Njoo, Unifuate
Aprili 29–Mei 5. Yohana 7–10: ‘Mimi Ndimi Mchungaji Mwema’


Aprilii 29–Mei 5. Yohana7–10: ‘Mimi Ndimi Mchungaji Mwema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

Aprilii 29–Mei 5. Yohana 7–10,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Kristo na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi

Yeye Asiye na Dhambi, na Liz Lemon Swindle

Aprili 29–Mei 5.

Yohana 7–10

“Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”

Unaposoma Yohana 7–10, unaweza kupokea mawazo kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu kanuni za mafundisho ya injili zilizoko katika ya sura hizi. Kuandika misukumo yako kunaweza kukusaidia kuweka mpango wa kuifanyia kazi.

Andika Misukumo Yako

Japokuwa Yesu Kristo alikuja kuleta “amani [na] kwa watu wote” (Luke 2:14), kulikuwa na “matengano katika mkutano kwa ajili yake” (John 7:43). Watu walioshuhudia matukio yanayofanana walifikia mahitimisho tofauti kuhusu Yesu alikuwa nani. Baadhi walihitimisha, “Ni mtu mwema,” na wengine wakasema, “Anawadanganya makutano” (Yohana 7:12). Alipomponya kipofu siku ya Sabato, baadhi walisisitiza, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki siku ya sabato,” wakati wengine waliuliza, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?” (Yohana 9:16). Bado licha ya mkanganyiko wote, wale waliotafuta ukweli walitambua nguvu katika maneno Yake, kwani “Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena” (Yohana 7:46). Wakati Wayahudi walipomuomba Yesu “tuambie wazi” kama alikuwa ndiye Kristo, Alifunua kanuni ambayo inaweza kutusaidia kutofautisha ukweli kutoka kwenye uongo: “Kondoo wangu waisikia sauti yangu,” Alisema, “nami nawajua, nao wanifuata” (Yohana 10:27).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Yohana 7:14–17

Ninapoishi kweli zilizofundishwa na Yesu Kristo, nitakuja kujua kwamba ni za kweli.

Wayahudi walishangaa kwamba Yesu alijua mengi wakati hakusoma (ona mstari wa 15)—angalau, siyo katika njia walizozifahamu. Katika jibu la Yesu, Yeye alifundisha njia tofauti ya kujua ukweli ambayo ipo kwa kila mmoja, bila kujali elimu au hustoria ya mtu. Kwa mujibu wa Yohana 7:14–17, je, ni kwa jinsi gani unaweza kujua kwamba mafundisho ambayo Yesu alifundisha ni ya kweli? Je, ni kwa jinsi gani mchakato huu umekusaidia wewe kukuza ushuhuda wako juu ya injili?

Yohana 8:2–11

Rehema ya Mwokozi ipo kwa wote.

Wakati akiongea kuhusu mchangamano wa Mwokozi na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, Mzee Dale G. Renlund alisema: “Hakika, Mwokozi hakusamehe uzinzi. Lakini Yeye pia hakumhukumu yule mwanamke. Alimtia moyo kubadilisha maisha yake. Alihamasishwa kubadilika kwa sababu ya huruma na rehema Yake. Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia inathibitisha matokeo ya ufuasi wake: ‘Na mwanamke alimtukuza Mungu kutoka saa ile, na kuamini katika jina lake’ [ona Yohana 8:11, tanbihi c]” (“Mchungaji Wetu Mwema,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 30).

Je, ni lini ulijisikia kama mwanamke yule, kupokea rehema badala ya hukumu kutoka kwa Mwokozi? Je, ni lini umekuwa kama waandishi na Mafarisayo, kushitaki au kuhukumu wengine hata ukiwa ungali una dhambi? (ona Yohana 8:7). Je, ni nini kingine unachoweza kujifunza kutokana na jinsi Mwokozi alivyochangamana na waandishi na Mafarisayo na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi? Je, ni nini unajifunza kuhusu msamaha wa Mwokozi unaposoma mistari hii?

Yohana 8:58–59

Je, ni kwa nini Wayahudi walichukizwa wakati Yesu aliposema, “Kabla ya Ibrahimu kuwepo, Mimi niko”?

