Februari 25–Machi 3. Mathayo 6–7: ‘Alikuwa Akiwafundisha kama Mtu Mwenye Amri’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Februari 25–Machi 3. Mathayo 6–7,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Februari 25–Machi 3
Mathayo 6–7
“Alikuwa Akiwafundisha kama Mtu Mwenye Amri”
Anza kwa kusoma Mathayo 6–7 ukiwa unafikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Ni jumbe gani kutoka katika sura hizi wanahitaji kusikia? Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unaweza kusaidia kukupa mawazo ya kufundisha kama inavyohitajika.
Andika Misukumo Zako
Alika Kushiriki
Waombe watoto kushiriki kile walichofanya wiki iliyopita ili kuwa nuru au mfano kwa mtu fulani.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Mimi naweza kuomba kwa Baba yangu wa Mbinguni kama Yesu alivyofanya.
Watoto wanaweza kujifunza kusali kwa kusikiliza sala za wengine. Unawezaje kuwasaidia kujifunza kutoka katika sala ya Yesu Kristo katika mistari hii?
Shughuli za Yakini
-
Rejea mafundisho ya Yesu kuhusu sala yapatikanayo katika Mathayo 6:5–13. Unaweza kutumia “Sura ya 20: Yesu Akifundisha Kuhusu Sala,” Hadithi za Agano Jipya, 51–52, au video zinazoambatana katika (LDS.org).
-
Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kukumbuka sehemu tofauti za sala.
-
Chora mikono ya kila mtoto kwenye kipande cha karatasi. Sema kuhusu kile tunachopaswa kufanya na mikono tunapoomba. Katika kila mchoro, andika kitu tufanyacho kuonyesha staha wakati tunasali (kwa mfano, kuinamisha vichwa vyetu, kufumba macho yetu, na kadhalika).
-
Wasaidie watoto kutengeneza bango au chati ambayo itawasaidia kukumbuka kuomba asubuhi na usiku, na kuwaalika kushiriki na familia zao.
-
Imba wimbo kuhusu sala pamoja na watoto (kama vile “Tunainamisha Vichwa Vyetu.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25), na toa ushuhuda wako wa nguvu ya sala. Unaweza pia kuwaalika watoto kushiriki uzoefu wao wa sala.
Ninapaswa kuwatendea wengine jinsi ninataka kutendewa.
Mafundisho ya Yesu katika Mathayo 7:12—pia yanafahamika kama Sheria ya Dhahabu—hutoa mwongozo rahisi wa jinsi ya kuwatendea wengine. Ni nini kitachowasaidia watoto unaowafundisha waishi kanuni hii?
Shughuli za Yakini
-
Soma Mathayo 7:12, na ufafanue kwa maneno rahisi ambayo watoto wanaweza kuelewa. Wasaidie watoto kufikiria njia tofauti kumalizia sentensi kama ifuatayo: “Ninapenda wakati wengine wanapo kwa ajili yangu.” Kila baada ya sentensi, waalike kurudia pamoja nawe, “Hivyo ninapaswa kwa wengine.”
-
Imba pamoja na watoto “Yesu Alisema Mpende Kila Mmoja,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61, na fanya vitendo rahisi kuongozana na wimbo. Waulize watoto kile wanachojifunza kuhusu jinsi tunapaswa kuwatendea wengine kutoka katika mfano wa Mwokozi.
-
Waalike watoto kuorodhesha mambo mazuri wazazi wao au wanafamilia wengine wanawafanyia. Soma Mathayo 7:12, na waalike watoto kutengeneza orodha ya mambo mazuri wanayoweza kuzifanyia familia zao.
Ninaweza kujenga juu ya msingi imara kwa kumfuata Yesu.
Kwa kutumia mfano wa Mwokozi kuhusu kujenga nyumba juu ya mchanga au kwenye mwamba kunaweza kuwa njia ya kukumbuka kufundisha watoto kuhusu umuhimu wa kutenda juu ya kile tunachojifunza.
Shughuli za Yakini
-
Imba pamoja na watoto “Mwanaume Mwenye Hekima na Mtu Mjinga” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 281, na fanya vitendo rahisi kuongozana na wimbo.
-
Tumia Mathayo 7:24 kufundisha kuhusu tofauti kati ya mtu mwenye hekima na mtu mpumbavu. Waalike watoto kujifanya wanajenga nyumba. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama mtu mwenye hekima?
