Njoo, Unifuate
Januari 28–Februari 3. Mathayo 3: Marko 1: Luka 3: ‘Itengenezeni Njia ya Bwana’


“Januari 28–Februari 3. Mathayo 3; Marko 1: Luka 3: ‘Itengenezeni Njia ya Bwana’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Januari 28–Februari 3. Mathayo 3 ; Marko 1: Luka 3.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Yohana Mbatizaji akimbatiza Yesu

Dirisha la kioo kilichotiwa rangi za kuona katika Hekalu la Illinois la Nauvoo, na Tom Holdman

Januari 28–Februari 3

Mathayo 3; Marko 1; Luka 3

“Itengenezeni Njia ya Bwana”

Unaposoma kuhusu Yohana Mbatizaji na ubatizo wa Yesu Kristo, andika hisia yoyote ya kiroho unayopokea. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa haya maandiko, na itakusaidia kuhimili mafunzo ambayo wanadarasa wako wanafanya peke yao.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwapa watoto nafasi ya kushiriki kile walichokwisha kusoma, onyesha picha ya Yesu akibatizwa, na waulize wao kukuambia ni kitu gani kinatendeka katika picha na wanahisi vipi kuhusiana na kubatizwa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 3:13–17

Ninaweza kubatizwa kama Yesu alivyobatizwa.

Unawezaje kutumia tukio la ubatizo wa Yesu kuwasaidia watoto kujiandaa kubatizwa?

Shughuli za Yakini

  • Fanya muhtasari hadithi ya ubatizo wa Mwokozi (ona Mathayo 3:13–17; ona pia “Sura 10: Yesu Anabatizwa.” Hadithi za Agano Jipya, 26–29. au video inayoambatana katika LDS.org). Rudia hadithi mara kadhaa na waalike watoto kushiriki utondoti wanaokumbuka. Elezea kwamba Yesu alibatizwa kwa kuzamishwa na mtu aliyekuwa na mamlaka ya ukuhani.

  • Onyesha picha ya Yesu akibatizwa na ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Waache watoto waonyeshe mfanano kati ya hizi picha mbili.

  • Unaweza kurejea ahadi watoto watafanya wanapobatizwa (ona Mosia 18:8–10; M&M 20:37; Kweli kwa Imani, 23. Waulize watoto kipi kati ya vitu hivi ambacho tayari wanafanya.

  • Mwalike mshiriki wa uaskofu kuwaambia watoto kuhusu mahojiano ya ubatizo ambayo watakuwa nayo kabla ya kubatizwa.

  • Imba “Ubatizo,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 100–101, pamoja na watoto. Fikiria kumwuliza mtoto ambaye anajua wimbo vizuri kuongoza watoto wengine wakati wanaimba

Picha
msichana akibatizwa

Ninaweza kufuata mfano wa Yesu kwa kubatizwa.

Mathayo 3:11 16

Roho Mtakatifu hunisaidia mimi.

Mbali na kujiandaa kwa ubatizo, watoto pia wanajiandaa kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Unawezaje kuwasaidia?

Shughuli za Yakini

  • Tumia Mathayo 3:11, 16 kuwafundisha watoto kwamba Roho Mtakatifu alimshukia Yesu wakati alipobatizwa (njiwa alitokea kama ishara kuonyesha kwamba hii imetendeka) Onyesha picha Kipawa cha Roho Mtakatifu (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 105), na elezea kwamba tunapokea kipawa cha Roho Mtakatifu wakati tunapothibitishwa.

  • Lete sanduku lenye vitu kama vile picha ya Yesu, blanketi yenye faraja, na dira. Waalike watoto kuchagua kifungu na kisha kushiriki jinsi kila kimoja kinawakilisha njia Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia—Anashuhudia juu ya Yesu, hutufariji (ona Yohana 15:26), na anatuonyesha njia sahihi (ona 2 Nefi 32:5).

  • Shiriki uzoefu wako mwenyewe wa kupokea msaada kutoka kwa Roho Mtakatifu.

  • Waalike watoto kusikiliza njia ambazo Roho Mtakatifu hutusaidia wanapoimba ”Roho Mtakatifu.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 3

Nimebarikiwa na ibada za Ukuhani wa Haruni.

