Njoo, Unifuate
Machi 11–17. Mathayo 10–12 ; Marko 2: Luka 7;11: ‘Hao Thenashara Yesu Aliwatuma’


Machi 11–17. Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7:11: “Hao Thenashara Yesu Aliwatuma’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 11–17. Mathayo 10-12; Marko 2: Luka 7:11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Yesu Akimtawaza Petro

Machi 11–17

Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 711

“Hao Thenashara Yesu Aliwatuma”

Unaposoma Mathayo 10–12; Marko 2; na Luka 711, utapokea mnong’ono kutoka kwa Roho Mtakatifu ambao utakusaidia kujiandaa. Minong’ono hii, ikiambatana na Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu, vinaweza kusaidia katika maandalizi yako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wahimize watoto kushiriki jinsi wanaitakasa siku ya sabato.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 10:1–10

Yesu Aliwaita Mitume Kumi na Wawili na kuwapatia uwezo wa kufanya kazi Yake.

Je, watoto unaowafundisha wanafahamu kwamba tuna Mitume Kumi na Wawili hivi leo? Unawezaje kutumia mistari hii kuwafundisha kuhusu umuhimu wa Mitume wa kisasa na kile wameitwa kufanya?

Shughuli za Yakini

  • Fanya muhtasari Mathayo 10:1–10 katika maneno rahisi. (Onyesha Kristo Akiwatawaza Mitume, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 38). Eleza kwamba Yesu huita Mitume kumsaidia kujenga Kanisa Lake.

  • Waache watoto wahesabu Mitume katika picha Yesu Akiwatawza Mitume (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 38) na katika picha ya hivi karibuni ya Akidi ya Mitume Kumi na Wawili (ona LDS.org au toleo la mkutano mkuu katika Ensign au Liahona). Elezea kwamba tuna Mitume kumi na wawili hivi leo, kama tu ilivyokuwa katika siku za Yesu.

  • Ficha picha ya Mitume wa kisasa chumbani kote (ili kupata picha, tazama toleo la hivi karibuni la mkutano mkuu la Ensign au Liahona). Waalike watoto kutafuta picha, na waambie kidogo kuhusiana na kila Mtume (ona “Kutana na Manabii na Mitume wa Leo” katika LDS.org).

  • Mwalike mtoto kushika picha ya Urais wa Kwanza na picha ya Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Muombe mtoto kuongoza watoto wengine kuzunguka chumbani hadi katika picha ya Yesu. Shuhudia kwamba manabii na mitume hutuongoza kuelekea kwa Kristo.

  • Shiriki ushuhuda wako juu ya Mitume wa Bwana.

Picha
Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

Mitume Kumi na Wawili wanafanya kazi ya Bwana leo.

Mathayo 11:28–30

Yesu Atanisaidia ninapokuja Kwake.

Watoto wanaweza kuhisi kufarijika wakijua kwamba Yesu Atawasaidia na mizigo yao watakapokuja Kwake.

Shughuli za Yakini

  • Soma Mathayo 11:28–30 na uonyeshe picha ya ng’ombe waliotiwa nira katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Elezea kwamba hao ng’ombe waliotiwa nira wanaweza kuvuta mzigo mkubwa zaidi kuliko kama wakivuta tofauti tofauti. Shuhudia kwamba tunapohisi vibaya, wasiwasi, au woga, tunaweza kumtafuta Yesu na Atatusaidia.

  • Muombe mtoto kunyanyua kitu kizito. Wakati anapohangaika, jitoe kumsaida. Ni kwa jinsi gani Yesu hutusaidia kufanya vitu vigumu? Watoto wamewahi kuhisi msaada Wake?

Mathayo 12:1–13

Ninaweza kuishika siku ya Sabato kitakatifu.

Je, ni njia gani za kujifurahisha ambazo unaweza kuwafundisha watoto kuhusu siku ya Sabato na kwa nini tunaishika kitakatifu?

Shughuli za Yakini

  • Soma Mathayo 12:10–13 kwa sauti. Waalike watoto kusimama na kukaa kila wakati unaposema “Sabato,” na rudia pamoja nao kirai “Ni [sahihi] kufanya vyema katika siku za Sabato” (Mathayo 12:12). Wanafikiri hiyo ina maana gani?

  • Onyesha kalenda kwa watoto na wasisitizie siku ya Sabato. Tunafanya kitu gani katika siku zingine za wiki? Tunaweza kufanya nini katika Sabato kuifanya iwe tofauti na siku zingine? (Ona Isaya 58:13–14).