“Mimi niko” ni neno ambalo Yehova alilitumia kujitambulisha kwa Musa, kama ilivyoandikwa katika Kutoka 3:14. Hivyo Yesu aliposema, “Mimi niko,” alijitambulisha Yeye mwenyewe kama Yehova, Mungu wa Agano la Kale. Wayahudi walichukulia hii kama kukufuru, na chini ya sheria ya Musa, adhabu ilikuwa kifo kwa kupigwa mawe.

Yohana 9

Kupitia changamoto zetu, Mungu anaweza kujionyesha katika maisha yetu.

Kwa sababu matokeo hasi mara nyingi hufuatia dhambi, tunaweza kuangalia baadhi ya bahati mbaya zetu kama matokeo ya matendo maovu. Hata hivyo, wakati wanafunzi wa Mwokozi walipofikiria kwamba mtu alizaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walifanya dhambi, Yesu aliwasahihisha. Je, ni kwa jinsi gani maneno ya Mwokozi katika Yohana 9:3 hubadilisha mtazamo wako kuhusu changamoto zako na changamoto za wengine? Unaposoma Yohana 9, tafakari jinsi “kazi za Mungu zilivyodhihirishwa” (Yohana 9:3). Je, ni kwa jinsi gani zimedhihirishwa ulipokabiliwa na changamoto?

Inavutia pia kukumbuka kwamba swali la wanafunzi katika Yohana 9:2 lilifunua kwamba wao waliamini katika kuwepo kabla ya kuzaliwa duniani, fundisho ambalo lilipotea kwenye Ukristo wakati wa Ukengeufu Mkuu lakini likarejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith (ona M&M 93:29; Musa 4:1–4; Ibrahimu 3:22–26).

Yohana 10:16

Je, ni nani hao “kondoo wengine” Mwokozi aliomaanisha katika Yohana 10:16?

Wakati Mwokozi alipotembelea mabara ya Amerika baada ya ufufuko Wake, Alielezea ni nani walikuwa kondoo Wake wengine (ona 3 Nefi 15:21–16:5).

ikoni  ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Yohana 7:24

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuisaidia familia yako kuelewa mafundisho ya Yesu katika Yohana 7:24? Njia moja ni kutoka nje na kumfanya mwanafamilia mmoja achafuke. Je, wageni wanaweza kufikiria nini juu ya mwanafamilia huyu kwa kuangalia muonekano wake wa nje? Orodhesha baadhi ya sifa nzuri alizonazo mwanafamilia huyu ambazo haziwezi kuonekana kwa kumuangalia tu (ona pia 1 Samueli 16:7).

Yohana 8:31–36

Je, ni kwa jinsi gani sisi wakati mwingine huwa watumwa wa dhambi? Je, ni ukweli gani uliofundishwa na Yesu unaoweza kutufanya sisi kuwa huru?

Kristo Akimponya Kipofu

Yesu Akimponya Kipofu, na Carl Heinrich Bloch

Yohana 9

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia familia yako kupata taswira ya tukio la Yesu akimponya kipofu katika Yohana 9? Mnaweza kuigiza hadithi pamoja au kuonyesha video “Yesu Akimponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu” (LDS.org). Simamisha hadithi mara chache ili kwamba wanafamilia waweze kusoma mistari inayohusika kutoka Yohana 9. Waalike kuandika somo lolote wanalojifunza kutoka kwenye tukio hili, kama vile inamaanisha nini kuongoka kwenye injili ya Yesu Kristo.

Yohana 10:1–18, 27–29

Ili kuwashirikisha wanafamilia kujifunza kutoka kwenye fumbo la Mchungaji Mwema, waombe kila mmoja kuchora picha ya mojawapo ya vitu vifuatavyo: mwizi, mlango, mchungaji, kibarua (mfanyakazi wa kukodiwa), mbwa mwitu, na kondoo. Waalike kusoma Yohana 10:1–18, 27–29, na kisha jadilini kama familia nini Mwokozi alifundisha kuhusu vitu walivyochora.

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Tafuta maneno na virai vyenye mwongozo. Unaposoma, Roho anaweza kukuletea maneno au virai kadha wa kadha ambavyo hukupa mwongozo na kukupa hamasa au kuvifanya vionekane kana kwamba vimeandikwa kwa ajili yako. Fikiria kuandika maneno au virai vyovyote vinavyokupa mwongozo katika Yohana 7–10.

Kristo na kondoo

Hakupotea Tena, na Greg K. Olsen