“Februari 11–17. Yohana 2–4: ‘Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Februari 11–17. Yohana 2–4 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Februari 11–17
Yohana 2–4
“Hamna Budi Kuzaliwa Mara ya Pili”
Maandalizi yako kufundisha yanaanza unaposoma Yohana 2–4. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa hizi sura, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Himiza watoto kushiriki kile wanachosoma na kupitia kwa kuwauliza kitu gani wamefanya hivi karibuni ili kuwa “wavuvi wa watu” (Mathayo 4:19). Unaweza kurejea somo la wiki iliyopita pamoja nao.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Ninahitaji kubatizwa na kuthibitishwa ili kurudi kuishi na Baba wa Mbinguni.
Watoto unaowafundisha wanajiandaa kuchukua hatua muhimu kuishi na Baba wa Mbinguni tena kwa kubatizwa (kuzaliwa kwa maji) na kuthibitishwa (kuzaliwa kwa Roho). Unawezaje kuwasaidia waelewe umuhimu wa ibada hizi mbili?
Shughuli za Yakini
-
Fanya muhtasari wa hadithi ya Yesu akimfundisha Nikodemo. Waahidi watoto kwamba wanapobatizwa, Baba wa Mbinguni Atawapatia kipawa cha Roho Mtakatifu.
-
Tumia Yohana 3:5 na ukurasa wa shughuli ya wiki hii kufundisha kwamba tunahitaji kubatizwa na kuthibitishwa ili kuishi tena na Baba wa Mbinguni.
-
Waulize watoto kuzungumza kuhusu kile wanafanya ili kuosha mikono yao. Onyesha picha Msichana Akibatizwa (Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 104), na wasaidie watoto kulinganisha kuosha mikono yetu kwa maji na kuwa wasafi kiroho kupitia ubatizo.
Baba wa Mbinguni Ananipenda, hivyo alinipa Mwokozi.
Unawezaje kuwasaidia watoto kujifunza ukweli huu wa thamani?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kukamilisha sentensi kama hii: “Kwa sababu wazazi wangu wananipenda, wana. …” Soma Yohana 3:16. Halafu msaidie kila mtoto kurudia Yohana 3:16, kwa kubadilisha neno “dunia” na jina lake mwenyewe, na uwaache watoto wasikilize kile Baba wa Mbinguni Alifanya kwa sababu Anatupenda. Waalike watoto kuchora picha za vitu vinavyowasaidia kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwao (kama vile familia, asili, maandiko, na kadhalika). Waache washiriki michoro yao wao kwa wao.
-
Waache watoto wainue juu picha ya Yesu kila wakati wanapoimba “Mwana” katika “Alimtuma Mwanawe.” Kitabu cha Nyimbo za watoto, 34–35.
Yesu Kristo ni “maji yangu ya uzima.”
Watoto katika darasa lako wanaweza wote kujihusisha na kuwa na kiu. Unawezaje kutumia uzoefu huo kuwasaidia watoto kuelewa jinsi gani tunahitaji maji ya uzima Yesu Kristo anatoa?
Shughuli za Yakini
-
Tumia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia kuwasimulia hadithi ya Yesu na mwanamke kisimani. Waombe watoto wasimulie tena hadithi hiyo.
-
Onyesha glasi ya maji, na waulize watoto kitu gani kingetokea kama tungekuwa na kiu sana na glasi lingekuwa tupu. Kwa ufupi fanya muhtasari Yohana 4:5–15, na kushuhudia kwamba Yesu Kristo na Injili Yake huzipa roho zetu uzima, kama vile maji huipa uzima miili yetu.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Ninaweza kumheshimu mama yangu kama Yesu alivyofanya.
Katika harusi huko Kana, Mariamu alimwambia Yesu kwamba divai imeisha. Kufuatana na tafsiri ya Joseph Smith, Yesu Alimjibu mama Yake kwa kumuuliza, “Mama, ni kitu gani ungetaka mimi nikifanye kwa ajili yako? ambacho nitafanya” (Yohana 2:4. tanbihi a). Yesu ni mfano wa jinsi watoto wanapaswa kuwatendea mama zao.
