Njoo, Unifuate
Juni 9–15: “Mimi Daima Nipo Pamoja na Waaminifu” Mafundisho na Maagano 60–63


“Juni 9–15: ‘Mimi Daima Nipo Pamoja na Waaminifu’: Mafundisho na Maagano 60–63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 60–63,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

kambi karibu na Mto Missouri

Utondoti kutoka Kambi huko Missouri, na Bryan Mark Taylor

Juni 9–15: “Mimi Daima Nipo Pamoja na Waaminifu”

Mafundisho na Maagano 60–63

Mapema Agosti 1831, Joseph Smith na wazee wengine wa Kanisa walikuwa wakijiandaa kurudi Kirtland baada ya matembezi mafupi kwenye “ardhi ya Sayuni” (Mafundisho na Maagano 59:3). Bwana alikuwa amewataka wahubiri injili wakati wa safari yao (ona Mafundisho na Maagano 52:10), na baadhi yao walifanya hivyo kwa bidii sana. Lakini wengine walisitasita. “Wanaficha vipaji ambavyo nimewapa,” Bwana alisema, “kwa sababu ya kumwogopa mwanadamu” (Mafundisho na Maagano 60:2). Wengi wetu wanajua jinsi wazee hawa walivyohisi. Hata ingawa tunaipenda injili, woga na mashaka vinaweza kutuzuia tusiishiriki. Lakini Bwana ni mwenye rehema. Yeye “anajua udhaifu wa mwanadamu na namna ya [kutusaidia] (Mafundisho na Maagano 62:1). lililoenea kote katika ufunuo huu kwa wamisionari wa mwanzo ni hakikisho ambalo linaweza kutusaidia tushinde hofu zetu na mapungufu yetu: “Mimi ninaweza kukufanya kuwa mtakatifu.” “Wenye mwili wako katika mikono yangu.” “Mimi daima nipo pamoja na waaminifu.” Na “Yule aliye mwaminifu na mwenye kustahimili ataushinda ulimwengu.” (Mafundisho na Maagano 60:7; 61:6; 62:9; 63:47.)

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 60; 62

Ninaweza kushiriki upendo wangu na ushuhuda wangu juu ya Yesu Kristo.

Ni kwa jinsi gani ushuhuda wako wa injili ni kama “kipaji,” au hazina kutoka kwa Mungu? Ni katika njia zipi sisi wakati mwingine “huficha kipaji [chetu]”? (Mafundisho na Maagano 60:2; ona pia Mathayo 25:14–30).

Ni ujumbe upi wa kutia moyo kutoka kwa Bwana unaupata katika sehemu ya 60 na 62? Ni kwa jinsi gani jumbe hizi zinajenga kujiamini kwako katika kushiriki injili? Unapotafakari maswali haya, fikiria kuimba au kusoma maneno ya “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168). Unajifunza nini kutoka kwenye wimbo huu wa watoto kuhusu kushiriki injili?

Ona pia “Sharing the Gospel” mkusanyiko katika Maktaba ya Injili.

kushiriki injili ndani ya basi

Ninaweza kuwa muwazi kuhusu kushiriki imani yangu katika Kristo.

Mafundisho na Maagano 60:2–4; 61:1–2, 20, 36–38; 62:1, 6

Maandiko yanafundisha juu ya Yesu Kristo.

Kama Yeye alivyowaelekeza wamisionari Wake, Bwana alifunua kweli muhimu kuhusu Yeye Mwenyewe. Tafuta kweli hizi katika Mafundisho na Maagano 60:2–4; 61:1–2, 20, 36–38; 62:1, 6. Ni hadithi zipi kutoka kwenye maandiko zinaonesha majukumu na sifa za Mwokozi ambazo umezipata? (ona kwa mfano, Yohana 8:1–11; Etheri 2:14–15).

Mafundisho na Maagano 62

Maamuzi yangu yanapaswa kuwa sawa na “hukumu na maelekezo ya Roho.”

