Njoo, Unifuate
Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’


“Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Februari 18–24. Mathayo 5; Luka 6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Mahubiri ya Mlimani

Mahubiri ya Mlimani, na Jorge Cocco

Februari 18–24

Mathayo 5; Luka 6

“Heri Ninyi ”

Kuwa makini kwa misukumo unayopokea unaposoma Mathayo 5 na Luka 6, na uiandike katika shajara ya kujifunzia. Muhtasari huu unaweza kukusaidia kutambua baadhi ya kanuni muhimu zaidi na zinazohusika katika sura hizi.

Andika Misukumo Yako

Katika hatua hii katika huduma Yake, ilikuwa wazi kwamba mafundisho ya Yesu yangekua tofauti na kile ambacho watu wa wakati Wake walikuwa wakisikia. Masikini watapokea ufalme wa Mbinguni? Wapole watairthi nchi? Heri wenye kuteswa? Waandishi na Mafarisayo hawakuwa wakifundisha mambo hayo. Na bado kwa wale ambao waliielewa sheria ya Mungu kikamilifu, mafundisho haya yalionekana sawa. “Jicho kwa jicho” na “mchukie adui yako” zilikuwa sheria ndogo (Mathayo 5:38, 43, zilizotolewa kwa watu ambao hawakuwa tayari kuishi sheria ya juu. Lakini Yesu Kristo alikuwa amekuja kutimiza ile sheria ndogo na kufundisha sheria kuu (ona 3 Nefi 15:2–10) imetengenezwa ili kutusaidia sisi siku moja kuwa “wakamilifu kama Baba [yetu] aliye mbinguni alivyo mkamilifu” (Mathayo 5:48).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 5:1–12; Luka 6:20–26

Furaha ya kudumu huja kwa kuishi jinsi Yesu Kristo alivyofundisha.

Kila mmoja anataka kuwa na furaha, lakini si kila mtu hutafuta furaha katika sehemu zinazofanana. Baadhi huitafuta katika nguvu na vyeo vya ulimwengu, wengine katika utajiri au kwa kutosheleza matamanio ya kimwili. Yesu Kristo alikuja kufundisha njia ya kupata furaha ya kudumu, kufundisha maana halisi ya kubarikiwa. Je, unajifunza nini kuhusu kupata furaha ya kudumu kutoka katika Mathayo 5:1–12 na Luka 6:20–26? Je, ni kwa jinsi gani hii ni tofauti na mtazamo wa ulimwengu kuhusu furaha?

Je, ni maswali au mawazo gani hukujia akilini unaposoma kila mstari? Je, mistari hii inakufundisha nini kuhusu kuwa mfuasi wa Yesu Kristo? Unahisi ushawishi wa kufanya nini ili kuendeleza sifa zilizoelezewa katika mistari hii?

Ona pia Yohana 13:17; 3 Nefi 12:3–12; “Mahubiri ya Mlimani: Mahubiri ya Heri” (video, LDS.org).

Mathayo 5:13

Je, ni kwa nini Mwokozi aliwafananisha wafuasi Wake na chumvi?

Chumvi kwa kipindi kirefu imekuwa ikitumika kuhifadhia, kuongeza ladha, na kusafishia. Chumvi pia ilikuwa na maana ya kidini kwa Waisraeli. Ilikuwa ikihusishwa na utamaduni wa kale wa kutoa wanyama kafara chini ya sheria ya Musa (ona Mambo ya Walawi 2:13; Hesabu 18:19). Chumvi ikiwa imeharibika, inakuwa “haifai tena kabisa” (Mathayo 5:13). Hii hutokea inapokuwa imechanganywa na au kuchafuliwa na elementi zingine. Kama wafuasi wa Kristo, tunatunza “ladha” yetu kwa kuepuka uchafu wa kiroho kutoka ulimwenguni. Hii hutusaidia kutimiza kazi yetu ya kuhifadhi na kusafisha kama chumvi ya dunia—kwa mfano, kupitia kushiriki na wengine injili na kuwa ushawishi kwa mema katika ulimwengu (ona M&M 103:9–10).

Picha
chumvi

“Ninyi ni chumvi ya dunia” (Mathayo 5:13).

Mathayo 5:17–48; Luka 6:27–35

Sheria ya Kristo huchukua nafasi ya sheria ya Musa.

