Njoo, Unifuate
Aprili 15–21. Pasaka: ‘Ku Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?’


“Aprili 15–21. Pasaka: ‘Ku Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?’“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Aprili 15–21. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Kaburi la Bustani.

Aprili 15–21

Pasaka

“Ku Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?”

Tumia muda wako na watoto kuwasaidia kuona pasaka kama kipindi cha kufurahia katika Mwokozi na kuongeza shukrani zao kwa dhabihu Yake. Mawazo katika muhtasari huu yanaweza kutoholewa kukusaidia kufundisha watoto wa rika lolote.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachofahamu kuhusu Mwokozi na Upatanisho Wake, unaweza kuonyesha picha za Mwokozi katika Gethsemane, katika msalaba, na baada ya Ufufuo Wake (ona picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56, 57, 58, 59, na 60).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.

Unaposoma kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo, tafakari ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuhisi ni kiasi gani Yesu Anawapenda.

Shughuli za Yakini

  • Wafundishe watoto kwamba kwa sababu sote tunatenda dhambi, hatuwezi kurudi kwa Mungu pasipo Mwokozi ambaye Aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu Kristo anaweza kutuokoa kutoka katika dhambi zetu kama tutatubu. Inua kioo juu, na uwaache watoto waje kwa zamu kukiangalia. Kila mtoto anapotazama, sema, “Yesu anakupenda [jina la mtoto], na Anaweza kukuokoa [jina la mtoto].”

  • Onyesha picha Yesu Akisali katika Gethsemane (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 56) unaposimulia hadithi ya Yesu akiteseka katika Gethsemane kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (ona Mathayo 26:36–46; Luka 22:39–44). Eleza kwamba kwa sababu ya mateso Yake, tunaweza kusamehewa tukifanya uchaguzi usio sahihi. Unaweza pia kutumia “Sura ya 51: Yesu Akiteseka katika Bustani ya Gethsemane,” Hadithi za Agano Jipya, 129–32, au video zinazoambatana katikaLDS.org).

  • Imbeni pamoja “Ninahisi Upendo wa Mwokozi Wangu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75. Maneno gani katika wimbo yanaelezea upendo wa Mwokozi? Uliza watoto jinsi wanavyoweza kuwasaidia wengine kuhisi upendo wa Mwokozi.

Kwa sababu Yesu alifufuka, mimi ninaweza kuishi tena.

Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi na wapendwa wetu tutafufuka siku moja?

Shughuli za Yakini

  • Wafundishe watoto hadithi ya Pasaka kwa kutumia picha ya Kristo katika Gethsemane, katika msalaba, na baada ya Ufufuo, inayopatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili (na. 56, 57, 58, 59, na 60), picha ya kurasa nzima katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Waache watoto wachache washikilie picha wakati unasimulia hadithi. Waeleze watoto kuhusu wachache kati ya watu waliomuona Yesu baada ya kufufuka, kama vile Mariamu (ona Yohana 20:1–18) au Tomaso (ona Yohana 20:24–29).

  • Angalia kama watoto wanafahamu kwa nini tunasherehekea Pasaka. Eleza kwamba katika Pasaka tunasherehekea siku muhimu sana katika historia—siku Yesu Kristo alifufuka. Uliza kama watoto wangependa kushiriki kile familia zao hufanya kukumbuka Ufufuo wa Yesu Kristo.

  • Eleza kwamba ufufuko ina maana kuishi tena baada wa kufa kwetu. Toa ushuhuda wako kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, tutafufuliwa—tutaishi tena baada ya kufa, na hatutakufa tena.

  • Tumia glavu kufundisha watoto kwamba sote tuna mwili (ukiwakilishwa na glavu) na roho (ikiwakilishwa na mkono). Tunapokufa, Roho zetu zinaendelea kuishi, lakini miili yetu haiishi. Tunapofufuliwa, roho na miili yetu huungana tena. Acha watoto wachukue zamu kuvaa na kuvua glavu.

  • Imbeni pamoja wimbo wa pasaka, kama vile “Je! Kweli Yesu Aliishi tena?” au “Yesu Amefufuka,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64, 70 na waonyeshe watoto picha za Yesu baada ya kufufuka (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 59, 60, 61).

  • Onyesha picha ya mtu fulani unayemjua aliyefariki. Shiriki ushuhuda wako kwamba yeye atafufuka kwa sababu ya Upatanisho na Ufufuko wa Yesu Kristo.

  • Tazameni pamoja video za “Yesu Amefufuka” au Bwana Aliyefufuka Akiwatokea Mitume” (LDS.org). Jumbe za Pasaka za ziada zinaweza kupatikana katika mormon.org/easter.

Picha
Yesu na Mariamu katika Kaburi tupu

Amefufuka, na Greg Olsen

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yangu huko Gethsemane na kwenye msalaba.

Unapojifunza Upatanisho wa Mwokozi, tafakari jinsi unaweza kuwasaidia watoto kujifunza na kukumbuka kwamba Kristo aliteseka katika Gethsemane na katika msalaba kwa ajili ya dhambi zao, magonjwa, na huzuni.

Shughuli za Yakini

  • Soma pamoja na watoto Luka 22:39–44 na mistari iliyochaguliwa kutoka Mathayo 27:29–50. Waalike kutafuta maneno ambayo yanawasaidia kuelewa kile Mwokozi alipitia katika Gethsemane na juu ya msalaba.

  • Wasaidie watoto kukariri makala ya imani ya tatu. Toa ushuhuda wako kwamba Yesu Kristo ana uwezo wa kutuokoa kutoka katika dhambi na kifo.

  • Wasaidie watoto kuandaa mazungumzo mafupi kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo ili waweze kushiriki na wengine. Wahimize kujumuisha maandiko na ushuhuda wao katika mazungumzo yao. Kama wanataka msaada wa ziada, wanaweza kusoma “Upatanisho wa Yesu Kristo” katika Kweli katika Imani (14–21).

Kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, mimi nitaishi tena.

Watoto unaowafundisha siku moja watakumbwa na kifo cha mpendwa wao kama bado hawajakumbwa. Wasaidie kujua kwamba kwa sababu Yesu Kristo alifufuka sisi sote tutafufuliwa.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 57, 58, na 59, na waombe watoto kulinganisha picha na vifungu vifuatavyo: Mathayo 27:29–38,– 59–60; Yohana 20:10–18.

  • Waalike watoto kila mmoja binafsi kusoma “Ufufuo” katika Kamusi ya Biblia na kuandika maswali ya jaribio wanayoweza kuuliza juu ya kile wanachosoma. Wapatie watoto muda wa kuulizana maswali na kutafuta majibu kwa pamoja.

  • Wasaidie watoto kuangalia katika kielezo cha mada za Kitabu cha Nyimbo za Watoto kupata wimbo ambao wangeweza kupenda kujifunza kuhusu Yesu Kristo au Ufufuo. Imbeni wimbo kwa pamoja mara chache. Waulize watoto ni nini wanajifunza kutokana na wimbo huu.

  • Kabla ya darasa, waalike watoto wachache kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki shuhuda zao kuhusu Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuko. Waalike watoto kuandika chini shuhuda zao na kushiriki nyumbani.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwasaidia watoto kushiriki kile walichojifunza na familia zao, wahimize kuimba nyumbani wimbo kuhusu Yesu Kristo wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wananufaika kutokana na marudio. Usiogope kurudia shughuli mara nyingi, hususani na watoto wadogo. Marudio yatawasaidia watoto kukumbuka kile unachofundisha.

Picha
ukurasa wa shughuli: Nitaishi tena

Chapisha