Njoo, Unifuate
Aprili 1–14 Mathayo 16-17: Marko 9: Luka 9: “Wewe ndiwe Kristo”


“Aprili 1–14. Mathayo 16–17: Marko 9: Luka 9: “Wewe ndiwe Kristo” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Aprili 1–14. Mathayo 16–17: Marko 9: Luka 9.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Kugeuka Sura kwa Kristo

Kugeuka Sura, ,na Carl Heinrich Bloch

Aprili 1–14

Mathayo 16–17; Marko 9; Luka 9

“Wewe ndiwe Kristo”

Unapotafakari sura hizi katika Agano Jipya na kusikiliza kwenye jumbe wakati wa mkutano mkuu, chukulia maanani jumbe unazohisi watoto katika darasa lako wanahitaji.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kama watoto katika darasa lako walisikiliza au kutazama mkutano mkuu, waalike kushiriki kitu walichosikia au kuona.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 16:13–17

Ninaweza kupata ushuhuda kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Fikiria jinsi unavyoweza kutumia ushuhuda wa Petro na mwitikio wa Yesu kufundisha watoto juu ya ushuhuda ni nini na kuwahimiza kutafuta ushuhuda wao wenyewe.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wasikilize kile Petro alisema unaposoma Mathayo 16:15–17. (Ona pia “Sura 32: Petro Akishuhudia juu ya Kristo.” Hadithi za Agano Jipya, 76–77, au video zinazoambatana katika LDS.org.) Elezea kwamba Petro alikuwa akitoa ushuhuda wake wa Yesu Kristo. Soma mistari tena. (Au onyesha video tena.) Wakati huu waombe watoto kusikiliza ni nani alimwambia Petro kwamba Yesu Alikuwa Mwana wa Mungu.

  • Toa ushuhuda wako wa Yesu Kristo, na ueleze jinsi ulivyoupokea. Waalike watoto kutafuta ushuhuda wao wenyewe kutoka kwa Baba wa Mbinguni.

Mathayo 16:15–19

Yesu Kristo aliwapa manabii na mitume funguo za ukuhani kuliongoza Kanisa Lake.

Mwokozi anafananisha ufunuo na mwamba, mamlaka ya ukuhani na funguo. Je, unawezaje kutumia mfanano huu kuwasaidia watoto kuwa na imani kwa wale wanaoongoza Kanisa Lake?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha watoto mwamba unaposoma Mathayo 16:18 pamoja nao. Rudia pamoja nao kirai “juu ya mwamba huu Nitalijenga Kanisa Langu,” ukiongezea vitendo kuandamana na maneno. Eleza kwamba Kanisa limejengwa juu ya “mwamba” wa ufunuo.

  • Onyesha watoto baadhi ya funguo na waulize tunatumia funguo kufanya nini. Elezea kwamba Petro na Mitume wengine walipokea funguo za ukuhani kutoka kwa Yesu. Funguo hizi “hufungua” baraka kwetu na hufungua njia ya mbinguni. Kwa mfano, funguo za ukuhani huturuhusu kubatizwa na kupokea sakramenti. Wapatie watoto funguo za karatasi, wafanye waandike baadhi ya baraka ambazo funguo za ukuhani “zimefungua”

  • Onyesha picha ya Rais wa Kanisa, na toa ushuhuda wako kwamba anashikilia funguo zote leo, kama tu Petro alivyokuwa nazo.

Picha
sanamu ya Petro akishikilia funguo

Yesu alitoa funguo za ukuhani kwa Petro.

Mathayo 17:19–20

Imani yangu inaweza kutenda miujiza.

Tunaposoma ahadi ya Yesu kwamba imani ni kama punje ya mbegu ya haradali inaweza kuhamisha mlima, ni misukumo gani unayopokea kuhusu watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuchukua zamu kuchora milima mikubwa na mbegu ndogo katika ubao unaposoma Mathayo 17:19–20 pamoja nao. Elezea kwamba milima tunayopaswa kuhamisha ni vitu ambavyo huonekana vigumu kwetu kufanya. Ni vitu gani ambavyo vinaweza kuonekana kama milima kwetu? Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kufikiria kuhusu jinsi imani inaweza kuwasaidia kufanya vitu ambavyo Mungu anawataka wafanye.

