Njoo, Unifuate
Aprili 22–28. Mathayo 18; Luka 10: ‘Nifanye Nini ili Kurithi Uzima wa Milele?’


“Aprili 22–28. Mathayo 18; Luka 10: ‘Nifanye Nini ili Kurithi Uzima wa Milele?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Aprili 22–28. Mathayo 18; Luka 10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Msamaria mwema

Msamaria Mwema, na Dan Burr

Aprili 22–28.

Mathayo 18; Luka 10

“Nifanye Nini ili Kurithi Uzima wa Milele?”

Kwa maombi unaposoma na kutafakari Mathayo 18 na Luka 10, kuwa mwangalifu na ushawishi wa kimya kimya wa Roho Mtakatifu. Atakuambia jinsi gani mafundisho na hadithi hizi zinatumika kwako. Andika misukumo unayopokea.

Andika Misukumo Yako

Unapomuuliza Bwana swali, unaweza kupokea jibu ambalo hukutegemea. Jirani yangu ni nani? Yeyote anayehitaji msaada na upendo wako. Je, ni nani aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Mtoto. Je, inatosha kumsamehe mkosaji mara saba? Hapana, unapaswa kusamehe sabini mara saba (Ona Luka 10:29–37; Mathayo 18:4, 21–22.) Kama unatafuta mapenzi ya Bwana, siyo kujihesabia haki “wewe [mwenyewe]” (Luka 10:29), bali kwa sababu ni kweli unataka kujifunza kutoka Kwake, Bwana atakufundisha jinsi ya kuishi katika njia inayokuongoza kwenye uzima wa milele pamoja na Yeye.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 18:21–35

Ni lazima niwasamehe wengine ili nipokee msamaha wa Bwana.

Pendekezo la Petro kwamba angeweza kumsamehe mtu mara saba lingeweza kuonekana la ukarimu sana, lakini Yesu alifundisha sheria ya juu zaidi. Jibu Lake, “Sikuambii, Hata mara saba: bali, Hata sabini mara saba” halikufundisha kuhusu idadi bali hasa kuhusu mtazamo kama wa Kristo juu ya msamaha. Unaposoma mfano wa mtumwa asiye na huruma, tafakari nyakati ambapo wewe ulisikia rehema na huruma ya Mungu. Je, kuna yeyote anayehitaji kuhisi neema na huruma kutoka kwako?

Mzee David E. Sorensen wa Sabini alifundisha: “ningependa kuweka wazi kwamba msamaha wa dhambi haupaswi kukanganywa na kuvumilia uovu. … Japokuwa tunapaswa kumsamehe jirani anayetukosea, bado tunapaswa kufanya juhudi za kutoa maoni yenye usaidizi wa kuzuia kosa hilo lisirudiwe” (“Msamaha Utabadili Uchungu kuwa Upendo,” Ensign au Liahona, Mei 2003, 12).

Ona pia “Msamaha,” Mada za Injili, topics.lds.org.

Luka 10:1–20

Sabini ni kina nani?

Akifuata mpangilio ulioanzishwa nyakati za Agano la Kale (ona Kutoka 24:1; Hesabu 11:1), Yesu Kristo “alichagua wengine sabini,” kuongezea kwa Mitume Wake Kumi na Wawili, kumshuhudia Yeye, kuhubiri injili Yake, na kumsaidia katika kazi Yake. Mpangilio huu unaendelea katika Kanisa lililorejeshwa. Sabini huitwa kuwasaidia Mitume katika huduma yao kama mashahidi maalumu wa Yesu Kristo kwa ulimwengu wote. Sabini wamepangwa katika akidi. Washiriki wa akidi mbili za kwanza wanasimikwa kama Viongozi Wakuu wenye Mamlaka Sabini, wakati washiriki wa akidi zingine wanasimikwa kama Sabini wa Maeneo. (Ona pia M&M 107:25–26, 33–34, 97.)

Luka 10:25–37

Kupata uzima wa milele, ninapaswa kumpenda Mungu na kumpenda jirani yangu kama ninavyojipenda mimi mwenyewe.

Inasaidia kukumbuka kwamba fumbo la Msamaria mwema lilikuwa ni njia ya Yesu kujibu swali: “Jirani yangu ni nani?” Unaposoma fumbo hili, lishike swali hilo akilini. Je, unapata majibu gani?