Yohana Mbatizaji alishikilia Ukuhani wa Haruni, kwa hiyo hii ni nafasi nzuri kufundisha watoto kuhusu Ukuhani wa Haruni na kuwasaidia kutambua baraka na nguvu ambazo huja kwa wote wanaume na wanawake kupitia kwa ukuhani huu.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ya wajibu wa Ukuhani wa Haruni, ukitumia Mafundisho na Maagano 20:46, 58–60; 84:111. Elezea kwamba makuhani kwenye Ukuhani wa Haruni wanaweza “kubatiza, na kusimamia sakramenti.” Makuhani, walimu, na mashemasi wanatakiwa “kufundisha, na kuwaalika wote kuja kwa Kristo” (M&M 20:46, 59). Waulize watoto kuangalia katika Mathayo 3 kwa mifano ya Yohana akitimiza wajibu huu. Sisi sote tunawezaje kuwaalika wengine kuja kwa Kristo, kama Yohana alivyofanya?

  • Onyesha baadhi ya picha za wenye Ukuhani wa Haruni wakifanya ibada za ubatizo na sakramenti (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 103, 108). Jadili jinsi ibada hizi zinavyotuandaa kumpokea Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 13:1, na uelezee kwamba Yohana Mbatizaji alirejesha Ukuhani wa Haruni kwa Joseph Smith. Waulize watoto jinsi walivyoweza kubarikiwa kwa sababu Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa.

Mathayo 3:13–17; Luka 3:2–18

Ninaweza kuyashika maagano yangu ya ubatizo.

Tukio la ubatizo wa Yesu ni nafasi nzuri kuwasaidia watoto kutathmini maagano yao na kuweka sharti tena kuyashika.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wawili wasome Luka 3:7–9, 15–17, mmoja akisoma maneno ya Yohana Mbatizaji na mwengine akisoma maneno yaliyosalia. Kila baada ya mstari, tua na wasaidie watoto kuelewa kile mstari unamaanisha.

  • Rejea maagano ambayo watoto waliyafanya kwenye ubatizo, yanayopatikana katika Mosia 18:8–10 na Mafundisho na Maagano 20:37. (Ona pia Kweli kwa Imani, 23–26.) Waalike watoto kuandika marejeo haya katika ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

  • Tayarisha jozi kadhaa za kadi na maneno yanayoambatana au picha zinazowakilisha maagano yetu ya ubatizo. Ziweke kadi zikiangalia chini. Waalike watoto kuchukua zamu wakizigeuza mbili kwa wakati, kutafuta zile zilizooana. Baada ya muoanisho kufanyika, waalike watoto kushiriki njia walizoshika maagano hayo.

  • Shiriki jinsi kushika maagano yako ya ubatizo kulivyokubariki.

Mathayo 3:11, 16

Roho Mtakatifu anaweza kuniongoza.

Watoto wanajifunza jinsi ya kutambua na kuufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwafundisha kwamba kushika maagano yao ya ubatizo kutawasaidia kuwa wenye kustahili kupokea mwongozo huu?

Shughuli za Yakini

  • Muombe kila mtoto kuchagua moja kati ya maandiko yafuatayo kuyasoma na kuelezea jinsi Roho Mtakatifu anavyozungumza nasi: Mafundisho na Maagano 6:23; 8:2–3.

  • Muombe mtoto asome Mathayo 3:11. Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu ni kama moto? Kwa mfano, moto unafariji, na unatupatia nuru kutuongoza (ona Yohana 15:26; 2 Nefi 32:5).

  • Waalike watoto kufunga macho yao na kushikilia mikono yao. Kisha taratibu sugua viganja vyao kwa nyoya au kamba. Waalike waseme pindi watakapohisi. Ni nini shughuli hii inafundisha kuhusu kutambua hisia za Roho Mtakatifu?

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu walioupata na Roho Mtakatifu. Kwa nini kushika maagano yetu kunatusaidia kuwa na mwongozo wa Roho Mtakatifu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Himiza watoto kuuliza wazazi wao au wanafamilia wengine kuhusu ubatizo wao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta mwongozo wako mwenyewe. Usione mihtasari hii kama maelekezo ambayo ni lazima kuyafuata unapofundisha. Badala yake, itumie kama mawazo ya kuchochea hisia zako mwenyewe unapotafakari mahitaji ya watoto unaofundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 7.)

Picha
ukurasa wa shughuli: Ninaweza kubatizwa jinsi Yesu alivyobatizwa

Chapisha