  • Weka picha ya mlima katika upande mmoja wa chumba, na andika maneno kama hofu, shaka, au wasiwasi. Waombe watoto kutaja baadhi ya vitu wanavyoweza kufanya kupata imani zaidi katika Yesu Kristo. Acha kila mtoto anayetaja kitu fulani ahamishe mlima karibu na upande mwingine wa chumba. Soma Mathayo 5:19–20, na ushuhudie juu ya uwezo wa imani katika maisha yako.

  • Waombe watoto waimbe “Imani.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 96–97, na halafu mpatie kila mtoto mbegu kuenda nayo nyumbani. Waalike wapande mbegu na kuiweka sehemu fulani ambapo wanaweza kuiona ikikua ili kuwasaidia kukumbuka kuwa na imani katika Baba na Mbinguni na Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 16:13–17

Ushuhuda wa Yesu Kristo huja kupitia ufunuo kutoka mbinguni.

Ni kwa jinsi gani ushuhuda wa Petro katika Mathayo 16:13–17 unawasaidia watoto wanapojenga shuhuda zao?

Shughuli za Yakini

  • Waulize watoto nini wangesema kama mtu fulani angewauliza, “Yesu ni nani?” Alika watoto wasome Mathayo 16:13–17 ili kupata ni jinsi gani Petro alijibu swali hilo. Aliupataje ushuhuda wake wa Yesu? Tunaweza kufanya nini ili kuimarisha shuhuda zetu?

  • Wasaidie watoto kulinganisha jinsi tunajua kweli za kiroho na jinsi tunajua kweli zingine. Kwa mfano, tunajuaje mtu ni mrefu kiasi gani au hali ya hewa ikoje? Tunajuaje kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu?

  • Shiriki ushuhuda wako wa Yesu Kristo, na waalike watoto kushiriki ushuhuda wao.

Mathayo 16:15–19

Kanisa la Yesu Kristo linaongozwa na wale wanaoshikilia funguo za ukuhani.

Kujifunza Mathayo 16 :15–19 kunaweza kujenga imani ya watoto kwamba Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni urejesho wa Kanisa lile lile ambalo Yesu alianzisha wakati Alipoishi duniani.

Shughuli za Yakini

  • Andika Mathayo 16:19 kwenye ubao, ukiacha maneno machache, likiwemo neno “funguo.” Waombe watoto kutafuta maneno yanayokosekana.

  • Onyesha video “Funguo za Ukuhani: Urejesho wa Funguo za Ukuhani”(LDS.org) au pitia habari juu ya funguo za ukuhani katika Kweli kwa Imani, 126–27. Funguo za ukuhani ni nini? Ni kwa jinsi gani funguo za ukuhani ni kama funguo halisi?

  • Wasaidie watoto kuorodhesha kwenye ubao watu wenye funguo za ukuhani. (Kweli kwa Imani, 126–27, ina orodha ambayo inaweza kuwasaidia.) Alika mtu kwenye kata yako ambaye anashikilia funguo hizi kuzungumza na darasa kuhusu kwa nini funguo za ukuhani ni muhimu.

  • Ficha funguo kadhaa (au picha za funguo) kote chumbani, na alika watoto kuzitafuta. Baada ya kila funguo kupatikana, wasaidie watoto kufikiria juu ya baraka tunazofurahia kwa sababu ya funguo za ukuhani (kwa mfano, familia za milele, ubatizo, na sakramenti).

Luka 9:28–36

Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Kugeuka Sura kwa Kristo ni moja kati ya nyakati chache katika maandiko wakati sauti ya Mungu Baba ilisikika akishuhudia juu ya Mwana Wake Mpendwa. Kujifunza tukio hili pamoja na watoto kunaweza kujenga imani yao katika Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuchora picha za Kugeuka Sura kwa Kristo, kama inavyoonekana katika Mathayo 17:1–9. Waombe kuelezeana picha zao wao kwa wao. (Ona pia muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia.)

  • Wape watoto muda kutafakari kile hadithi hii inawafundisha kuhusu Yesu Kristo. Waalike kuandika mawazo yao ubaoni. Alika wachache kushiriki jinsi wanavyojua kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Alika watoto kuuliza wazazi wao au wana familia wengine jinsi gani walipata shuhuda zao juu ya Yesu Kristo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki. Nyimbo za msingi na nyimbo za kawaida zinaweza kuwasaidia watoto wa rika zote kuelewa na kukumbuka kweli za injili. Kuimba kunaweza pia kuwafanya watoto washiriki kikamilifu katika uzoefu wa kujifunza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22.)

Picha
ukurasa wa shughuli: imani yetu inaweza kutenda miujiza

Chapisha