  • Waombe watoto wachore vitu vizuri wanavyoweza kufanya katika siku ya Sabato (ona ukurasa wa shughuli ya wiki).

  • Waalike watoto wabuni vitendo vya kuwasaidia kukumbuka njia tunayoweza kuwa tayari kwa Sabato wanapoimba wimbo “Jumamosi.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 196.

  • Chora macho, masikio, mdomo, na mikono katika ubao. Waombe watoto kukuambia ni kitu gani kila sehemu ya miili yetu inaweza kufanya kuishika siku ya Sabato kitakatifu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 10:1–10; Marko 3:13–19

Mitume Kumi na Wawili wanaweza kunifundisha kuhusu Yesu.

Ni kwa jinsi gani kujifunza kuhusu Mitume Kumi na Wawili husaidia watoto kuelewa vyema kile Mitume Kumi na Wawili wanafanya leo?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha za Mitume katika kipindi cha Yesu na katika siku yetu (ona Kristo Akiwatawaza Mitume Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 38, na toleo la mkutano wa hivi karibuni katika magazeti ya Kanisa). Waombe watoto wasome Mathayo 10:1–10 na Marko 3:14–15 ili kujua kile Mitume Wanafanya.

  • Waalike watoto wachache kuja wamejiandaa kushiriki hadithi iliyotolewa na mmoja kati ya Mitume wanaoishi. Ni kwa jinsi gani Mitume wanaoishi wanatusaidia kuwa kama Mwokozi zaidi?

  • Andika majina ya Mitume wa siku hizi katika vipande vya karatasi. Waalike watoto kuoanisha kila jina la Mtume na picha yake (LDS.org). Shughuli hii inaweza kurudiwa mara kadhaa.

  • Shiriki na watoto mifano kadhaa ya shuhuda za Mitume wa siku hizi (ona jumbe za hivi karibuni za mkutano mkuu au “Kristo Anayeishi: Shuhuda za Mitume.” Ensign au Liahona, Apri. 2000, 2).

  • Wasaidie watoto kukariri na kuelewa Makala ya Imani 1:6.

Mathayo 11:28–30

Yesu Atanisaidia ninapokuja Kwake.

Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Mwokozi Atawapatia pumziko kutoka katika changamoto zao wanapokuja Kwake?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto washiriki nyakati walipokuwa na woga au wasiwasi kuhusu kitu fulani. Waalike wapekue Mathayo 11:28–30 kwa ajili ya ushauri ambao utawasaidia katika hali kama hizo.

  • Waalike watoto wachore picha za kile wanachokifanya ili kuja kwa Yesu na kujifunza juu Yake. Makala ya nne ya imani inaweza kuwapatia mawazo.

Mathayo 12:1–14

Sabato ni siku ya kufanya mambo mazuri ambayo hunileta karibu na Mungu.

Watoto unaowafundisha wataimarika unaposisitizia malengo na baraka za kuishika siku ya Sabato kitakatifu.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mtoto aigize mtu ambaye mkono wake uliponywa na Mwokozi (ona Mathayo 12:10–13). Mtoto mwingine anaweza kumsahili kuhusiana na uzoefu huo.

  • Someni pamoja Mathayo 12:12. Je, ni mambo gani mazuri tunaweza kufanya katika Sabato? Waache watoto wachore mawazo yao katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii, kata vipande, na badilishaneni katika kuweka kila chamsha bongo ya moja na mwingine pamoja.

  • Ficha picha kadhaa za watu wakifanya vitu vinavyoonyesha upendo kwa Baba wa Mbinguni katika siku ya Sabato. Waombe watoto kutafuta picha hizo na kushiriki jinsi kufanya vitu katika picha huonyesha upendo wetu kwa Mungu.

  • Mpatie kila mtoto begi la kujaza mawazo ya vitu vizuri vya kufanya katika Sabato. Wanaweza kupata baadhi ya mawazo katika “Kuishika Siku ya Sabato” katika Kwa Nguvu ya Vijana, 30–31.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kushiriki na familia zao mawazo ya kuishika siku ya Sabato kitakatifu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba kwa kimya au kwa mvumo au kuonyesha picha ya Yesu.

Picha
ukurasa wa shughuli: Nitaishika siku ya Sabato kitakatifu

Chapisha