Njoo, Unifuate
April 15–21. Pasaka: ‘Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?’


“April 15–21. Pasaka: ‘Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“April 15–21. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Kaburi la Bustani.

April 15–21

Pasaka

“Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?”

Unaposoma shuhuda za ufufuko wa Mwokozi katika muhtasari huu, andika hisia na misukumo inayokujia kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Andika Misukumo Yako

Wakati wa wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi, Wayahudi wengi waliomzunguka walikuwa wakishiriki katika utamaduni wa Pasaka. Waliandaa vyakula, kuimba nyimbo, na kukusanyika pamoja kukumbuka ukombozi wa nyumba ya Israeli kutoka utumwani kwa Wamisri. Familia zilisikiliza hadithi ya malaika muangamizaji akipita juu ya nyumba za mababu zao ambao waliweka alama milango yao kwa damu ya kondoo. Katikati ya sherehe hizi zilizojaa ishara nyingi za ukombozi, wachache tu walikuwa wakielewa kwamba Yesu Kristo, Mwanakondoo wa Mungu, alikuwa karibu kuwakomboa kutoka utumwa wa dhambi na kifo—kupitia mateso Yake, kifo Chake, na Ufufuko Wake. Hata hivyo, kuna wale waliomtambua Yesu kama Masiya wao aliyeahidiwa, Mkombozi wao wa milele. Toka siku ile na kuendelea, wafuasi wa Yesu Kristo wametoa ushahidi kwa ulimwengu wote “kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu … ; na kwamba alizikwa, na kwamba alifufuka tena siku ya tatu”(1 Wakorintho 15:3–4).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 21–28

Yesu Kristo ana nguvu ya kunisaidia kushinda dhambi, kifo, majaribu, na udhaifu.

Njia moja ya kuzingatia kwenye baraka za Upatanisho wa Mwokozi wiki hii ni kutumia muda kila siku kusoma kuhusu wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi (ratiba ya kusoma inayowezekana inafuata). Ni nini unapata katika sura hizi kinachokusaidia wewe kuhisi upendo wa Mwokozi? Ni nini unajifunza kuhusu nguvu Zake za kukukomboa kutoka katika dhambi na kifo? Ni nini unajifunza kuhusu kuvumilia majaribu na kushinda udhaifu? Ni kwa jinsi gani unaonyesha imani katika nguvu Zake za ukombozi?

Karamu ya Mwisho

Karamu ya Mwisho, na Carl Heinrich Bloch

Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:19–29; 1 Wakorintho 15:1–8, 55

Mashahidi wengi hushuhudia juu ya Ufufuko wa Yesu Kristo.

Fikiria jinsi ambavyo ilikuwa kwa wanafunzi kumwangalia Yesu akifanyiwa mzaha, akiteswa, na kusulubiwa. Walikuwa wamekuwa mashahidi wa nguvu Zake, kuhisi ukweli wa mafundisho Yake, na walikuwa na imani kwamba Alikuwa Mwana wa Mungu. Kushuhudia kifo Chake kunaweza kuwa jaribu la imani kwa baadhi, lakini baada ya mda mfupi walikuwa mashahidi wa muujiza mkuu wa Ufufuko Wake.

Ni nini unaweza kujifunza kutoka kwenye maelezo ya wale walioshuhudia Ufufuko wa Mwokozi? Wekea alama au andika uzoefu wa kila mtu katika Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:19–29; na 1 Wakorintho 15:1–8, 55. (Kumbuka kwamba mashahidi wengine wa Kristo aliyefufuka wanaweza kupatikana katika 3 Nefi 11; Mormon 1:15; Etheri 12:38–39; Mafundisho na Maagano 76:19–24; 110:1–10; na Historia ya—Joseph Smith 1:15–17.) Katika matukio haya, ni nini huimarisha imani yako katika Ufufuko halisi wa Bwana? Baada ya Ufufuko wa Mwokozi, wengine walifufuka na kuwatokea wengi (ona Mathayo 27:52–53; 3 Nefi 23:9). Kwa nini unahisi ni muhimu kwamba hili liliwekwa kumbukumbu kote katika Biblia na Kitabu cha Mormoni?

Ona pia “Yesu Amefufuka,” “Mwokozi Aliyefufuka anawatokea Mitume,” “Heri yao ambao Hawakuona, na Bado wameamini” (video, LDS.org).

1 Petro 1:3–11

Yesu Kristo hunipa tumaini na shangwe.

Binti wa Mzee Paul V. Johnson Alisa, aliyesumbuliwa na saratani mbaya na kuvumilia upasuaji mwingi, alitoa mfano wa “tumaini hai” Petro aliloelezea katika 1 Peter 1:3–11. Mzee Johnson alishiriki barua Alisa aliyoandika wakati wa Pasaka, muda mfupi kabla ya kufariki: “Pasaka ni ukumbusho wa yote ninayotumaini kwa ajili yangu. Kwamba siku moja nitaponywa na siku moja nitakuwa mzima. Siku moja sitakuwa na chuma chochote au plastiki ndani yangu. Siku moja moyo wangu utakuwa huru kwa hofu na akili yangu huru kwa wasiwasi. … Nina furaha ninaamini kikweli katika maisha mazuri baada ya kifo” (“Hakutakuwepo kifo tena,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 121).

Ni maneno au vishazi gani katika 1 Petro 1:3–11 vinakupa tumaini kwa sababu ya Yesu Kristo? Ni lini umehisi tumaini hilo? Ni kwa jinsi gani unaweza kushiriki tumaini ulilonalo kupitia Yesu Kristo na wale uwapendao?

Ona pia Alma 27:28; 36:1–24; 3 Nefi 9:11–17; Moroni 7:40–41.

ikoni ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Mormon.org

Sehemu “Wiki Takatifu” ya mormon.org/easter inajumuisha ratiba ya wakati ya kila kilichotendeka kila siku ya wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi. Kila siku ya wiki familia yako inaweza kupitia maelezo haya kuona nini Mwokozi alifanya siku hiyo, au unaweza kusoma kuhusu wiki Yake ya mwisho katika maandiko kama familia (ona orodha iliyopendekezwa kwenye “Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi”).

Nyimbo na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Fikiria kuimba nyimbo pamoja kuhusu Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuko wiki hii, ikijumuisha baadhi ambazo hazijulikani sana kwenu (ona kielezo cha mada cha Nyimbo za Kanisa au Kitabu cha nyimbo za Watoto, chini ya mada kama vile “Upatanisho,” “Pasaka,” au “Ufufuko”). Kuwasaidia wanafamilia kujifunza nyimbo, unaweza kuonyesha picha ambazo zinaendana na maneno.

“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Manabii”

Kama familia someni “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Manabii” (Ensign au Liahona, Apr. 2000, 2–3; ona pia LDS.org), na mualike kila mwana familia kuchagua ujumbe wa Pasaka kutoka kwenye ushuhuda huu kushiriki na wengine. Kwa mfano, unaweza kutengeneza mabango ya kuweka kwenye mtandao wa kijamii, juu ya mlango wako wa mbele, au dirishani kwako.

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Weka malengo yanayowezekana. Kutumia hata dakika chache katika siku kujifunza maandiko kunaweza kubariki maisha yako. Jiwekee sharti la kujifunza kila siku, tafuta njia ya kujikumbusha mwenyewe ahadi yako, na fanya kwa uwezo wako wote kuifuata.

Kristo katika Gethsemane

Gethsemane, na Adam Abram