-
Waache watoto wachore picha za mfano wa mtu mwenye hekima na mtu mpumbavu.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Mahubiri ya Mlimani yana ujumbe kwangu.
Sura hizi zina ujumbe mwingi ambao unaweza kuwafaa watoto unaowafundisha. Zisome ukiwafikiria watoto akilini. Ni nini kinachokuvutia wewe?
Shughuli za Yakini
-
Wakumbushe watoto kwamba wamekuwa wakijifunza kuhusu kile Yesu alichofundisha wakati wa Mahubiri ya Mlimani. Kweli gani wanaweza kukumbuka kujifunza kuhusu wiki ya mwisho?
-
Andika kwenye ubao baadhi ya virai kutoka kwenye Mahubiri ya Mlimani na virai vingine ambavyo haviko katika maandiko. Waalike watoto kutambua ni virai gani vinavyotokea kwenye Mahubiri ya Mlimani na kushiriki wanachojifunza kutoka kwavyo.
-
Chagua mistari kadhaa kutoka Mathayo 6–7 ambayo unahisi itakuwa na maana kwa watoto. Andika marejeo ya maandiko katika kadi, na zifiche kote chumbani. Waache watoto wazitafute, wasome mistari, na kuelezea kwa nini mafundisho haya ni muhimu kwao.
-
Shiriki kifungu unachokipenda kutoka katika Mathayo 6–7, na elezea kwa nini unakipenda. Ikiwa watoto wana kifungu wanachokipenda, waalike kushiriki kwa nini wanakipenda na kile wanachojifunza kutoka hicho kifungu.
-
Imba “Ninajaribu Kuwa Kama Yesu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 78–79, pamoja na watoto na kutua wimbo unapokuja kwenye kirai ambacho kinahusiana na kanuni iliyofundishwa katika Mathayo 6–7 (kama vile “kujifunza kutumikia marafiki zangu”). Wasaidie watoto kufanya miunganiko na mambo wanayojifunza kutoka katika sura hizi.
Baba wa Mbinguni atasikia na kunijibu ninaposali.
Unapojifunza Mathayo 6:5–13; 7:7–11, unahisi nini watoto wanapaswa kuelewa kuhusu sala?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto wasome Mathayo 6:9–13 kwa sauti na kisha kuorodhesha mambo Mwokozi Alisema katika Sala Yake. Je, tunawezaje kufuata mfano Wake tunaposali?
-
Imba wimbo kuhusu sala pamoja na watoto, kama vile “Ulifikiria Kusali?” Nyimbo, na. 140. Kuwasaidia watoto kutafuta maneno ya wimbo ili kupata sababu tunaomba na baraka ambazo zinazotokana na sala.
-
Wasaidie watoto kukariri Mathayo 7:7 kwa kucheza mchezo kama ufuatao: Mtoto mmoja anakariri neno la kwanza au maneno kutoka kwenye aya hiyo na kisha kurusha mpira kwa mtoto mwingine, ambaye kisha anakariri neno au maneno yajayo.
-
Igiza Mathayo 7:9–10 pamoja na watoto kwa kutumia vifaa rahisi. Waombe watoto washiriki kitu gani hii inawafundisha kuhusu sala.
-
Shiriki wakati ulipohisi kwamba sala zako zilijibiwa.
Ninaweza kutafuta hazina za milele badala ya hazina za kidunia.
Ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia watoto unaowafundisha kuthamini zaidi vitu vya milele kuliko vitu vya kidunia?
Shughuli za Yakini
-
Leta sanduku la “hazina” likiwa limejaa vitu au picha ambazo zinawakilisha vitu ambavyo dunia inathamini—kwa mfano, pesa au mwanasesere. Someni Mathayo 6:19–21 pamoja, na halafu waulize watoto kukusaidia kufikiria juu ya hazina za mbinguni ambazo zinaweza kuchukua nafasi ya vitu vya kidunia katika sanduku.
-
Waalike watoto kutaja au kuchora baadhi ya mambo wanayoweza kufanya “kuweka … hazina mbinguni” (Mathayo 6:20).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki na familia zao mafundisho wanayoyapenda kutoka katika Mahubiri ya Mlimani.