Njoo, Unifuate
Mei 20–26. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako’


“Mei 20–26. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Mei 20–26. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
mtu juu ya mti wakati Yesu akikaribia

Zakayo katika Mti wa Mkuyu, na James Tissot

Mei 20–26.

Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12

“Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako”

Kabla ya kusoma mawazo katika muhtasari huu, soma Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; na Yohana 12. Andika kumbukumbu ya mawazo ambayo unaweza kushiriki na familia yako au katika madarasa yako kanisani.

Andika Misukumo Yako

Mwokozi alikuwa na njaa baada ya kusafiri kutoka Bethania kwenda Yerusalemu, na mti wa mtini kwa mbali ulionekana kama chanzo cha chakula. Lakini Yesu alipoukaribia mti, alikuta kwamba haukuwa na matunda (ona Mathayo 21:17–20; Marko 11:12–14, 20). Kwa namna fulani, mti wa mtini ulikuwa kama viongozi wa dini wanafiki katika Yerusalemu: mafundisho yao matupu na kuonyesha utakatifu kwa nje haukutoa lishe ya kiroho. Mafarisayo na waandishi walionekana kutii amri nyingi lakini bado walikosa amri kuu mbili: kumpenda Mungu na kumpenda jirani yako kama nafsi yako (ona Mathayo 22:34–40; 23:23).

Kwa upande mwingine, watu wengi walikuwa wameanza kutambua matunda mazuri katika mafundisho ya Yesu. Alipofika Yerusalemu, walimkaribisha kwa matawi yaliyokatwa kutoka kwenye miti kumuandalia njia Yake, wakishangilia kwamba hatimaye, kama unabii wa kale ulivyosema, “Mfalme wako anakuja kwako” (Zakaria 9:9). Unaposoma wiki hii, fikiria kuhusu matunda ya mafundisho ya Mwokozi na dhabihu ya kulipia dhambi katika maisha yako na kwa jinsi gani unaweza kutoa “mazao mengi” (Yohana 12:24).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 23; Luka 19:1–10; 20:45–47

Bwana hahukumu kwa muonekano wa nje bali kwa matamanio ya moyo.

Katika siku za Yesu, watu wengi walidhania kwamba watoza ushuru, au wakusanya kodi, hawakuwa waaminifu na waliwaibia watu. Hivyo kwa sababu Zakayo, mtoza ushuru mkuu, alikuwa tajiri, aliweza hata kutiliwa shaka zaidi. Lakini Yesu aliangalia moyo wa Zakayo. Je, Luka 19:1–10 hufunua nini kuhusu moyo wa Zakayo? Unaweza kuandika maneno katika mistari hii ambayo huelezea ni kitu gani Zakayo alifanya kuonyesha kujitoa kwake kwa Mwokozi. Je, ni yapi matamanio ya moyo wako? Je, unafanya nini ili kumtafuta Mwokozi, kama Zakayo alivyofanya?

Mchangamano wa Mwokozi na waandishi na Mafarisayo unatengeneza utofauti wa kuvutia kwenye mchangamano Wake na Zakayo. Kama Rais Dieter F. Uchtdorf alivyoelezea, “[Yesu] alipandwa na hasira ya haki dhidi ya wanafiki kama waandishi, Mafarisayo na Masadukayo—wale ambao walijaribu kuonekana wenye haki ili kupokea sifa, ushawishi na utajiri wa ulimwengu, na wakati huo huo wakidhulumu watu ambao wangepaswa kuwabariki” (“Katika Kuwa Wakweli,” Ensign au Liahona, Mei 2015, 81).

Katika Mathayo 23, Mwokozi alitumia sitiari kadhaa kuelezea unafiki. Fikiria kuwekea alama au kuorodhesha sitiari hizi na kuandika nini zinafundisha kuhusu unafiki. Je, wewe unashawishika kufanya nini tofauti kwa sababu ya mafundisho ya Mwokozi?

Ona pia Mafundisho na Maagano 88:62–63; 137:9; Kamusi ya Biblia, “Mnafiki.”