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto wasome Yohana 2:1–11 na kuchukua zamu mmoja baada ya mwingine kusimulia tena sehemu zake katika maneno yao wenyewe.
-
Waulize watoto kuorodhesha vitu mama yao anaweza kuhitaji msaada. Waalike wafanye kile wanachoweza kumwambia wakitumia baadhi ya maneno ya Yesu: “Ni kitu gani ungetaka Mimi nifanye kwa ajili yako?” (Yohana 2:4. tanbihi a).
-
Waalike baadhi ya akina mama kutembelea darasa lako na kushiriki kile watoto wao hufanya kuonyesha heshima kwao.
Kubatizwa na kuthibitishwa ni kama kuzaliwa kwa mara ya pili.
Tunapobatizwa, ambayo Yesu aliita “kuzaliwa kwa maji,” tunapokea ondoleo la dhambi zetu na “kuingia katika ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuelewa kuzaliwa kwa mara ya pili inamaanisha nini?
Shughuli za Yakini
-
Paranganya maneno ya Mwokozi katika Yohana 3:3 na wafanye watoto wayaweke katika utaratibu sahihi. Ni kwa jinsi gani kubatizwa na kuthibitishwa ni kama kuzaliwa kwa mara ya pili?
-
Onyesha picha ya mtoto mchanga aliyezaliwa na mtu mwingine akibatizwa na kuthibitishwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 104 na 105). Ni kwa jinsi gani sisi tuko kama mtoto mchanga aliyezaliwa baada ya kubatizwa na kuthibitishwa? (Ona Yohana 3:3-5.)
-
Waalike watoto kushiriki kumbukumbu za ubatizo wao. Soma Mosia 18:8–10 na Mafundisho na Maagano 20:37 kurejea upya agano la ubatizo. Wafundishe watoto kwamba kupokea sakramenti kwa umakini kila wiki ni njia ya kuendelea na mchakato wa kuzaliwa tena.
-
Wasaidie watoto kukariri Makala ya Imani 1:4.
Baba wa Mbinguni Ananipenda, hivyo Alimtuma Mwanawe.
Unawezaje kuwasaidia watoto kujua kwamba Yesu Kristo alitumwa duniani kama kielelezo cha upendo wa Baba wa Mbinguni?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kuchora picha ya zawadi waipendayo na mtu aliyewapatia hiyo zawadi. Halafu muuliza mtoto asome Yohana 3:16. Ni zawadi gani Baba wa Mbinguni Ametupatia? Ni kwa jinsi gani zawadi hii inaonyesha upendo Wake?
-
Waombe watoto kusikiliza majibu ya swali, “Kwa nini Baba wa Mbinguni Alitutumia Yesu Kristo?” Wanapoimba au kusikiliza “Alimtuma Mwanawe.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35.
Yesu Kristo ananipa “maji ya uzima.”
Kama Yesu Alivyotumia maji kumfundisha mwanamke wa Samaria, unaweza kutumia maji kuwafundisha watoto kwa nini tunahitaji injili ya Yesu Kristo.
Shughuli za Yakini
-
Wapeni watoto kinywaji cha maji, na waombe washiriki uzoefu wakati wana kiu. Zungumza kuhusu jinsi ulivyohisi hatimaye kupata maji ya kunywa.
-
Andika sentensi fupi kutoka katika hadithi ya mwanamke kisimani, na waombe watoto kupitia Yohana 4:6–23 kuweka sentensi katika utaratibu sahihi. Ni nini Yesu alikuwa anajaribu kumfundisha mwanamke?
-
Chora katika ubao kikombe cha maji na chemchemi au mto. Waalike watoto kutaja vitu ambavyo, kama kikombe cha maji, huturidhisha kwa muda. Ni vitu gani kama “maji ya uzima” ambavyo vinaweza kuturidhisha milele?
-
Andika ubaoni Ni kwa namna gani injili ni kama maji? Uliza watoto kufikiria kuhusu jinsi wanangeweza kujibu hili swali wanaposoma katika Yohana 4:6–23.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Fikiria kuwaomba watoto kuwapatia wanafamilia wenzao kinywaji cha maji watakapofika nyumbani. Wanapofanya, wanaweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu maji ya uzima.