Njoo, Unifuate
Machi 25–31. Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6: ‘Msiogope’


“Machi 25–31. Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6: ‘Usiogope’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 25–31. Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Kristo analisha umati

Wapeni chakula, na Jorge Cocco

Machi 25–31.

Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6

“Usiogope”

Unapojiandaa kufundisha kutoka Mathayo 14–15; Marko 6–7; na Yohana 5–6, angalia jumbe ambazo zinafaa kwenye maisha ya watoto unaowafundisha. Nini unafikiri kinaweza kuwasaidia kuelewa jumbe hizi? Muhtasari huu unaweza kukupatia baadhi ya mawazo.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha ya Yesu akitembea juu ya maji (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia), na waombe watoto kushiriki kile wanafahamu kuhusu hadithi hii.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Yohana 5:1–9

Yesu Kristo anajua kile tunahitaji na anaweza kutusaidia.

Unaposoma kuhusu Yesu akimponya mtu kwenye bwawa la Bethzatha, tafakari ni jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuona kile hadithi inafundisha kuhusu wema wa Yesu, upendo, na sifa nyingine.

Shughuli za Yakini

  • Tumia picha Kristo Akiponya Wagonjwa Bethzatha (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 42) kuwasimulia watoto hadithi katika Yohana 5:1–9. Au onyesha video “Yesu Anamponya Mtu Siku ya Sabato” (LDS.org). Waambie watoto waweke dhana kwamba wao ni mtu ambaye Yesu alimponya. Ni kwa jinsi gani wangejisikia kama Yesu angewaponya?

  • Waombe watoto wataje baadhi ya mambo ambayo ni magumu kwao au yale huwahuzuni. Waambie kuhusu wakati katika maisha yako ulipopokea msaada kutoka kwa Kristo kipindi cha jaribio gumu. Shuhudia kwamba Yesu anajua kuhusu matatizo yetu yote na anataka kutusaidia.

Mathayo 14:13–21

Tunafuata mfano wa Yesu wakati tunapokuwa wakarimu kwa wengine.

Njia moja Yesu alionyesha upendo ilikuwa ni kuwalisha wafuasi Wake walipokuwa na njaa. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kuhudumia wengine kama Yesu alivyofanya?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha watoto kikapu na mkate unapowasimulia hadithi katika Mathayo 14:13–21. Elezea kwamba hata ingawa Yesu alikuwa amejaribu kupata mahali pa kuwa peke yake, watu walitaka kuwa karibu Nae. Shiriki hadithi yote na watoto, na uwaombe wasikilize kile Yesu alifanya kuonyesha wema na upendo kwao.

  • Waombe watoto kushiriki njia ambazo mtu fulani amekuwa mkarimu kwao. Unaweza kufanya nini wiki hii kuwa mkarimu kwa wengine? Kwa kila jibu wanalotoa, chora mkate au samaki katika ubao. Waambie watoto kwamba wanapofanya vitu hivi, wanafuata mfano wa Yesu aliotoa wakati alilisha watu elfu tano waliokuwa na njaa.

Mathayo 14:22–33

Imani katika Yesu Kristo inaweza kutusaidia kutoogopa.

Petro alionyesha imani wakati alitembea juu ya maji kumwelekea Yesu. Masomo gani yanayoweza kuwa kwa ajili ya watoto katika hadithi hii?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha Yesu Anatembea juu ya Maji (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 43) unaposimulia hadithi kwa maneno yako mwenyewe. Fikiria kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kukusimulia wewe hadithi hiyo. Unaweza pia kuleta bakuli dogo la maji na waalike watoto kujifanya ku “tembea” kwa vidole vyao kwenye wa uso wa maji.

  • Onyesha video “Mbona uliona shaka?” (LDS.org), na waombe watoto kuangalia kilichomfanya Petro kuogopa. Kisha waombe wasimulie kuhusu nyakati ambazo wamehisi uoga na kushiriki kile kilichowasaidia. Wasaidie kuona kwamba imani katika Yesu Kristo inatusaidia kushinda hofu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Yohana 5:17–47

Yesu Kristo anatufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni.

Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Yesu kuhusu Baba Yake yanawasaidia watoto kujifunza kuhusu Baba wa Mbinguni?

Shughuli za Yakini

  • Unda seti mbili za kadi zinazofanana zilizoandikwa kwa maneno ambayo Yesu aliyatumia kufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni katika Yohana 5, kama vile upendo, maisha, na kazi (ona Yohana 5:20, 26, 36). Weka kadi kuangalia chini, na waombe watoto kutafuta zile zilizofanana kwa kugeuza kadi mbili kwa wakati. Pindi kila mfanano unapokwisha kutengenezwa, soma mstari wenye neno, na uliza watoto kile neno hilo linatufundisha kuhusu Baba wa Mbinguni.

  • Waombe watoto wasome Yohana 5:30, na kisha kukamilisha sentensi hii: “Sitafuti mapenzi yangu, lakini …” Ni kwa jinsi gani Kristo anafanya mapenzi ya Baba Yake wa Mbinguni? Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

Yohana 6:5–14

Matoleo yetu madogo yanaweza kuleta tofauti.

Ilikuwa ni mvulana mdogo ambaye alitoa mkate na samaki ambazo Yesu alitumia kuwalisha elfu tano. Ni kwa jiinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuona jinsi wanaweza kuchangia katika kazi ya Bwana?

Shughuli za Yakini

  • Gawanya biskuti kavu chache au vipande vya mkate kati ya watoto. Wasaidie kufikiria ni umati mkubwa kiasi gani wa watu elfu tano ungelikuwa. Ingelikuwaje kuwalisha watu hao wengi kwa mikate mitano na samaki wawili tu?

  • Alika mtoto kusimulia hadithi ya kulishwa kwa watu elfu tano kwa maneno yake mwenyewe. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama mvulana katika Yohana 6:9? Alika watoto wachore mikate na samaki kwenye karatasi na waziandike vitu kadhaa wanaweza kumpatia Bwana kusaidia kazi Yake.

  • Wape watoto chamsha bongo ndogo kuikamilisha. Ni nini kingetokea kama mojawapo ya vipande vya chamsha bongo havikuwepo? Elezea kwamba sisi sote ni kama vipande vya chamsha bongo—sisi sote tuna kitu muhimu cha kuchangia katika maisha ya wengine. Ni kwa jinsi gani watoto wanachangia kwenye familia zao au darasani?

Mikate na samaki

Yesu kimiujiza aliwalisha watu 5,000 kwa mikate mitano na samaki wawili.

Mathayo 14:22–33

Imani katika Yesu Kristo inaweza kutusaidia kutoogopa.

Imani na hofu inachukua nafasi kubwa katika hadithi ya Yesu na Petro kutembea juu ya bahari. Ni nini watoto wanaweza kujifunza kutoka kwenye hadithi hii?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Waombe watoto watafute mstari katika Mathayo 14 ambao unaelezea picha hii.

  • Waombe watoto watafute ishara za imani na ishara za hofu wanaposoma Mathayo 14:22–33. Unaweza pia kuonyesha video “Mbona Uliona Shaka?” (LDS.org). Inamaanisha nini kuwa na imani katika Yesu Kristo? Ni kwa jinsi gani tunabadilisha hofu kwa imani?

  • Waombe watoto kufikiria walikuwepo na walikuwa na kamera wakati Yesu na Petro walitembea juu ya bahari. Ni wakati gani wangechagua kuchukua picha na kwa nini? Pendekeza kwamba wapekue Mathayo 14:22–33 kwa ajili ya mawazo. Waalike wachore picha ya wakati waliouchagua, washiriki picha zao, na kueleza kwa nini walichagua wakati huo.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kama watoto wamemaliza ukurasa wa shughuli ya wiki hii, waalike kuutumia kufundisha familia zao kile walijifunza leo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Alika kushiriki Waulize watoto kuhusu mawazo yao, hisia, na uzoefu. Utagundua kwamba mara nyingi wana mawazo rahisi lakini ya kina.