Machi 4–10. Mathayo 8–9; Marko 2–5: ‘Imani Yako Imekuponya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
Machi 4–10. Mathayo 8–9; Marko 2–5 4–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Machi 4–10
Mathayo 8–9; Marko 2–5
“Imani Yako Imekuponya”
Anza kwa kusoma Mathayo 8–9 na Marko 2–5 Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa sura hizi, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waombe watoto washiriki hadithi ya Yesu akifanya muujiza (ona orodha ya miujiza katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia). Unaweza pia kuonyesha picha husika (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 40, 41, au LDS.org).
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Yesu ana nguvu ya kutenda miujiza.
Wakati unaposoma kuhusu miujiza ya uponyaji ya Mwokozi, tafakari miujiza gani ya kushiriki. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kazi ya imani katika miujiza Yesu aliyoitenda?
Shughuli za Yakini
-
Shiriki tukio la mtu mwenye kupooza kutoka Marko 2:1–12. Kwa msaada, ona “Sura ya 23: Mtu Ambaye Hakuweza Kutembea,” Hadithi za Agano Jipya, 57–58, au video zinazoambatana (LDS.org). Waambie watoto kwamba mtu mwenye kupooza hakuweza kutembea. Wasaidie kutambua kwamba mtu huyu aliponywa na kusamehewa na Mwokozi.
-
Alika watoto kujifanya wana “amka” kama binti ya Yairo unaposoma kutoka Marko 5:22–23, 35–43. Wasaidie kuelewa kwamba Yesu amewezesha kwetu sisi sote kupata uzima wa milele.
-
Soma Marko 5:34. Wasaidie watoto kukariri kirai “Imani yako imekuponya,” pengine kwa kuwapatia kila mtoto neno alafu uwaache watoto wayaseme maneno kwa utaratibu. Kuna yeyote wanayemfahamu aliyewahi kuponywa wakati alipokuwa anaumwa?
-
Waombe watoto kufunga macho yao na kusikiliza wakati unasoma kutoka Mathayo 9:27–30. Wakati unasoma kuhusu Yesu Akiwaponya wapofu, alika watoto kufungua macho yao. Watoto wangejisikiaje kama Yesu angewaponya?
-
Waalike waelezee kuhusu wakati walipokuwa wagonjwa. Eleza mojawapo ya matukio ya Yesu akiponya wagonjwa, na shuhudia kwamba nguvu ya Yesu inaweza kutuponya na kutubariki tunaposali na kupokea baraka za ukuhani. Elezea kwamba ingawa saa zingine Bwana hatupatii miujiza tunayohitaji, Anatupenda na anatambua mahitaji yetu. Atatupatia faraja tunayohitaji.
Wakati ninapokuwa na woga au hatarini, Yesu anaweza kunisaidia kuhisi amani.
Tukio la Yesu akituliza dhoruba linaweza kuwasaidia watoto kujua kwamba Anaweza kuwapatia amani wakati wanahisi hofu.
Shughuli za Yakini
-
Wasaidie watoto wafikirie kwamba wapo kwenye meli unaposoma Marko 4:35–41. (Ona pia “Sura 21: Yesu Anaamuru Upepo na Mawimbi,” Hadithi za Agano Jipya, 53, au video zinazoambatana katika LDS.org.) Waombe watoto kuelezea jinsi wangejisikia kama wangekuwa pale. Wakati gani watoto walipata hofu? Ni kwa jinsi gani walipata faraja?
-
Waalike watoto kutoa sauti ya dhoruba na kuacha wakati mmoja anaposema “Nyamaza, utulie.” Shuhudia kwamba kama vile Yesu anaweza kuleta amani wakati kuna dhoruba nje, Anaweza kutuletea amani mioyoni mwetu tunapohisi vibaya ndani yetu.
-
Fikiria matendo yenye kuendana na mstari wa tatu wa “Niambie Hadithi za Yesu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 57
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Yesu anaweza kutenda miujiza kwenye maisha yangu kama nina imani kwake.
