“Januari 7–13. Mathayo 1: Luka 1: ‘Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema ’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Januari 7–13. Mathayo 1: Luka 1 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Januari 7–13
Mathayo 1; Luka 1
“Na Iwe Kwangu kama Ulivyosema”
Anza kwa kusoma Mathayo 1 na Luka 1. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa hizi sura, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia. Kama utahitaji msaada wa ziada kuwafundisha watoto wadogo, ona “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” mwanzoni mwa hii nyenzo.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waombe watoto kukaa katika duara, na kisha muulize mtoto mmoja kushiriki kitu alichojifunza kutoka katika maandiko wiki hii au wakati mwingine. Mtoto huyo anaweza kubingirisha mpira au kumuota mtoto mwingine katika duara, ambaye tena atachukua zamu ya kushiriki.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Malaika walitangaza kuzaliwa kwa Yesu.
Mariamu na Yusufu walitembelewa kila mmoja na malaika aliyetangaza kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Uzoefu huu unaweza kuwasaidia watoto kuona umuhimu wa kuzaliwa kwa Kristo.
Shughuli za Yakini
-
Waalike wazazi wa watoto kuja darasani wakiwa wamevaa kama Mariamu na Yusufu. Waombe washiriki uzoefu wao kama ilivyoandikwa katika Mathayo 1:18–25 na Luka 1:26–38.
-
Simulia hadithi ya malaika wakimtokea Mariamu na Yusufu, kama ilivyoandikwa katika mistari hii. (Ona pia “Sura ya 2: Mariamu na Malaika” na “Sura ya 4: Yusufu na Malaika.” Hadithi za Agano Jipya, 8–9, 12. Au video zinazoambatana katika LDS.org.) Unaweza kuonyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Waalike watoto kurudia hadithi kwa kukusimulia wewe.
-
Waalike watoto kuchora picha za hadithi zipatikanazo katika Mathayo 1:18–25 na Luka 1:26–38.
Baba wa Mbinguni hujibu sala zangu.
Zakaria na Elisabeti walikuwa pengine wakiomba kupata mtoto kwa miaka mingi. Hatimaye Baba wa Mbinguni alijibu sala zao kwa kuwapa mwana, Yohana Mbatizaji. Unawezaje kutumia hadithi hii kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni hujibu sala?
Shughuli za Yakini
-
Kwa maneno yako mwenyewe, simulia hadithi kutoka Luka 1:5–20, 57–63. Unaweza kutaka kurudia hadithi hii mara chache. Wapange watoto kucheza nafasi za malaika, Zakaria, na Elisabeti na kuigiza hadithi hiyo. Sisitiza kwamba Baba wa Mbinguni alijibu maombi ya Elisabeti na Zakaria, na shiriki uzoefu ambao Baba wa Mbinguni alijibu sala yako.
-
Tumia “Tunainamisha Vichwa Vyetu.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25, au wimbo mwingine kufundisha watoto jinsi ya kusali. Pia mnaweza kuimba pamoja “Sala ya Mtoto.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13. Kila wakati watoto wanapoimba maneno “sali” au “sala,” waalike wao kuinamisha vichwa vyao na kukunja mikono yao.
-
Omba kila mtoto afanye vitendo vinavyowakilisha kitu ambacho anaweza kukisalia. Waache watoto wengine wakisie vitendo vinawakilisha nini. Wanaweza kupata mawazo kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii.
Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.
Yesu Kristo ni Mwana wa Baba wa Mbinguni na Mariamu. Kitu gani unaweza kufanya kuwasaidia watoto kujifunza zaidi juu Yake?
Shughuli za Yakini
-
Waambie watoto kwamba malaika alimwambia Mariamu kwamba mtoto wake angeitwa Mwana wa Mungu (ona Luka 1:35). Wasaidie watoto kurudia msemo “Yesu ni Mwana wa Mungu.” Wasaidie watoto kuelewa wazazi wa Yesu ni nani kwa kuwaalika kuchora picha za wazazi wao wenyewe. Wanapofanya hivyo, waambie kwamba Yesu alikuwa na wazazi pia—Mariamu na Baba wa Mbinguni. Zaidi ya hayo, Yusufu aliombwa kumlinda na kumtunza Yesu wakati aliishi duniani.
-
Shiriki ushuhuda wako kwamba kwa sababu Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, Angeweza kufa kwa ajili ya dhambi zetu na kurudi uzimani. Onyesha picha za Kusulibiwa na Ufufuo wa Yesu (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 57, 59).
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Kwa Mungu hakuna kitu kisichowezekana.
Kuzaliwa kwa Yesu na Yohana Mbatizaji kuliwezekana tu kupitia nguvu za Mungu. Kujifunza kuhusu miujiza hii kunaweza kuimarisha imani ya watoto kwamba Mungu ana uwezo wa kufanya miujiza katika maisha yao.
Shughuli za Yakini
-
Wewe na watoto mnaporejea Mathayo 1:18–25 na Luka 1:5–37, Waulize watoto maswali kama “Ungesemaje ikiwa ungekuwa Mariamu?” au “Ungehisije ikiwa ungekuwa Zakaria?”
-
Kwa maneno rahisi, waambie hadithi za kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji na Yesu Kristo. Waombe watoto wainue mikono wanaposikia kitu ambacho kinaonekana hakiwezekani bila nguvu za Mungu. Ni hadithi zipi zingine watoto wanaweza kushiriki ambazo Mungu alifanya kitu kilichoonekana kuwa haiwezekani?
-
Wasaidie watoto kukariri Luka 1:37. Kwa kufanya hivyo, unaweza kuandika aya kwenye ubao na kuwaalika watoto kuisoma mara kadhaa. Baada ya kila wakati, futa neno moja.
Mathayo 1:21–25; Luka 1:30–35,46–47
Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.
Yesu Kristo ni Mwana wa Baba wa Mbinguni na Mariamu. Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza ukweli huu?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto wasome Luka 1:30–35, wakitafuta majibu ya maswali haya: “Ni nani mama yake Yesu?” na “Ni nani Baba yake Yesu?” Wasaidie kuelewa kuwa Yesu Kristo ni mtu peke ambaye baba yake wa kimwili alikuwa Baba wa Mbinguni (ona pia 1 Nefi 11:18–21).
-
Unaposoma aya hizi, waalike watoto kutafuta majina au vyeo vya Yesu Kristo. Majina haya yanamaanisha nini, na yanatufundisha nini kuhusu Yesu?
-
Shiriki ushuhuda wako wa Yesu Kristo, na waalike watoto kushiriki zao.
Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.
Mungu hujibu sala lakini si katika njia ambazo tunatarajia kila mara. Unawezaje kutumia tukio la Zakaria na Elisabeti ili kuwafundisha watoto ukweli huu?
Shughuli za Yakini
-
Waulize watoto kile wanachoweza kumwambia mtu aliyeomba baraka lakini bado hajapokea. Waalike kufikiria juu ya swali hili wanaposoma pamoja Luka 1:5–25, 57–80. (Ona pia “Sura 1: Elisabeti na Zakaria” na “Sura 3: Yohana Mbatizaji Anazaliwa.” Hadithi za Agano Jipya, 6–7,10–11. au video zinazoambatana katika LDS.org.) Je, Zakaria na Elisabeti wanaweza kumwambiaje mtu aliyehisi sala yao haikujibiwa?
-
Waalike watoto kadhaa kabla ya wakati kushiriki uzoefu wakati Baba wa Mbinguni alijibu sala zao. Shiriki wakati ulipohisi kwamba sala zako zilijibiwa kwa njia isiyotarajiwa.
-
Waalike watoto wachore picha ya wakati ambapo Baba wa Mbinguni alijibu maombi–hasa yao wenyewe. Waache washiriki michoro yao na darasa.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki na familia zao picha walizochora na kisha waombe wana familia wao kushiriki nyakati Mungu alijibu maombi yao.