Njoo, Unifuate
Machi 18–24. Mathayo 13; Luka 8; 13 ‘Mwenye Masikio, na Asikie’


“Machi 18–24. Mathayo 13: Luka 8:13: ‘Mwenye Masikio, na Asikie’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 18–24. Mathayo 13: Luka 8:13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
ngano i tayari kwa mavuno

Machi 18–24

Mathayo 13; Luka 813

“Mwenye Masikio, na Asikie”

Mafumbo ni hadithi rahisi zinazowezesha kushiriki kwa watoto. Muhtasari huu na Njoo, Nifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kutumia mafumbo ya Mwokozi kufundisha watoto kweli muhimu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Lete vifaa kadhaa ambavyo vitawasaidia watoto kukumbuka baadhi ya mafumbo katika Mathayo 13, kama vile mbegu, lulu, au sanduku la hazina. Waalike watoto kushiriki kile wanakumbuka kuhusu mafumbo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 13:1–23

Nahitaji kujiandaa kujifunza mafundisho ya Yesu.

Watoto wadogo wanaweza wasielewe ishara zote kwenye fumbo la mpanzi, lakini wanaweza kujifunza ukweli wa injili rahisi linalofundisha. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kuelewa vizuri jinsi fumbo hili linavyohusiana nao?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha udongo wa aina tofauti (au picha za udongo unapofanya muhtasari Mathayo 13:3–8. Mpe kila mtoto mbegu apande kwenye udongo. Waulize watoto kile wanaweza kufanya kusaidia mbegu zetu kukua. Elezea kwamba kuwa na imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni njia mojawapo tunasaidia ushuhuda wetu “mbegu” kukua.

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kuelewa kile kila aina ya udongo iliyoelezwa katika Mathayo 13 inafundisha kuhusu mioyo yetu. Waulize watoto ni aina gani ya moyo Yesu anawataka wao kuwa nao ili kujifunza mafundisho Yake.

  • Soma Mathayo 13:9, 15, na uwaalike watoto kuonyesha sehemu mbalimbali za mwili wao wakati wakisikia zimetajwa. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia sehemu hizi za mwili kujifunza mafundisho ya Yesu?

Mathayo 13:24–30, 36–43, 47–48

Baba wa Mbinguni ananitaka nifanye chaguo sahihi.

Baadhi ya mafumbo ya Yesu yanafundisha kwamba siku ya mwisho, Mungu atawatenga waovu kutoka kwa wenye haki. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mafumbo kuwashawishi watoto kuchagua kile kilicho sahihi?

Shughuli za Yakini

  • Waache watoto waigize fumbo la ngano na magugu (ona Mathayo 13:24–30). Elezea kwamba ngano inawakilisha watu wanaofanya chaguo sahihi na magugu (majani hatari) yanawakilisha watu ambao hawafanyi hivyo. Siku moja, Baba wa Mbinguni atawakusanya watu wenye haki kuishi Naye.

  • Eleza baadhi ya hadithi rahisi za watoto wakifanya chaguo. Waombe watoto kusema “chaguo la ngano” wakati watoto katika hadithi wakichagua sahihi na “chaguo la magugu” wakati watoto wakifanya chaguo baya.

  • Lete picha za mabua ya ngano, na waache watoto wachore katika picha baadhi ya njia wanaweza kuwa wenye haki.

  • Buni mchezo ambao watoto wanalinganisha utondoti kutoka katika fumbo la mpanzi na tafsiri yake katika Mathayo 13:18–23.

Mathayo 13:44–46

Uumini wangu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni hazina.

Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia picha ya hazina na lulu za thamani ili kuwasaidia watoto kuelewa thamani ya kuwa wa Kanisa la Kristo?

Shughuli za Yakini

  • Ficha picha za kasha la hazina na lulu katika chumba, na waache watoto wazitafute. Tumia picha kukusaidia kufundisha kuhusu mafumbo katika Mathayo 13:44–46. Ni nini watoto wangeweza kutoa ili kupata lulu nzuri au hazina katika shamba? Elezea kwamba wakati fulani tunatoa kitu kizuri kwa ajili ya kitu bora zaidi. Waambie watoto kwa nini injili ni ya thamani kwako.