Yesu alifanya miujiza mingi wakati wa huduma Yake duniani. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuwa na ufahamu kwamba miujiza inatokea leo?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kuchagua moja kati ya miujiza ifuatayo ili kusoma kuihusu na kuchora: Marko 2:1–12; Marko 5:22–23, 35–43; au Marko 5:24–34. Waalike watoto kuelezea michoro yao kwa darasa. Ni nini wanajifunza kuhusu Yesu katika hadithi hizi?
-
Waombe watoto kuigiza jinsi wanavyohisi wakati wanapokuwa wagonjwa, huzunika, hofu, au wasiwasi. Ni kwa jinsi gani Yesu anatusaidia wakati tuna hisia hizi? Shuhudia kwamba Yesu anaweza kuwasaidia watoto kwenye hali hizi zote.
-
Waalike watoto washiriki uzoefu wakati wao au mtu mwengine wanayemfahamu alipokea baraka ya ukuhani. Ni kwa jinsi gani aliponywa au kubarikiwa?
Ninaweza kuonyesha upendo kwa wengine kama Yesu alivyofanya.
Yesu alionyesha upendo mkuu kwa kuponya wenye magonjwa na waliosumbuliwa. Tafakari jinsi unavyoweza kuwafundisha watoto kuonyesha huruma kwa watu wenye mahitaji.
Shughuli za Yakini
-
Chagua moja au zaidi ya miujiza ya Yesu na kuipitia na watoto, kama ile iliyomo kwenye Marko 2:1–12; Marko 5:22–23, 35–43; au Marko 5:24–34. (Ona pia video “Yesu Anasamehe Dhambi na Kumponya Mtu Aliyepatwa na Kupooza,” “Yesu Anamfufua Binti ya Yairo,” na “Yesu Anamponya Mwanamke mwenye Imani” katika LDS.org.) Waalike watoto washiriki wakati ambapo walimsaidia mtu mwenye mahitaji na jinsi gani walijisikia.
-
Onyesha video “Gordon Hinckley: Masomo Niliyojifunza kama Mvulana” au “Koti” (LDS.org). Ni kwa jinsi gani wavulana kwenye video hizi wanafuata mfano wa Yesu? Waalike watoto kushiriki hali zingine wakati mtu anaweza kuwa na mahitaji. Nini tunaweza kufanya kuwasaidia?
-
Wakumbushe watoto kwamba kuwasaidia wengine ni sehemu ya maagano yao ya ubatizo (ona Mosia 18:8–10; Alma 34:28).
Wakati ninapokuwa na woga au hatarini, Yesu anaweza kunisaidia kuhisi amani.
Watoto wanahitajika kujua kwamba Mwokozi anaweza kuwapatia amani wakati wanakabiliwa na dhoruba za maisha—sasa na katika wakati ujao.
Shughuli za Yakini
-
Muombe mmoja wa watoto kutumia Marko 4:35–41 na picha Yesu Anatuliza Dhoruba (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 40) kusimulia hadithi ya Yesu Akituliza Dhoruba. Waombe watoto kuelezea jinsi wangejisikia kama wangekuwa hapo.
-
Waalike watoto washiriki uzoefu wakati walihisi amani baada ya kusali kwa ajili ya msaada. Wakumbushe kwamba amani hii inatoka kwa Mwokozi.
-
Imba Bwana, Tufani Inavuma” Nyimbo, namba. 105, na watoto, ukiwaalika kunon’gona wakati wanaimba “Nyamaza, utulie.”
-
Mpatie kila mtoto karatasi ya wingu la mvua, na waombe kuiandika jaribu ambalo mtu anaweza kupata. Weka mawingu yote ubaoni, yakifunika picha ya Mwokozi. Mwalike mtoto kuondoa moja ya mawingu na shauri njia tungeweza kumsaidia mtu mwenye majaribu kupata amani. Wakati mawingu yote yakishatolewa, shuhudia juu ya nguvu ya Mwokozi kutuliza dhoruba za maisha yetu.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wasaidie watoto kuandika na kuigiza huduma watakazofanya kwa mtu fulani wiki hii.