“Februari 4–10. Mathayo 4: Luka 4–5: ‘Roho wa Bwana Yu juu Yangu’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Februari 4–10. Mathayo 4: Luka 4–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Februari 4–10
Mathayo 4; Luka 4–5
“Roho wa Bwana Yu juu Yangu”
Anza maandalizi yako ya somo hili kwa kusoma Mathayo 4 na Luka 4–5. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa hizi sura, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waombe watoto wapitishe picha ya Yesu kutoka mtoto mmoja hadi kwa mwingine. Kila mtoto anapopokea picha, mwalike kushiriki kitu fulani ambacho Yesu alifanya Alipokuwa duniani.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Ninaweza kuchagua kilicho sahihi jinsi Yesu alivyofanya.
Watoto wachanga “hawawezi kutenda dhambi” (M&M 29: 47). Hata hivyo, tukio la Yesu akipinga majaribu ya Shetani linaweza kuwahamasisha watoto kuanza sasa kuchagua kilicho sahihi.
Shughuli za Yakini
-
Simulia hadithi ya majaribu ya Yesu, kutoka Mathayo 4:1–11. (Ona pia “Sura 11: Yesu Akijaribiwa” Hadithi za Agano Jipya, 30–31, au video zinazoambatana katika LDS.org.) Katika sehemu inayofaa katika hadithi, uliza, “Unafikiri Yesu Angefanya nini?”
-
Onyesha picha ya Yesu Kristo, na halafu elezea chaguzi mtoto mdogo anaweza kufanya. Kwa kila uchaguzi mwema muombe mtoto atembee hatua kuelekea kwenye picha. Kwa kila uchaguzi mbaya, muombe mtoto atembee hatua kuelekea mbali na picha.
-
Wasaidie watoto kusoma maneno “Chagua Njia Sahihi.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 160–61. Kwa kutumia picha, vitu, au vifaa vya kuonyeshea vinavyolingana na maneno.
Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.
Luka 4: 18–19 orodhesha vipengele vya huduma ya Yesu. Unawezaje kuwasaidia watoto kuthamini alichokifanya kwa ajili yao?
Shughuli za Yakini
-
Wasomee watoto Luka 4:18–19, na ueleze ni kitu gani Yesu Kristo alitumwa kukifanya duniani (kufundisha, kufariji, na kuponya watu). Shiriki jinsi alivyofanya hivi kwako.
-
Waalike watoto wachache wajifanye wamechanganyikiwa, wanasikitika, au wagonjwa. Waombe watoto wengine kuigiza kile ambacho wangefanya kuwasaidia. Shuhudia kwamba Yesu Kristo alikuja kufundisha, kufariji, na kutuponya, na kwamba tunatakiwa kufuata mfano Wake.
-
Onyesha picha ya Yesu Kristo akitimiza vipengele vya huduma yake (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili), na waulize watoto waelezee kile Yesu anachofanya. Pia onyesha picha za watu wakijaribu kuwa kama Yesu (unaweza kuzipata baadhi kwenye magazeti ya kanisa).
-
Andika kwenye vipande vya karatasi maneno ambayo yanaanza na “Kwa sababu ya Yesu Kristo” (kama vile “Kwa sababu ya Yesu Kristo, familia yangu inaweza kuwa pamoja milele”). Alika kila mtoto kuokota kipande kimoja cha karatasi, na umsaidie kusoma kirai.
Yesu Kristo anatualika sisi tuwe “wavuvi wa watu.”
Wito wa Mwokozi, “Nifuate, na nitawafanya wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19), inatumika kwa kila mtu, hata watoto.
Shughuli za Yakini
-
Alika watoto wawili kujifanya kuwa Simoni Petro na Andrea unaposoma Mathayo 4:18–22. Wasaidie watoto kutambua nini wanaume hawa waliachana nacho kumfuata Yesu.
-
Waache watoto wachukue zamu kusimulia hadithi kutoka kwenye mistari hii wakitumia picha kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia.
-
Imbeni pamoja “Nitafuata Mpango wa Mungu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 164. Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwenye wimbo huu kuhusu kumfuata Yesu Kristo?
