Njoo, Unifuate
Machi 18–24. Mathayo 13; Luka 8; 13: ’Mwenye Masikio Asikie’


“Machi 18–24. Mathayo 13; Luka 8; 13: ‘Mwenye Masikio Asikie’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 18–24. Mathayo 13; Luka 8; 13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
ngano tayari kuvunwa

Machi 18–24.

Mathayo 13; Luka 813

“Mwenye Masikio Asikie”

Unaposoma Mathayo 13 na Luka 813, fikiria jinsi gani utajiandaa “kusikia” na kuthamini mafundisho ya Mwokozi katika mifano hii. Nini utafanya kutumia mafundisho haya maishani mwako?

Andika Misukumo Yako

Baadhi ya mafundisho ya kukumbukwa ya Mwokozi yalikuwa katika mfumo wa hadithi rahisi zilizoitwa mafumbo. Hizi zilikuwa zaidi tu ya hadithi fupi za kuvutia kuhusu vitu au matukio ya kawaida. Zilibeba kweli za kina kuhusu ufalme wa Mungu kwa wale waliokuwa wamejiandaa kiroho. Mojawapo ya mafumbo ya kwanza yaliyoandikwa katika Agano Jipya—fumbo la mpanzi (ona Mathayo 13:3–23)—hutualika kujichunguza utayari wetu kupokea neno la Mungu. “Kwa maana yeyote mwenye kitu,” Yesu alitangaza, “atapewa, naye atazidishiwa tele” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 13:10 [katika Mathayo 13:12, tanbihi a]). Hivyo tunapojiandaa kujifunza mafumbo ya Mwokozi—au mafundisho yake yoyote—sehemu nzuri ya kuanzia ni kujichunguza mioyo yetu na kuamua kama tunalipa neno la Mungu “udongo mzuri” ambamo litakua, kuchanua, kustawi na kuzaa matunda ambayo yatatubariki sisi na familia zetu kwa wingi (Mathayo 13:8).

Picha
ikoni yakujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 13

Ni nini “ufalme wa mbinguni” ambao Kristo alimaanisha katika Mathayo 13?

Katika sura hii, “ufalme wa mbinguni” humaanisha Kanisa la kweli la Kristo, ambalo ni ufalme wa mbinguni duniani. Kwa maelezo zaidi, ona Kamusi ya Biblia, “Ufalme wa mbinguni au ufalme wa Mungu.”

Mathayo 13:3–23; Luka 8:4–15

Moyo wangu unapaswa kujiandaa kupokea neno la Mungu.

Kwa nini kwamba baadhi ya mioyo hupokea ukweli wakati mingine huonekana kuukataa? Kusoma fumbo la mpanzi kunaweza kutoa nafasi nzuri kufikiria kuhusu jinsi unavyopokea ukweli kutoka kwa Bwana. Inaweza kusaidia kwanza kulinganisha mistari 3–8 ya Mathayo 13 na maana iliyotolewa katika mistari 18–23. Nini unaweza kufanya kutengeneza “udongo mzuri” ndani yako? Nini kinaweza kuwa baadhi ya “miiba” ambayo hukuzuia kusikia na kufuata kwa dhati neno la Mungu?

Ona pia Luka 13:34; Mosia 2:9; 3:19; Alma 12:10–11; 32:28–43; Dallin H. Oaks, “Mfano wa Mpanzi,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 32–35.

Mathayo 13:24–35, 44–52

Mafumbo ya Yesu hunisaidia kuelewa ukuaji na hatima ya Kanisa Lake.

Nabii Joseph Smith alifundisha kwamba mafumbo katika Mathayo 13 huelezea ukuaji na hatima ya Kanisa katika siku za mwisho (ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 293–303). Unaposoma mafumbo haya, andika kile yanachokufundisha kuhusu Kanisa la Bwana (unaweza kutaka kurejea kwenye kile Nabii Joseph alifundisha kuhusu baadhi ya mafumbo haya):

Baada ya kutafakari mafumbo haya, unahisi kushawishika kufanya nini kushiriki zaidi katika kazi ya Kanisa la Kristo la siku za mwisho? Maswali yapi huja akilini ambayo yanaweza kukusaidia kutumia mafumbo haya? Kwa mfano, “Nini niko radhi kujitolea kwa ajili ya Kanisa?