  • Weka katika sanduku au kasha vitu kadhaa au picha ambazo zinawakilisha “hazina” katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kama vile mahekalu au Kitabu cha Mormoni. Muombe kila mtoto kuchagua kitu au picha na kuzungumza kuhusu kwa nini ni hazina.

  • Imbeni pamoja “Kanisa la Yesu Kristo.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77, na waombe watoto kusikiliza baraka ambazo huja kutokana na kuwa muumini wa Kanisa. Shuhudia juu ya baraka ulizopata kwa sababu ya uumini wako katika Kanisa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 13:1–23

Nahitaji kuandaa moyo wangu kupokea mafundisho ya Yesu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kugundua umuhimu wa kuwa na moyo laini na ulio tayari ili kwamba Yesu awafundishe?

Shughuli za Yakini

  • Teua kila mtoto kusoma kuhusu moja ya aina nne za udongo katika Mathayo 13:4–8. Waalike watafute na kushiriki kile kinachotokea kwa mbegu katika aina ya udongo wanaousoma. Ni kwa jinsi gani mioyo yetu inaweza kuwa kama aina tofauti za udongo? (ona Mathayo 13:19–23).

  • Mpe kila mtoto mbegu mbili, na waalike wapande mbegu zao katika udongo laini na katika rundo la miamba. Ni udongo gani utakuwa na nafasi bora ya kukua? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha mioyo yetu iko kama udongo laini ili kwamba tuweze kupokea mafundisho ya Mwokozi?

  • Waalike watoto wasome Mathayo 13:9–17. Chora jicho, sikio, na moyo katika ubao. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia sehemu hizi za mwili kujifunza mafundisho ya Yesu?

Mathayo 13:24–30, 36–43

Ninaweza kuchagua kilicho sahihi hata kama wale walionizunguka hawachagui hivyo.

Unaposoma aya hizi ukiwafikiria watoto akilini, misukumo gani inakujia?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuchora picha tofauti kutoka kwenye fumbo la ngano na magugu, lipatikanalo katika Mathayo 13:24–30, na shiriki michoro yao pamoja na darasa. Waombe waonyeshe michoro yao kwa kutumia tafsiri ya fumbo linalopatikana katika Mathayo 13:36–43. Eleza kwamba magugu ni majani yenye madhara.

  • Kama inawezekana, onyesha picha ya ngano na magugu. Eleza kwamba ngano na magugu vitakua pamoja hadi mwisho wa dunia. Hii inatufundisha kwamba tunaishi na yote mema na maovu yakituzunguka, na lazima tuwe makini ili kuchagua kilicho sahihi. Waombe watoto washiriki jinsi wanavyoweza kuelezea tofauti kati ya mema na maovu.

Mathayo 13:44–46

Uumini wangu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni hazina.

Je, watoto unaowafundisha wanaona uumini wao katika Kanisa kama na hazina ya thamani? Yamkini fumbo katika Mathayo 13:44–46 linaweza kuwasaidia.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wasome Mathayo 13:44–46 wao binafsi na kushiriki fumbo katika maneno yao wenyewe na mwanadarasa mwingine.

  • Kata duara kadhaa kuwakilisha sarafu, na uziweke katika sanduku la hazina. Waalike watoto kuchukua sarafu na kuchora au kuandika juu yake kitu kimoja wanachopenda katika kuwa muumini wa Kanisa. Waombe watoto kushiriki kile walichokiweka katika sarafu.

  • Mwalike mshiriki wa kata kushiriki na watoto hadithi yake ya kuongoka na kusema ni kitu gani alichotoa dhabihu ili kujiunga na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kufundisha familia zao kuhusu moja kati ya mafumbo waliyosoma katika Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanapenda kushiriki kile wanachojifunza. Ingawa ni wadogo, watoto wanaweza kuwaimarisha wanafamilia wao. Wahimize kushiriki na familia zao vitu walivyojifunza katika Msingi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.

Picha
ukurasa wa shughuli: Ninahitaji kujifunza ili kuwa tayari

Chapisha