Wafuasi wanaweza kuwa walishangaa kusikia Yesu akisema kwamba haki yao ilihitaji kuzidi ile ya waandishi na Mafarisayo (ona Mathayo 5:20), ambao walijiinua kwa jinsi walivyotii sheria ya Musa vyema. Lakini Yesu alifundisha sheria ya juu ambayo siyo tu iliinua matendo yetu lakini pia mawazo na hisia zinazoyapa msukumo. Sheria hii ya juu ilihitaji mengi zaidi: moyo, nafsi, na akili (ona Mathayo 22:37).

Unaposoma Mathayo 5:21–48 na Luka 6:27–35, fikiria kuwekea alama kote tabia zilizohitajika katika sheria ya Musa (“Mmesikia ya kwamba …”) na kile Yesu alifundisha ili kuziinua.

Kwa mfano, nini Yesu alifundisha katika Mathayo 5:27–28 kuhusu jukumu letu juu ya mawazo yetu? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kupata udhibiti zaidi wa mawazo yanayokujia akilini na moyoni? (ona M&M 121:45).

Ona pia “Mahubiri ya Mlimani: Sheria ya Juu” (video, LDS.org).

Mathayo 5:48

Je, Baba wa Mbinguni anatarajia mimi niwe mkamilifu?

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

“Neno ukamilifu lilitafsiriwa kutoka Kigiriki teleios, ambalo humaanisha ‘timilifu.’ … Kitenzi jina cha tendo ni teleiono, ambacho humaanisha ‘kufika mwisho mrefu, kuwa kikamilifu, kukamilisha, au kumaliza.’ Tafadhali kumbuka kwamba neno halimaanishi ‘uhuru wa kutofanya kosa’; humaanisha ‘kufikia malengo ya mbali.’ …

“… Bwana alifundisha, ‘Ninyi hamuwezi kustahimili uwepo wa Mungu sasa … ; kwa hiyo, endeleeni katika uvumilivu hadi mtakapokuwa mmekamilika’ [M&M 67:13].

“Hatupaswi kufa moyo kama jitihada zetu za dhati kuelekea ukamilifu sasa zinaonekana kuwa ngumu na zisizo na mwisho. Ukamilifu unasubiri. Unaweza kuja kwa ukamilifu tu baada ya Ufufuko na kupitia tu kwa Bwana. unawasubiri wote wampendao, na kutii amri zake” (“Perfection Pending,” Ensign, Nov. 1995, 86, 88).

Ona pia Wafilipi 3:13–15; 2 Petro 1:3–11; Ufunuo 3:21–22; 3 Nefi 27:27; Moroni 10:32–33; Mafundisho na Maagano 76:69.

Picha
ikoni ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani

Familia yako inaposoma maandiko pamoja, Roho anaweza kuwasaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Mathayo 5:1–9

Kanuni zipi zilizofundishwa katika Mathayo 5:1–9 zingeweza kusaidia nyumba yako kuwa mahali pa furaha? Unaweza kuzingatia kwenye kanuni moja au mbili unapojifunza Mahubiri ya Mlimani wiki chache zijazo. Kwa mfano, ni mafundisho gani wanafamilia wako wanapata ambayo yatawasaidia kuwa waleta amani? (ona Mathayo 5:21–25, 38–44). Je, ni malengo gani unaweza kuweka? Je, ni kwa jinsi gani utafuatilia?

Mathayo 5:14–16

Ili kuwasaidia wana familia wako kuelewa inamaanisha nini kuwa “nuru ya ulimwengu,” unaweza kutafiti baadhi ya vyanzo vya nuru nyumbani mwako, mazingira ya jirani na kwako, na ulimwenguni. Inaweza kusaidia kuonyesha kinachotokea unapoficha nuru. Je, Yesu alimaanisha nini aliposema, Ninyi ni nuru ya ulimwengu”? (Mathayo 5:14). Je, ni nani amekuwa kama nuru kwa familia yetu? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kuwa nuru kwa wengine? (ona M&M 103:9–10).

Mathayo 5:43–44

Je, kwa nini Bwana anatutaka tuwaombee wale ambao wamekuwa si wema kwetu? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuishi kanuni hii katika familia yetu?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa Makini. Unapokuwa na usikivu kwa kile kinachotokea maishani mwa watoto wako, utapata fursa nzuri sana za kufundisha. Maoni na maswali ya watoto wako kwa siku nzima yanaweza pia kuelekeza kwenye nyakati zinazowezekana kufundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 16.)

Picha
mshumaa

“Ninyi ni nuru ya ulimwengu” (Mathayo 5:14).

Chapisha