“Machi 11–17. Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7; 11: ‘Hao Thenashara Yesu Aliwatuma’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)
“Machi 11–17. Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7; 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019
Machi 11–17.
Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7; 11
“Hao Thenashara Yesu Aliwatuma”
Unaposoma Mathayo 10–12; Marko 2; na Luka 7; 11, andika mawazo unayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Fikiria kuitafakari na kuandika kumbukumbu.
Andika Misukumo Yako
Habari ya miujiza ya uponyaji wa Yesu ilikuwa ikisambaa kwa kasi. Makutano walimfuata, wakitumainia nafuu kutokana na magonjwa yao. Lakini wakati Mwokozi alipowatazama makutano, Aliona zaidi ya maradhi yao ya kimwili. Akijawa na huruma, Aliwaona “kondoo wasio na mchungaji” (Mathayo 9:36). “Mavuno ni mengi, Aligundua, lakini watenda kazi ni wachache” (Mahayo 9:37). Hivyo aliwaita Mitume kumi na wawili, “akawapa amri,” na kuwatuma kufundisha na kuhudumia “kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (Mathayo 10:1, 6). Leo hii hitaji la watenda kazi zaidi kuwahudumia watoto wa Baba wa Mbinguni bado ni kubwa. Bado kuna Mitume kumi na wawili, lakini kuna wafuasi wengi wa Yesu Kristo kuliko ilivyowahi kuwa hapo mwanzo—watu ambao wanaweza kutangaza ulimwenguni kote, “Ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 10:7).
Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi
Bwana huwapa watumishi wake nguvu ya kufanya kazi Yake.
Maelekezo ambayo Yesu aliyatoa katika Mathayo 10 yalikuwa kwa Mitume Wake, lakini sisi sote tunahusika katika kazi ya Bwana. Ni nguvu gani Kristo aliwapa Mitume Wake ili kuwasaidia kutimiza misheni yao? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kufikia nguvu Zake katika kazi uliyoitwa kufanya? (ona 2 Wakorintho 6:1–10; M&M 121:34–46).
Unaposoma mamlaka Kristo aliyowapa wanafunzi Wake, unaweza kupokea mawazo kuhusu kazi ambayo Bwana anakutaka ufanye. Chati kama hii ifuatayo inaweza kukusaidia wewe kuyapanga mawazo yako:
Misukumo ninayopata | |
---|---|
Mwokozi aliwapa wanafunzi Wake nguvu. | Misukumo ninayopata Mungu atanipatia nguvu ninazohitaji katika kufanya kazi yangu. |
Misukumo ninayopata |
Ona pia Makala ya Imani 1:6; Kamusi ya Biblia, “Mtume”; “Yesu Anawaita Mitume Kumi na Wawili ili Kuhubiri na Kuwabariki Wengine” (video, LDS.org).
Ninapomtumikia Bwana, Atanifunulia nini cha kusema.
Bwana aliona mapema kabla kwamba wanafunzi Wake wangeteswa na kuulizwa kuhusu imani yao—kitu ambacho ni sawa sawa na kile ambacho wanafunzi leo wanaweza kupitia. Lakini aliwaahidi wanafunzi wale kwamba wangejua kupitia Roho nini cha kusema. Je, umewahi kupatwa na matukio ambapo ahadi hii takatifu ilitimizwa katika maisha yako, pengine wakati ulipotoa ushuhuda wako, ulipotoa baraka, au ulipokuwa na mazungumzo na mtu? Fikiria kusimulia matukio hayo kwa mpendwa wako au yaandike kama kumbukumbu katika shajara ya kujifunza.
Ona pia Luka 12:11–12; Mafundisho na Maagano 84:85.
Je, Yesu alimaanisha nini kwa kusema “Sikuja kuleta amani, bali upanga”?
Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Nina uhakika kwamba wengi wenu mmekataliwa na kutengwa na baba na mama, kina kaka na kina dada mlipokubali injili ya Yesu Kristo na kuingia katika agano Lake. Kwa njia moja au nyingine, upendo wenu mkuu kwa Kristo umehitaji kuacha mahusiano ambayo yalikuwa ya thamani kwenu, na mmedondosha machozi mengi. Bado kwa upendo wenu usiopunguka, mnashikilia kwa uthabiti chini ya msalaba huu, mkijionyesha kutomuonea haya Mwana wa Mungu” (“Kupata Maisha Yako,” Ensign, Machi 2016, 28).
Utayari huu wa kupoteza mahusiano mliyoyaenzi kwa upendo mkubwa kwa ajili ya kumfuata Mwokozi huja na ahadi kwamba “mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona” (Mathayo 10:39).
Yesu Kristo atanipa pumziko ninapomtegemea Yeye na Upatanisho Wake.
Sote tunabeba mizigo—mingine ikiwa matokeo ya dhambi zetu na makosa yetu wenyewe, mingine ikisababishwa na chaguzi za wengine, na mingine ambayo si kosa la mtu yeyote lakini tu ni sehemu ya maisha duniani. Bila kujali sababu za masumbuko yetu, Yesu anatuomba tuje Kwake ili Aweze kutusaidia kubeba mizigo yetu na kupata usaidizi (ona pia Mosia 24). Mzee David A. Bednar alifundisha, “Kufanya na kushika maagano matakatifu hutuunganisha na Bwana Yesu Kristo” (“Walibeba Mizigo Yao kwa Urahisi,” Ensign au Liahona, Mei 2014, 88). Ukiwa na hili akilini, tafakari maswali kama yafuatayo ili kuelewa zaidi maneno ya Mwokozi katika mistari hii: “Je, ni kwa jinsi gani maagano yangu huniunganisha na Mwokozi?” Je, nahitajika kufanya nini ili kuja kwa Kristo?” au “Ni kwa namna gani nira ya Mwokozi ni laini na mzigo Wake ni mwepesi?”
Je, ni maswali gani mengine hukujia akilini unaposoma? Yaandike kama kumbukumbu na tafuta majibu wiki hii katika maandiko na maneno ya manabii. Unaweza kupata majibu kwa baadhi ya maswali yako katika ujumbe wa Mzee David A. Bednar uliorejewa hapo juu.
Ninaposamehewa dhambi zangu, upendo wangu kwa Mwokozi huongezeka.
Je, unajiona wewe katika hadithi kwenye mistari hii ya ziara ya Mwokozi kwa Simoni Farisayo? Je, wewe ni kama Simoni? Je, unaweza kufanya nini katika kufuata mfano wa mwanamke wa kuonyesha unyenyekevu na upendo kwa Yesu Kristo? Je, ni lini umeuona upole na huruma ambayo Mwokozi alimuonyesha mwanamke huyu? Je, unajifunza nini kutoka katika mistari hii kuhusu jinsi msamaha unavyoimarisha upendo wetu kwa Mwokozi?
Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:
Tunapofikiria ujumbe wa hivi karibuni wa mkutano mkuu, je tunafanyaje kama familia katika kupokea na kufuata ushauri wa Mitume wa siku hizi? Je, ni kwa jinsi gani utiifu wetu kwa ushauri wao hutuleta karibu na Yesu Kristo?
Unaweza kuisaidia familia yako kupiga taswira kichwani ya mafundisho ya Mwokozi katika mistari hii kwa kuwafanya wapeane zamu kujaribu kuvuta kitu kizito, kwanza wao peke yao na kisha kwa usaidizi. Je, ni ipi baadhi ya mizigo tunayobeba? Je, inamaanisha nini kujitia nira ya Kristo? Picha inayoambatana na muhtasari huu inaweza kukusaidia kuelezea nira ni nini.
Je, tunawezaje “kutenda mema” katika siku ya Sabato? (Mathayo 12:12). Je, ni kwa njia zipi Mwokozi anaweza kutuponya katika siku ya Sabato?
Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.