Bwana hutupatia maelekezo kuhusu kweli za milele na kanuni za milele, lakini Yeye kila mara hutuacha sisi kuamua utondoti mahususi kuhusu jinsi ya kutenda juu ya kanuni hizi. Ni kwa jinsi gani unaona kanuni hii ikioneshwa katika Mafundisho na Maagano 62? (ona pia Mafundisho na Maagano 60:5; 61:22). Ni kwa jinsi gani umeiona kanuni hii katika maisha yako? Kwa nini ni vizuri kwetu kufanya baadhi ya maamuzi bila kumtarajia Mungu kutuambia nini hasa cha kufanya?

Ona pia Etheri 2:18–25; Mafundisho na Maagano 58:27–28.

Mafundisho na Maagano 63:7–12

Ishara huja kwa imani na kwa mapenzi ya Mungu.

Mwisho wa muhtasari huu, kuna kielelezo cha muujiza ambao kwa kina ulimvutia Ezra Booth: mkono wa Elsa Johnson uliponywa kimiujiza. Baada ya kuliona hilo, Ezra alikuwa na ari ya kubatizwa. Na bado, ndani ya miezi michache, Ezra alipoteza imani yake na kuwa mkosoaji wa Nabii. Hili lingewezekanaje, ukizingatia muujiza aliokuwa ameushuhudia?

Tafakari hili unaposoma Mafundisho na Maagano 63:7–12. Ni kweli zipi unajifunza kuhusu ishara na imani?

Ona pia Mathayo 16:1–4; Yohana 12:37; Mormoni 9:10–21; Etheri 12:12, 18.

Mafundisho na Maagano 63:16

ikoni ya seminari
Ninaweza kuwa msafi katika mawazo yangu na matendo yangu.

Katika Mafundiaho na Maagano 63:16, Mwokozi alithibitisha kile alichofundisha katika Agano Jipya—kwamba sheria ya usafi wa kimwili inapaswa kutawala si tu matendo yetu bali pia mawazo yetu (ona Mathayo 5:27–28). Unaposoma Mafundusho na Maagano 63:16, andika maonyo Mwokozi aliyotoa kuhusu mawazo ya tamaa. Ungeweza pia kutafakari kinyume cha kila onyo. Kwa mfano, ni yapi baadhi ya maneno au virai ambavyo ni kinyume cha woga? Ni baraka zipi zingine huja kutokana na kuwa na mawazo na matendo safi?

Watu wengi wanadhani viwango vya Bwana juu ya usafi wa mawazo na matendo vimepitwa na wakati au hata vinakandamiza. Ingeleta tofauti gani kama watoto wote wa Mungu wangejitahidi kuishi sheria hii? Ungeweza kutafuta majibu ya swali hili katika ujumbe wa Mzee David A. Bednar“Tunaamini Katika Kuwa Wasafi Kimwili” (Liahona, Mei 2023, 41–44) au “Mwili wako ni Mtakatifu” (Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mwongozo kwa ajili ya kufanya chaguzi, 23–26). Ni ujumbe upi wa tumaini unaoupata?

Hata wakati ambapo tunazijua baraka za kuwa wasafi kimwili katika mawazo na matendo yetu, hiyo haimaanishi kwamba ni rahisi. Ungeweza kuchukua muda kutafakari kile ambacho hufanya iwe vigumu kwetu kushika viwango vya Mwokozi vya usafi wa kimwili—na kile ambacho hufanya iwe rahisi. Ni vidokezo gani ungeweza kushiriki na wengine kuhusu nini cha kufanya unapojaribiwa kwa mawazo yasiyostahili?

Saidianeni. Moja ya baraka kubwa ya kukutana pamoja katika mikutano ya Kanisa na madarasa ya kanisa ni fursa ya kupata msaada kutoka kwa watakatifu wenzetu katika juhudi zetu za kumfuata Mwokozi. Wengi wetu wanakabiliana na changamoto zinazofanana, na uzoefu wetu wa pamoja unaweza kuwa nguvu kuu. Usiogope kukubali kwamba una changamoto. Shiriki na kila mmoja kile ambacho hukusaidia uishi sheria za Mungu na kushinda majaribu.

Ona pia Mafundisho na Maagano 121:45; Topics and Questions, “Virtue,” Maktaba ya Injili; “Standards: Sexual Purity and Modesty—True Confidence” (video), Maktaba ya Injili; AddressingPornography.ChurchofJesusChrist.org.

