Njoo, Unifuate
Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’


“Februari 18–24. Mathayo 5: Luka 6: ‘Heri Ninyi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Februari 18–24. Mathayo 5: Luka 6.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Mahubiri ya Mlimani

Mahubiri ya Mlimani, na Jorge Cocco

Februari 18–24

Mathayo 5; Luka 6

“Heri Ninyi ”

Anza kwa kusoma Mathayo 1 na Luka 6. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa hizi sura, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto wazungumze kuhusu kitu walichokifanya wiki hii ili kushiriki nuru ya Bwana na mtu mwingine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 5:9

Ninaweza kuwa mleta amani.

Watoto unaowafundisha wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa nyumbani wanapowatendea wengine kwa upendo na ukarimu.

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto Mathayo 5:9, na uelezee kwamba waleta amani hufanya sehemu yoyote kuwa mahali penye amani, pasipo kujali ni wapi walipo. Shiriki matukio machache yasiyo halisi, na uwasaidie watoto kutambua kama watu husika ni waleta amani.

  • Waalike wazazi wachache wa watoto kutembelea darasa lako na kushiriki mifano ya nyakati watoto wao walikuwa waleta amani nyumbani.

  • Andika katika vipande vya karatasi hali mbalimbali ngumu ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo (kwa mfano, ndugu wanapigania mwanasesere). Mwalike kila mtoto kuchukua kipande cha karatasi. Unaposoma matukio, waambie washiriki jinsi wanavyoweza kuwa waleta amani katika hali hiyo.

Mathayo 5:14–16

Yesu anataka niwe nuru kwa wengine.

Watoto wadogo wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa wa mema kwa wengine. Unaweza kuwahamasishaje ili waangaze nuru yao?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha watoto vitu kadhaa vinavyotoa mwanga, ikiwa ni pamoja na picha ya watoto. Soma Mathayo 5:14–16, na uwaambie watoto kwamba sote tuna nuru ndani yetu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia nuru yetu kuwaleta wengine kwa Mungu?

  • Angaza tochi katika chumba. Nuru inatusaidiaje sisi? Tunawezaje kuwa nuru kwenye dunia? Ziba tochi. Ni nini hutokea kama hatushiriki nuru yetu au kama tunaificha?

  • Ficha tochi chumbani, na uzime taa. Waache watoto wajaribu kuitafuta. Rejea Mathayo 5:15, na uzungumzie kuhusu kwa nini hatupaswi kuficha nuru yetu.

  • Angaza tochi katika ukuta, na waalike watoto kufuata nuru kwa macho yao. Tumia nuru kuongoza macho yao hadi kwenye picha ya Mwokozi. Waombe watoto kushiriki jinsi tunavyoweza kuwa nuru iongozayo wengine kwa Yesu Kristo.

  • Wasaidie watoto kutafuta na kupaka rangi mishumaa iliyofichwa katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

  • Imba pamoja na watoto Yesu Ananitaka Mimi kwa Mwale wa Jua.” “Endelea kung’aa,” au ‘Mimi ni kama Nyota,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 60–61, 144, 163.

Mathayo 5:44–45

Yesu Kristo anataka nimpende kila mmoja.

Watoto wadogo wanaweza kuanza sasa kufanya mazoezi ya kuonyesha upendo, hata wakati wanapoteswa na wenzao au ndugu zao. Unaposoma Mathayo 5:44–45, fikiria jinsi mafundisho ya Mwokozi yanawahusu watoto unaowafundisha.

Shughuli za Yakini

  • Rudia tena Mathayo 5:44 kwa kutumia maneno na hali ambazo watoto wataelewa na kuhusika nazo. Waombe watoto kushiriki nyakati walipoonyesha upendo kwa mtu mmoja hata kama ilikuwa ni vigumu. Ni jinsi gani uzoefu huu uliwafanya wajihisi?