Mathayo 21:1–11; Marko 11:1–11; Luka 19:29–44; Yohana 12:12–16

Yesu Kristo ni Mfalme wangu

Matukio katika Mathayo 21:1–11; Marko 11:1–11; Luka 19:29–44; na Yohana 12:12–16 huelezea mwanzo wa wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi, ikijumuisha kuingia Kwake kwa shangwe Yerusalemu. Wale waliomtambua kama Mfalme wao walionyesha kujitoa kwao kwa kumpaka mafuta (ona Yohana 12:1–8), kutandaza nguo na matawi ya mitende katika njia Yake ya kuingia Yerusalemu, na wakipiga kelele za sifa. Fikiria jinsi gani nyenzo hizi zinavyoweza kuongeza uelewa wako wa matukio yaliyoanza wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kumpokea Mwokozi kama Bwana na Mfalme wako?

Ona pia “Kuingia kwa Bwana Yerusalemu kwa Shangwe” (video, LDS.org).

Mathayo 22:34–40

Amri mbili kuu ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine kama nafsi yangu.

Kama umewahi kuhisi kushindwa unapojitahidi kumfuata Yesu Kristo, maneno ya Mwokozi kwa mwanasheria katika Mathayo 22 yanaweza kukusaidia kurahisisha na kuzingatia ufuasi wako. Hii ni njia mojawapo ya kufanya hili: Tengeneza orodha ya amri kadhaa za Bwana. Je, ni kwa jinsi gani kila amri katika orodha yako huunganika kwenye amri kuu mbili? Je, ni kwa jinsi gani kuzingatia kwenye amri hizi kuu mbili hukusaidia kushika hizo nyingine?

Mathayo 23:5

Je, hirizi ni nini?

Hirizi ilikuwa ni visanduku vya ngozi vilivyokuwa na utepe wa karatasi za ngozi zikiwa na vifungu vya maandiko juu yake. Wayahudi walibana visanduku hivi vidogo kwenye mkanda wa ngozi na kuvivaa kuzunguka vichwa vyao au mikono kama njia ya kukumbuka amri (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–8). Kwa kujiinua, Mafarisayo walivaa hirizi kubwa kupita kiasi ili kwamba kila mtu angeona jinsi walivyopenda sana neno la Mungu.

Picha
ikoni ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Yohana 12:1–8

Je, ni kwa jinsi gani Mariamu alionyesha upendo wake kwa Mwokozi? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaonyesha upendo wetu Kwake?

Picha
mwanamke akipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake

Kuosha Miguu ya Yesu na Brian Call

Yohana 12:42–43

Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuonyesha heshima kwa wengine pale wanapoelezea au kutetea imani zao za kidini? Je, ni matokeo gani ya kijamii wakati mwingine hutuvunja moyo kuelezea au kutetea imani yetu katika Kristo? Kwa mfano wa watu ambao hawakukubali kushindwa na shinikizo la kijamii, ona Danieli 1:3–20; 3; 6; Yohana 7:45–53; 9:1–38; na Mosia 17:1–4.

Mathayo 21:12–17

Je, ni kwa jinsi gani tunaonyesha unyenyekevu na heshima yetu kwa hekalu? Je, ni kitu gani tunaweza “kutupa nje” ya maisha yetu ambacho hutuzuia kupata uzoefu wa hekalu kama “nyumba ya sala” (Mathayo 21:12–13) na mahali pa uponyaji wa kiroho? Fikiria kuimba “Napenda kuona Hekalu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95.

Mathayo 21:28–32

Je, ni masomo gani kutoka kwenye mfano wa mtu mwenye wana wawili yanaweza kuisaidia familia yako? Kwa mfano, unaweza kutumia hadithi kujadili umuhimu wa utiifu wa dhati na toba. Pengine familia yako inaweza kuandika mfano huu kama muswada wa mchezo wa kuigiza na kupeana zamu kuigiza majukumu tofauti.

Mathayo 22:15–22

Je, ni vipi baadhi ya “vitu ambavyo ni vya Mungu” (mstari 21) ambavyo tunapaswa kumpa?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia Sanaa Kuwashirikisha wanafamiliaKitabu cha Sanaa ya Injili na LDS Maktaba ya Vyombo vya habari kwenye LDS.org kuna picha nyingi na video ambazo zinaweza kusaidia [familia yako] kupata taswira ya dhana au matukio” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22). Kwa mfano, mchoro unaoambatana na muhtasari huu unaweza kusaidia kuipa uhai hadithi ya kuingia kwa Kristo Yerusalemu.

Picha
Kuingia kwa shangwe kwa Kristo

Kuingia kwa Shangwe, na Walter Rane

Chapisha