Katika siku ya Yesu, chuki kati ya Wayahudi na Wasamaria ilikuwa imekithiri kwa karne nyingi. Wasamaria walikuwa ni wazao wa Wayahudi walioishi katika Samaria ambao walikuwa wameoana na Wayunani. Wayahudi waliona kwamba Wasamaria walikuwa wameharibika kwa muingiliano wao na Wayunani na walikuwa wamekengeuka. Wayahudi wangesafiri maili nyingi nje ya njia yao kuepuka kupita katika Samaria. (Ona pia Luka 9:52–54; 17:11–18; Yohana 4:9; 8:48.)

Je, ni kwa nini unafikiri Mwokozi alimchagua Msamaria, mtu ambaye alichukiwa na Wayahudi, kama mfano wa huruma na kumpenda jirani yako? Je, ni kitu gani fumbo hili linakushawishi kufanya ili kuonyesha rehema zaidi kwa wengine?

Ona pia Mosia 2:17; “Fumbo la Msamaria Mwema” (video, LDS.org); “Bwana, Nitakufuata,” Nyimbo za Dini, namba. 220.

Luka 10:38–42

Tunachagua “fungu lililo jema” kwa kufanya chaguzi ambazo zinapelekea kwenye uzima wa milele.

Dada Bonnie D. Parkin, Rais mkuu wa zamani wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, alifundisha: “Mariamu na Martha ni mimi na wewe. … Wawili hawa walimpenda Bwana na walitaka kuonyesha upendo huo. Katika tukio hili, inaonekana kwangu kwamba Mariamu alionyesha upendo wake kwa kusikiliza neno Lake, wakati Martha alionyesha wake kwa kumtumikia Yeye. … Yesu hakupuuza kujishughulisha kwa Martha, lakini badala yake alielekeza upya kuzingatia kwake kwa kusema chagua ‘fungu lililo jema.’ Na hicho ni nini? … Kitu kimoja ambacho kinahitajika ni kuchagua uzima wa milele [ona 2 Nefi 2:28]. Tunachagua kila siku” (“Chagua Hisani: Fungu lile Jema,” Ensign au Liahona, Nov. 2003, 104). Ni kwa jinsi gani unaweza kufanyia muhtasari ushauri wa Bwana kwa Martha kwa maneno yako mwenyewe? Chunguza ratiba yako—kuna jambo “linalohitajika” ambalo huitaji zaidi usikivu wako?

Picha
ikoni ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Mathayo 18; Luka 10

Je, ni nyimbo zipi za dini familia yako inaweza kuimba ambazo zinahusiana na ukweli ulioofundishwa katika sura hizi? Mifano miwili ni “Bwana, Nitakufuata” “Nimefanya Jema Leo?” Nyimbo za Dini, namba. 220, 223, lakini kuna nyingine nyingi. Je, ni kwa jinsi gani maneno katika nyimbo hizi za dini husaidia familia yako kuelewa vizuri mafundisho ya Mwokozi?

Mathayo 18:1–11

Je, ni kwa nini Yesu alitaka sisi tuwe kama mtoto mdogo? Je, ni zipi baadhi ya sifa za watoto ambazo zinatufanya kuwa zaidi kama Kristo endapo tukizitumia katika maisha yetu? (Ona Mosia 3:19).

Picha
Yesu pamoja na watoto mapajani mwake.

Yesu huwataka wafuasi Wake kuwa kama watoto wadogo.

Luka 10:25–37

Je, ni nini kingefanya mfano wa Msamaria mwema kuwa hai kwa familia yako? Je, wao wangependa kufurahia kuvaa mavazi na kuigiza? Hakikisha unawasaidia wanafamilia kuona jinsi wanavyoweza kuwa kama Msamaria Mwema. Je, kuna mtu mwenye shida shuleni au kanisani ambaye tunaweza kuwa hatumwoni? Je, tunaweza kufanya nini kwa ajili ya mtu huyu?

Luka 10:40–42

Je, ni vigumu kuingiza mambo ya kiroho katika ratiba ya familia yako? Hadithi ya Mariamu na Martha inaweza kushawishi baraza la familia au jioni ya familia nyumbani kuhusu jinsi ya kufanya hili. Kama familia, mnaweza kutengeneza orodha ya njia za kuchagua “fungu lililo jema” (ona Luka 10:42).

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuza mazingira ya upendo. Jinsi wanafamilia wanavyojisikia kuhusu na kutendeana kunaweza kushawishi kwa kina roho ya nyumbani kwako. Wasaidie wanafamilia wote kufanya sehemu yao ili kustawisha nyumba yenye upendo, heshima ili kwamba kila mmoja ajisikie yu salama kuelezea uzoefu, maswali, na shuhuda zao. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 15.)

Picha
Kristo akiwa na Mariamu na Martha

Kristo Nyumbani kwa Mariamu na Martha, na Walter Rane

Chapisha