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Chachu,” “Mifano.”

Picha
lulu

Injili ya Yesu Kristo ni “lulu ya thamni kuu” (Mathayo 13:46).

Mathayo 13:24–30, 36–43

Wema lazima wakue katikati ya waovu mpaka mwisho wa ulimwengu.

Njia moja ya kuchambua fumbo hili ni kuchora picha yake na kuiwekea alama za utambulisho kwa ufafanuzi katika Mathayo 13:36–43 na Mafundisho na Maagano 86:1–7. Kigugu mwitu ni “gugu lenye sumu, ambalo, mpaka lifikie urefu wa sikioni, linafanana kwa muonekano na ngano” (Kamusi ya Biblia, “Magugu mwitu”). Ni kweli zipi katika fumbo hili zinakushawishi kubaki mwaminifu licha ya maovu ulimwenguni?

Luka 8:1–3

Ni kwa njia zipi “wanawake shupavu” walimhudumia Mwokozi?

“Wafuasi wa kike walisafiri na Yesu na wale Kumi na Wawili, wakijifunza kutoka kwa [Yesu] kiroho na kumtumikia kwa muda. … Kwa kuongezea kwenye kupokea huduma ya Yesu—habari njema ya injili Yake na baraka za nguvu Yake ya uponyaji—wanawake hawa walimhudumia, wakitoa vitu vyao na bidii yao” (Mabinti katika Ufalme Wangu [2011], 4). Wanawake waliomfuata Mwokozi pia walitoa shuhuda zenye nguvu juu Yake (ona Linda K. Burton, “Wanawake Shupavu,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 12–15).

Picha
ikoni yakujifunza kwa familia

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unapojifunza mafundisho ya Mwokozi na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo”

Mathayo 13

Wanafamilia wako wanaposoma mafumbo ya Mwokozi, wanaweza kufurahia kufikiria mafumbo yao wenyewe ambayo hufundisha kweli zinazofanana kuhusu ufalme wa mbinguni (Kanisa), kwa kutumia vitu au hali ambazo zinafahamika kwao.

Mathayo 13:3–23; Luka 8:4–15

Ni nini tunaweza kufanya kama familia kutengeneza “udongo mzuri” katika mioyo yetu na nyumba zetu? (Mathayo 13:23). Kama una watoto wadogo katika familia yako, itakuwa inafurahisha kuwaalika wanafamilia kuigiza njia tofauti za kuandaa mioyo yetu kusikia neno la Mungu wakati wanafamilia wengine wakibahatisha kile wanachofanya.

Mathayo 13:13–16

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wanafamilia kuelewa umuhimu wa kupokea kwa hiari neno la Kristo? Kwa mfano, unaweza kufunga masikio ya mwanafamilia wakati ukisoma kwa unyenyekevu Mathayo 13:13–16. Ni nini mwanafamilia huyo ameelewa kutoka katika mistari? Ni kazi gani macho yetu, masikio, na mioyo hufanya katika kupokea neno la Mungu? Ni njia zipi ambazo tunafunga macho yetu, masikio, na mioyo kwa neno la Mungu?

Mathayo 13:44–46

Ni nini watu wawili katika mafumbo haya wanavyo vyenye kufanana? Je, kuna mambo ya ziada tunayopaswa kuwa tunafanya kama mtu binafsi na kama familia kuweka ufalme wa Mungu kwanza katika maisha yetu?

Luka 13:11–17

Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Mwokozi na kuwaokoa watu kutoka utumwani?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kariri maandiko. Chagua kifungu cha maandiko ambacho hasa kina maana kwa familia yako, na waalike wanafamilia kukikariri. Mzee Richard G. Scott alifundisha, “Andiko takatifu lililokaririwa linakuwa rafiki mvumilivu ambaye hadhoofishwi na muda kupita” (“Nguvu ya maandiko,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 6).

Picha
mtu akipanda mbegu

Fumbo la Mpanzi, na George Soper

Chapisha