-
Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kujadili na watoto jinsi wanavyoweza kuwa “wavuvi wa watu” kwa kumfuata Yesu. Unaweza pia kucheza mchezo wa kuoanisha: kata nakala mbili za kila samaki, ziweke zikiangalia chini, na alika watoto kuchukua zamu kuzigeuza moja kwa wakati kutengeneza muoano.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Kristo aliweka mfano kwangu kwa kushinda majaribu.
Hata Yesu Kristo alijaribiwa na Shetani, lakini Hakukubali. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kufuata mfano Wake?
Shughuli za Yakini
-
Tengeneza chati kwenye ubao iliyoandikwa Majaribu ya Shetani na Majibu ya Yesu. Wasaidie watoto kujaza chati wakitumia Mathayo 4:1–11 na Luka 4:1–13. Uliza watoto jinsi wanavyoweza kufuata mfano wa Yesu.
-
Andika baadhi ya matukio ambapo mtoto angeweza kujaribiwa kufanya chaguo baya. Mwache mtoto achague mmoja wa kusoma, na wajadili kama darasa jinsi wangeweza kupinga majaribu katika hali hiyo.
Kufunga kunaweza kunisaidia kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni.
Kabla ya kuanza huduma Yake, Yesu alifunga na “kuwasiliana na Mungu” (Tafsiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:2 [katika Mathayo 4:2, tanbihi c]). Wasaidie watoto kuona jinsi kufunga kunaweza kuwapatia nguvu ya kiroho na kuwasaidia kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni.
Shughuli za Yakini
-
Alika mtoto asome kwa sauti Mathayo 4:1–2 akitumia Tafsiri ya Joseph Smith ya marekebisho yanayopatikana kwenye tanbihi. Ni nini Yesu alifanya ili “kuwa na Mungu”? Shiriki jinsi kufunga kumekusaidia kuhisi kuwa karibu na Baba wa Mbinguni.
-
Alika watoto ambao wamewahi kufunga kushiriki uzoefu wao. Wanawezaje kuelezea kuhusu kufunga kwa mtu ambaye hajawahi kufunga hapo awali?
-
Andika maswali kuhusu kufunga (kama vile kwa nini, wakati gani, au jinsi gani tunafunga) kwenye vipande vya karatasi na uweke kwenye bakuli. Alika watoto waokote swali na kujaribu kulijibu. Ni uzoefu gani wewe au watoto mnaweza kushiriki kuhusu kufunga?
Yesu Kristo ni Mwokozi wangu.
Tafakari jinsi Mwokozi amebariki maisha yako. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuthamini vyema ushawishi Wake katika maisha yao?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kuja darasani wakiwa wamejiandaa kufanya muhtasari Luka 4:16 –30. Inaweza msaada kutumia “Mlango 17: Watu wenye Hasira huko Nazareti,” Hadithi za Agano Jipya, 42–43; video zinazoambatana (LDS.org; au video “Yesu Anatangaza Yeye Ni Masiya” (LDS.org).
-
Soma Luka 4:1 kwa sauti wakati watoto wanafuatilizia. Waombe watengeneze orodha ya vitu ambavyo Mwokozi alisema amekuja kuvifanya. Waalike watoto kushiriki mifano ya nyakati ambapo Kristo alitenda vitu hivi, aidha kwenye maandiko au kwenye maisha yao.
Yesu Kristo anatualika tumfuate na tuwe “wavuvi wa watu.”
Kuna njia nyingi ambazo watoto wanaweza kumfuata Mwokozi na kuwa “wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kuona ushawishi mzuri wanaoweza kuwa nao kwa wengine?
Shughuli za Yakini
-
Alika watoto wasome Mathayo 4:18–22 na Luka 5:1–11. Ni kwa jinsi gani wanafunzi wa Yesu waliitikia wito wa kumfuata Yeye? Ni nini tunaweza kufanya kufuata mfano wao?
-
Onyesha watoto baadhi ya vifaa vya uvuvi au picha ya mvuvi. Inamaanisha nini kuwa “mvuvi wa watu”? Vifaa gani tulivyonavyo kutusaidia kuwa wavuvi wa watu?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kushiriki na familia zao kile wamejifunza kuhusu kuwa wavuvi wa watu.