo inaweza kumkumbusha kuwa na tumaini katika Yesu Kristo.

Moroni 7:40–41; 9:25–26

Ninaweza kuwa na tumaini katika Yesu Kristo, hata wakati wa majaribu magumu.

  • Wafundishe watoto wako kuhusu tumaini katika Yesu Kristo, ungeweza kujaza chombo kitupu kwa maji na dondosha vitu viwili ndani yake—kimoja kinachoelea na kingine kinachozama. Mnaposoma pamoja Moroni 7:40–41 na 9:25–26, watoto wako wangeweza kutafuta kitu ambacho tumaini hutufanyia sisi. Kisha wangeweza kufananisha kitu kinachoelea na mtu mwenye tumaini katika Kristo. Ni kwa jinsi gani Yeye “hutuinua [sisi] juu” wakati tunapokabiliwa na majaribu magumu? Wasaidie watoto wako wafikirie njia wanazoweza kumweka Mwokozi na mafundisho Yake ya kutia moyo “katika akili [zao] milele.”

Moroni 7:45–48

“Hisani ni upendo msafi wa Kristo.”

  • Wimbo kuhusu upendo, kama vile “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136), unaweza kuanzisha mjadala kuhusu hisani ni nini. Ungeweza kusoma au kufanya muhtasari wa Moroni 7:47 na waalike watoto wachore picha zao wenyewe wakionesha upendo kwa mtu mwingine. Pendekeza kwamba waweke picha zao mahali ambapo zitawakumbusha wao kuwapenda wengine kama Yesu anavyowapenda wengine.

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwapa msukumo watoto watafute na wakuze upendo msafi wa Kristo katika maisha yao? Pengine ungeweza kuwasaidia wafikirie njia ambazo Yesu alionesha hisani (ona, kwa mfano, Luka 23:34; Yohana 8:1–11; Etheri 12:33–34). Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano Wake?

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Yesu Kristo

Picha ya Kristo Mwokozi, na Heinrich Hofmann

Chapisha