“Januari 21–27. Yohana 1: Tumemwona Masiya Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Januari 21–27. Yohana 1 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Januari 21–27.
Yohana 1
Tumemwona Masiya
Unaposoma Yohana 1, andika misukumo ya kiroho unayopokea. Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa sura hii. Shughuli zifuatazo zilizopendekezwa zinaweza kukupa mawazo kuhusu jinsi ya kuwasaidia watoto kujifunza kanuni katika Yohana 1. Shughuli kwa ajili ya watoto wakubwa zinaweza kutoholewa, kama zitahitajika, kwa watoto wadogo.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu Yesu, unaweza kuonyesha picha Zake akitimiza baadhi ya wajibu wake ulioelezewa katika Yohana 1. Kisha waulize kuelezea kile kinachotendeka (kama vile kuumba dunia au kufundisha injili).
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Yesu aliishi na Baba wa Mbinguni kabla hajazaliwa.
Yohana alifundisha kuwa Yesu Kristo aliishi kabla ya uzoefu Wake wa duniani. Sisi pia tuliishi na Mungu kabla hatujazaliwa (Ona “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129). Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza ukweli huu?
Shughuli za Yakini
-
Elezea kwamba “Neno” katika Yohana1:1 linamrejea Yesu. Soma mstari kwa sauti, na waombe watoto kusema “Yesu” kila wakati unaposoma “Neno.” Onyesha mchoro wa mstari Maisha Kabla ya Duniani (LDS.org). Elezea kwamba Yesu Kristo aliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani.
-
Wafundishe watoto kwamba sisi pia tuliishi na Mungu kabla ya kuja duniani. Unaweza kuhitaji kutumia “Utambulisho: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni,” Hadithi za Agano Jipya, 1–5; video zinazofuatana (LDS.org); au Mwongozo kwenye Maandiko, “Maisha kabla ya Duniani,” scriptures.lds.org.
-
Mwalike mzazi kumleta mtoto mchanga darasani, na kutumia hii kama nafasi kufundisha kwamba tuliishi mbinguni na Baba wa Mbinguni kama watoto wa kiroho kabla ya kuzaliwa.
Yesu aliviumba vitu vyote.
Watoto wengi kawaida wanafurahia kuwa miongoni mwa uumbaji wa Bwana. Kujua kuhusu wajibu wa Kristo kama Muumbaji kunaweza kuongeza staha yao kwake.
Shughuli za Yakini
-
Soma Yohana 1:3 pamoja na watoto, na kuonyesha picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Wasaidie watoto kukariri maneno “vitu vyote vilitengenezwa na [Yesu Kristo].”
-
Wapeleke watoto nje kwa matembezi. Waache watoto wachukue zamu kuelezea uumbaji wauonao, na uliza darasa kukisia kile ambacho wanaelezea.
-
Waulize watoto kufikiria juu ya njia ambazo wanaweza kutunza uumbaji unaowazunguka (kwa mfano, kuwa wakarimu kwa wanyama).
Ninaweza kuwaalika wengine kuja kwa Yesu Kristo na kujifunza juu Yake.
Yohana 1 ina simulizi ya wafuasi ambao wakiwaalika watu “njooni muone” kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Hata watoto wadogo wanaweza kufuata mfano huu.
Shughuli za Yakini
-
Elezea jinsi Yohana alimfundisha Andrea kuhusu Yesu, na sema jinsi Andrea kwa upande wake alivyomfundisha Petro (ona Yohana 1:35–42). Shiriki jinsi ulivyojifunza kuhusu Kanisa, au mwalike mshiriki mpya kushiriki jinsi yeye alivyojifunza kuhusu kanisa.
-
Shiriki hadithi ya Filipo akimkaribisha Natanieli “Njoo uone” (Yohana1:43–51). Ficha picha ya Yesu kwenye sanduku, na umwalike mtoto mmoja “Njoo uone” hiyo na kisha awaambie watoto wengine kuhusu kile amekiona.
-
Waache watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii, na wahimize kuitumia kumwalike mtu kujifunza kuhusu Yesu.
-
Muombe mtoto kueleza kuhusu kipindi ambacho yeye alishiriki kitu, kama vile mwanasesere au zawadi, na mtu mwingine. Ni kwa jinsi gani tunaweza kushiriki injili? Elezea hadithi ya mtoto ambaye alishiriki injili na rafiki, kama vile Hadithi ya Mzee M. Russell Ballard kuhusu Yoshua(“Kufuatilia.” Ensign au Liahona, Mai 2014, 78–81).
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Yesu aliishi na Baba wa Mbinguni kabla ya Kuzaliwa.
Hata kabla ya kuzaliwa, Yesu Kristo alitekeleza wajibu katika mpango wa Baba wa Mbinguni. Unaposoma Yohana 1:1–5, ni nini kinachokuvutia kuhusu kazi ya Kristo kabla kuja duniani.
Shughuli za Yakini
-
Waulize watoto kama wanajua chochote kuhusu kile Yesu alifanya kabla hajazaliwa. Waalike watafute majibu katika Yohana 1:1–5. Inaweza kusaidia kuangalia katika Tafsiri ya Joseph Smith, Yohana1:1–5 (katika kiambatisho cha Biblia).
-
Shiriki “Utambulisho: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni,” Hadithi za Agano Jipya, 1–5, na watoto au onyesha video zinazoambatana (LDS.org). Waulize watoto kile wanachojifunza kuhusu Yesu Kristo.
-
Waalike baadhi ya watoto kuja darasani wakiwa wamejiandaa kuonyesha au kuelezea kitu walichounda. Onyesha baadhi ya picha za uumbaji wa Bwana, na tumia Yohana 1:3 kuelezea kwamba Yesu aliumba vitu vyote.
Yesu Kristo ni nuru yangu.
Mfano wa nuru unaweza kuwasaidia watoto kumuelewa Mwokozi na injili Yake. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwahamasisha watoto kutafuta nuru ya Mwokozi wakati dunia inaonekana giza?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kusoma Zaburi 27:1; Yohana 1:4–9; Mosia 16:9; na Mafundisho na Maagano 39:1–2, wakiangalia maneno ambayo yanalingana kwenye maandiko haya. Ni kwa njia gani Yesu Kristo ni kama nuru?
-
Onyesha picha ya Mwokozi na baadhi ya vitu ambavyo hutoa nuru kama vile tochi. Ni kwa njia gani Yesu Kristo ni kama vitu hivi? Ni kwa insi gani tunaweza kushiriki mwanga Wake na wengine? Imba kwa pamoja “Bwana Ni Nuru Yangu.” Hymns, namba. 89, au nyimbo nyingine kuhusu nuru ya injili.
-
Waulize watoto kile wanachofanya wanapokuwa gizani na wanapohisi hofu. Shuhudia kwamba kila wakati wanaweza kumgeukia Mwokozi wanapokuwa na woga.
Kama mfuasi wa Yesu Kristo, Ninawaalika wengine kumfuata Yeye.
Fikiria jinsi unavyoweza kutumia mifano katika Yohana 1:35–51 kuwahimiza watoto kuwaalika wengine kujifunza kuhusu Mwokozi.
Shughuli za Yakini
-
Wasaidie watoto kupekua Yohana 1:35–51 kutafuta vitu ambavyo watu walisema kuwaalika wengine kujifunza kuhusu Mwokozi. Waache wafanyie mazoezi kile wanachoweza kusema kumwalika rafiki kujifunza juu Yake.
-
Waombe watoto watumie ukurasa wa shughuli ya wiki hii kutengeneza mwaliko wanaoweza kutumia kumwalika rafiki au mmoja wa familia kujifunza zaidi kuhusu Yesu Kristo.
-
Wape watoto nafasi kuelezea darasa kuhusu kitu ambacho wanapenda. Wasaidie watoto kuona jinsi kushiriki injili kunaweza kuwa kama kushiriki vitu vingine tunavyopenda. Unaweza kuhitaji kuonyesha video “Mambo Mazuri ya Kushiriki” (LDS.org).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Himiza watoto kualika mtu fulani wanayependa ajifunze zaidi kuhusu Yesu Kristo.