  • Kama darasa, imbeni “Nitatembea Nawe,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41. Ni nini tunajifunza kutoka kwenye nyimbo hizi kuhusu kuwapenda wengine?

  • Wape watoto karatasi za mioyo zilizoandikwa kwa maneno “Nitaonyesha upendo wangu kwa kila mtu.” Waombe wapambe mioyo na kuining’iniza nyumbani mwao kama ukumbusho wa kuwapenda wengine.

  • Wasaidie watoto kujifunza matendo kuendana na “Pendaneni.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37, kama ilivyoshauriwa katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 5:3–12

Ninaweza kuwa na furaha ninapoishi kama Yesu Alivyofundisha.

Unaposoma Mathayo 5:3–12, ni maneno na virai gani vinakuvutia? Ni kwa jinsi gani mafundisho haya yatabadilisha maisha ya watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Unda chati kwenye bodi yenye nguzo mbili, zilizoandikwa Heri wale … na Baraka. Waalike watoto kutafuta Mathayo 5:3–12 ni nani Yesu anasema amebarikiwa na baraka Alizowaahidi.

  • Andika kila sifa na baraka zake zinazoambatana kutoka kwenye mistari hii katika kadi, na waache watoto walinganishe sifa na baraka. Waombe watoto kuchagua sifa moja katika mistari hii ambayo wanahitaji kuiendeleza.

Mathayo 5:9, 21–24, 38–47

Ninaweza kuwa mleta amani.

Yesu Alifundisha kwamba waleta amani wataitwa watoto wa Mungu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwahamasisha watoto kuwa waleta amani?

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mtoto asome Mathayo 5:9. Halafu uliza: Mleta amani ni nani? Ni njia zipi tunazoweza kuwa waleta amani kwa familia zetu na marafiki? (Kwa baadhi ya mawazo, ona mistari 21–24, 38–47.)

  • Muombe kila mtoto kufikiria hali ambayo itahitaji msaada wa mleta amani. Mleta amani angefanya nini katika hiyo hali?

  • Waalike watoto kushiriki nyakati ambapo walionyesha upendo kwa mtu fulani, hata kama mtu huyo alikuwa tofauti nao au alikuwa mgumu kupendwa.

Mathayo 5:14–16

Mfano wangu unaweza kuangaza njia kwa wengine kumfuata Yesu.

Fikiria kuhusu watoto unaowafundisha unaposoma mistari hii. Ni ujumbe gani Bwana Angeweza kuwa nao kwa watoto katika kifungu hiki?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kukariri Mathayo 5:16. Andika mstari ubaoni. Someni pamoja mara kadhaa, mkifuta maneno machache kila mara. Baada ya watoto kukariri mstari, unaweza pia kuimba “Endelea Kung’aa.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 144.

  • Waombe watoto wachore vitu vinavyotupatia nuru. Soma Mathayo 5:14–16. Waulize kwa nini Yesu anatuhitaji kuwa nuru katika dunia.

  • Waalike watoto kuchora vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa nuru kwa wengine. Unaweza pia onyesha video “Angaza Dunia: 25 Siku za Huduma” (LDS.org). Waalike watoto wawili kuangaliana, na muombe mmoja kujaribu kumfanya mwingine atabasamu pasipo kumgusa. Zungumzia kuhusu uwezo walio nao watoto kuleta furaha kwa wengine.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wape changamoto watoto kumtazama mtu ambaye akiwa mleta amani wiki hii. Mwanzoni mwa darasa la wiki ijayo, waalike kuzungumzia kuhusu nani na kitu kipi walichoona.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kuwa wachangamfu. Unapowafundisha watoto, waruhusu kujenga, kuchora, kupaka rangi, kuandika, na kubuni. Vitu hivi ni zaidi ya shughuli za kufurahisha—ni muhimu katika kujifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

Picha
ukurasa wa shughuli: Yesu anataka niwe nuru

Chapisha