3:58

Standards: Sexual Purity and Modesty - True Confidence

Two young women share their secret for confidence and self-worth: the companionship of the Holy Ghost.

Mafundisho na Maagano 63:58–64

Vitu vitakatifu vinapaswa kutendewa kwa staha.

Kanuni katika Mafundisho na Maagano 63:58–64 ni zaidi ya kulitaja bure jina la Bwana? Ni vitu gani vingine vitakatifu ambavyo huja “kutoka juu,” au kutoka kwa Mungu? Inamaanisha nini kwako kuvitamka vitu hivi “kwa tahadhari”?

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana. .

Nyenzo za Mafundisho na Maagano
ikoni ya 03 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 60:4; 61:1–2; 36; 62:1

Maandiko yanafundisha juu ya Yesu Kristo.

  • Pengine ungeweza kuandika baadhi ya kauli kuhusu Mwokozi zinazopatikana katika Mafundisho na Maagano 60–62 kwenye vipande vidogo vya karatasi. Watoto wako kisha wangeweza kuoanisha kauli hizi na picha za Yesu kutoka kwenye huduma Yake duniani (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 34–61) ambazo zinaonesha sifa hizi. Ni kwa jinsi gani anafanya Yeye Mwenyewe kujulikana kwetu leo hii?

    Jesus Christ at age twelve in the temple at Jerusalem during the Feast of the Passover. A group of learned Jewish doctors are gathered around Christ. The doctors are expressing astonishment at the wisdom and understanding of the young Christ. (Luke 2:41-50)
Yesu Kristo aliyefufuka

Utondoti kutoka Kwa Kusudi Hili, na Yongsung Kim

Mafundisho na Maagano 60:7; 61:1–2; 62:1

Bwana atanisamehe kama nitatubu.

  • Unaposoma Mafundisho na Maagano 60:7; 61:2 pamoja na watoto wako, wasaidie wapate maneno ambayo yanafanana katika mistari hii. Wakumbushe kwamba ufunuo huu ulitolewa kwa Joseph Smith na viongozi wengine wa Kanisa. Ni kipi Bwana aliwataka wajue? Ungeweza pia kuzungumza kuhusu jinsi Mwokozi anavyohisi kuhusu sisi wakati tunapofanya makosa na kile inachomaanisha kutubu. Kulingana na Mafundisho na Maagano 62:1, ni kwa jinsi gani Yesu anaweza kusaidia wakati tunapojaribiwa?

Mafundisho na Maagano 62:3, 9

Yesu Kristo ananitaka nishiriki injili Yake.

  • Ungeweza kuwauliza watoto wako kile ambacho wangesema kama mtu fulani angewauliza ni kipi wanakipenda kuhusu Yesu Kristo na Kanisa Lake. Kuimba pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168) kungeweza kuwapa mawazo. Ungeweza kisha kusoma Mafundisho na Maagano 62:3 na waombe watoto wako wasikilize kile ambacho hutokea wakati tunaposhiriki shuhuda zetu. Ni kwa jinsi gani ahadi katika mstari wa 9 husaidia tunapohisi wasiwasi?

Mafundisho na Maagano 63:64

Ninaweza kuwa na staha.

  • Ili kutambulisha Mafundisho na Maagano 63:64, ungeweza kuimba wimbo kuhusu staha pamoja watoto wako, kama vile “Reverence Is Love” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, na. 31). Kisha ungeweza kuzungumza kuhusu njia tofauti za kuonesha staha kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

  • Unaweza kuwasaidia watoto wako waelewe staha ni nini kwa kuzungumza nao kuhusu kitu ambacho ni muhimu kwao, kama vile mwanasesere wanayempenda au kitabu, au blanketi. Waulize ni kwa jinsi gani wanavitunza na kuvilinda vitu ambavyo ni maalumu kwao. Kisha mngeweza kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 63:64. Ni vitu gani maalumu—au vitakatifu—kwa Baba wa Mbinguni? (ona kwa mfano, mstari wa 61 na ukurasa wa shughuli) ya wiki hii. Ni kwa jinsi gani tunapaswa kuvitendea vitu hivi—kwa maneno na matendo yetu?

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

kuponywa kwa Elsa Johnson

Uponyaji wa Bega la Elsa Johnson, na Sam Lawlor

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto