“Januari 14–20. Luka 2: Mathayo 2: Tumekuja Kumsujudia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Januari 14–20. Luka 2 : Mathayo 2, “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Januari 14–20
Luka 2; Mathayo 2
Tumekuja Kumsujudia
Anza kwa kusoma Mathayo 2 na Luka 2. Muhtasari wa wiki hii kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa hizi sura, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waombe watoto kukuambia kile wanachokumbuka kuhusu kuzaliwa kwa Kristo. Je! Ni sehemu gani wanazopenda katika hadithi?
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Yesu alizaliwa.
Yesu aliondoka nyumbani kwa Baba wa Mbinguni kuzaliwa duniani ili apate kuwa Mwokozi wetu. Unawezaje kuwasaidia watoto kukumbuka hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo?
Shughuli za Yakini
-
Unaposoma hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo, waalike watoto waigize hadithi wenyewe au kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii. (Ona pia “Sura ya 5: Elisabeti na Zakaria” Hadithi za Agano Jipya, 13–15, au video zinazoambatana katika (LDS.org).
-
Kama una moja, leta seti ya kuigiza Kuzaliwa kwa Kristo na waalike watoto waweke vipande katika sehemu zinazofaa unapowasimulia hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Unaweza kuonyesha picha ya Kuzaliwa kwa Kristo (ona, kwa mfano, muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Onyesha watu tofauti kwenye tukio la kuzaliwa kwa Yesu na waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu kila mtu.
-
Imbeni pamoja nyimbo zipendwazo na watoto kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Unapofanya, angalia fursa za kutoa ushuhuda wa Mwokozi na waalike watoto kushiriki kwa nini wanampenda Yesu.
Ninaweza kutoa zawadi nzuri kwa Yesu.
Mamajusi walimtolea Yesu zawadi za dhahabu, uvumba na manemane. Unawezaje kutumia hadithi hii kufundisha watoto kwamba wanaweza kutoa zawadi kwa Yesu pia—kama upendo, huduma, na utii?
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha ya Mamajusi mnaporejea hadithi yao, inayopatikana katika Mathayo 2:1–12, pamoja na watoto. Unaweza kuonyesha picha Mamajusi Wakitoa Zawadi (LDS.org).
-
Funika picha za zawadi au vitu ambavyo vinawakilisha zawadi tunazoweza kumpa Yesu. Waalike watoto kukusaidia kufungua zawadi na kujadili jinsi tunavyotoa zawadi hizi kwa Mwokozi.
-
Msaidie kila mtoto kuchora au kuandika orodha ya zawadi wanazoweza kutoa kwa Yesu, kama vile “kuwa rafiki mwema” au “kusali.” Waalike watoto kushiriki orodha zao pamoja na darasa na kuchagua moja ya kuitendea wiki hii.
Yesu alikuwa mtoto kama mimi.
Kujifunza kuhusu utoto wa Mwokozi kunaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujihusisha Naye. Waulize watoto kile wanachoweza kujifunza kutokana na mistari hii kuhusu jinsi wanavyoweza kuwa kama Yesu sasa.
Shughuli za Yakini
-
Mwalike mmoja wa vijana katika kata ili kutembelea darasa na kushiriki hadithi ya Yesu Akifundisha katika hekalu wakati Alikuwa kijana.
-
Waulize watoto kadhaa kabla ya muda kuleta picha zao wenyewe wakiwa watoto wachanga za kushiriki. Waulize jinsi walivyokua. Shiriki baadhi ya njia ambazo Yesu alikua (ona Luka 2:40, 52). Imba na watoto “Wakati Fulani Yesu alikuwa Mtoto Mdogo,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 55, au wimbo mwingine kuhusu Mwokozi.
-
Soma Luka 2:52 na eleza kile “hekima” na “ukubwa” inamaanisha. Unaweza kuwauliza watoto kufanya vitendo vinavyoonyesha kile inamaanisha kuongezeka kwa hekima na kwa fadhila na Mungu na watu wengine. Kwa mfano, wanaweza kuigiza kusoma kitabu au kumsaidia mtu aliye na hitaji
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Manabii wa kale walitabiri kuzaliwa kwa Mwokozi.
Manabii na waumini walikuwa wanatarajia kuzaliwa kwa Mwokozi kwa karne nyingi. Kuelewa ukweli huu kunaweza kuwasaidia watoto kupata kuthamini zaidi kwa maisha ya Mwokozi na huduma Yake.
Shughuli za Yakini
-
Waulize watoto kuzungumza juu ya mambo wanayotarajia, kama siku ya kuzaliwa au likizo. Waache watoto wasome Helamani 14:2–5 kupata kitu fulani manabii walikuwa wanatazamia.
-
Someni pamoja baadhi ya unabii wa kuzaliwa kwa Mwokozi (ona Isaya 7:14; 9:6; 1 Nefi 11:18; Helamani 14:5). Wasaidie watoto kuorodhesha maelezo yaliyomo katika unabii huu na utafute utimilifu wake katika Luka 2:1–21 na Mathayo 2:1–2.
-
Waalike watoto kuchora picha ya kuzaliwa kwa Yesu na kushiriki kwa nini wanashukuru kuwa Yesu alizaliwa.
Yesu alikuwa mtoto kama mimi.
Kama Yesu, watoto unaowafundisha wana huduma muhimu ya kujiandaa kwa ajili yake. Wanaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa Yesu?
Shughuli za Yakini
-
Unaposoma Luka 2:40, 52, waambie watoto wasikilize vitu Yesu alifanya. Waalike watoto kushiriki njia ambazo wamekua tangu walipokuwa wadogo. Shiriki uzoefu wako mwenyewe wa kujifunza injili kidogo kidogo; kisha toa ushuhuda wako.
-
Kamilisha shughuli zinazoonyesha virai katika Luka 2:40, 52. Kwa mfano, unaweza kupima urefu wa kila mtoto (“Yesu aliongezeka katika … kimo”) au waache washiriki maandiko yao wayapendayo (“alikua imara kiroho”). Wasaidie watoto kuweka kumbukumbu ya njia wanazokua na kushiriki na familia zao.
-
Baada ya kurejea Luka 2:40, 52, waalike watoto kushiriki kile wanachofikiria Yesu angelikuwa Alipokuwa wa umri wao. Angemtendeaje mama Yake? Kaka na Dada Zake?
Ninaweza kufuata mfano wa Yesu.
Hata alipokuwa kijana mdogo, Yesu Alikuwa Akifundisha wazee katika hekalu. Vivyo hivyo, watoto katika darasa lako wana mengi ya kuwafundisha wale walio karibu nao.
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kuja wakiwa wamejiandaa kufanya muhtasari hadithi katika Luka 2:41–52. Ili kuwasaidia watoto kuelewa hadithi, fundisha “Kazi ya Baba” inamaanisha nini. Kwa mfano, unaweza kuwaelezea watoto kazi gani wewe au wazazi wako mnafanya. Yusufu alikuwa anakazi au “shughuli” gani, Baba ya Yesu duniani? (ona Mathayo 13:55). Kazi ya Baba Yake wa Mbinguni ilikuwa ni ipi? (ona Luka 2:46–49; ona pia Musa 1:39).
-
Pamoja na watoto, someni Luka 2:46–49 na uulize, “Yesu Alifanya ‘Kazi ya Baba Yake’ vipi?” Wasaidie watoto kuorodhesha au kuchora ubaoni njia wanazoweza kusaidia kufanya kazi ya Baba wa Mbinguni pia.
-
Ili kuwasaidia watoto kujenga kujiamini kwamba wao, kama mvulana Yesu, wanaweza kufundisha injili, wasaidie kufanya mazoezi kufundishana wao kwa wao kanuni kutoka Kwa Nguvu ya Vijana.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto kuelezea familia zao kile ambacho wamejifunza kuhusu kuzaliwa kwa Kristo.