Njoo, Unifuate
Mei 20–26. Mathayo 21–23: Marko 11: Luka 19–20: Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako’


“Mei 20–26. Mathayo 21–23; Marko 11: Luka 19–20: Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Mei 20–26. Mathayo 21–23; Marko 11: Luka 19–20: Yohana 12.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

mtu akiwa kwenye mti wakati Yesu anakaribia

Zakayo katika mti wa Mkuyu na James Tissot

Mei 20–26

Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12

“Tazama, Mfalme Wako Anakuja Kwako”

Unaposoma Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; na Yohana 12, tilia maanani misukumo unayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Rejea “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” mwanzoni mwa kitabu hiki cha kiada kwa mambo ya kukumbuka wakati ukifundisha kanuni hizi.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha iliyopo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia, na waalike watoto kushiriki kile wanajua kuhusu kinachotokea katika picha.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Luka 19:1–10

Baba wa Mbinguni na Yesu wananijua mimi kwa jina.

Unaposoma juu ya mwingiliano wa Mwokozi na Zakayo, ni ujumbe gani unaopata ambao unaweza kuwabariki watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha Zakayo juu Mkuyuni (LDS.org). Wasaidie watoto wamtambue Zakayo na kusema jina lake. Buni vitendo vya watoto kufanya wakati unaposimulia hadithi ya Zakayo na Yesu—kwa mfano, wasimame juu ya vidole vyao ili kuona juu ya umati au kujifanya kupanda mti. Eleza kwamba Mwokozi Alimuona Zakayo na kumuita kwa jina. Shuhudia kwamba Mwokozi pia Anajua kila mmoja wa watoto na majina yao.

  • Leta fremu tupu ya picha kwenye darasa, au utengeneze moja kwa kutumia karatasi. Mwalike kila mtoto kuchukua zamu kushika fremu kuzunguka uso wake wakati wanadarasa wengine wakisema, “Baba wa Mbinguni na Yesu wanakujua [jina la mtoto].”

  • Waalike watoto kuchukua zamu wakijifanya kupanda mti, kama vile Zakayo alivyofanya. Waombe wengine katika darasa kusema, “Baba wa Mbinguni na Yesu wanakujua [jina la mtoto].”

  • Imbeni pamoja “Mimi Mwana wa Mungu.” Kitabu cha Nyimbo za watoto, 2–3 na wasaidie watoto kusikiliza vitu ambavyo vitawasaidia kujua Baba wa Mbinguni Anawapenda.

Mathayo 21:12–14

Hekalu ni mahali patakatifu

Ushuhuda wako wa hekalu unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba hekalu ni mahali patakatifu.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha Yesu Akisafisha Hekalu (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 51), na simulia hadithi kama ilivyoandikwa katika Mathayo 21:12–14. Wasaidie watoto kutafuta mchoro ya pesa na wanyama katika picha. Kisha jadili kwa nini Mwokozi Aliwataka wabadilisha pesa na watu wauzao wanyama kuondoka hekaluni.

  • Onyesha picha za mahekalu (kwa mfano, ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, 117–21), na waombe watoto kushiriki jinsi wanavyohisi walionapo hekalu. Waambie watoto kwamba hizo hisia ni Roho Mtakatifu akituambia kwamba hekalu ni sehemu maalum. Waombe watoto kuigiza vile ambavyo wangefanya kama wangekuwa ndani ya hekalu. Kwa mfano, wangezungumza kwa kunong’ona na kukaa kwa staha. Imbeni pamoja “Ninapenda Kuliona Hekalu.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95 na waalike watoto kuweka lengo kuingia ndani ya hekalu siku moja.

Hekalu la Fort Collins, Colorado

Hekalu ni nyumba ya Bwana.

Mathayo 21:28–32

Mimi ninaweza kuwa mtiifu.

Baba wa Mbinguni anataka tuwe watiifu. Fumbo la wana wawili ni fursa kufundisha kuhusu umuhimu wa utiifu.

Shughuli za Yakini

  • Chora picha ya wana wawili ubaoni, na tumia michoro unapopitia fumbo katika Mathayo 21:28–32. Mwana yupi alifanya uamuzi sahihi mwishoni? Waombe watoto kutaja vitu wanavyoweza kuwafanya kuwa watiifu nyumbani. Waache wachore picha zao wenyewe wakifanya mojawapo ya mambo hayo.

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu walioupata kwa kuwa watiifu kwa wazazi wao au mtu mwingine mlezi au kiongozi. Walibarikiwaje kwa kuwa watiifu? Wanawezaje kuwa watiifu zaidi wakati ujao?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Luka 19:1–10

Ninapomtafuta Mwokozi, Nitampata.

Unaweza kutumia hadithi ya Zakayo kuwasaidia watoto kufikiria mambo wanayoweza kufanya kuja karibu kwa Mwokozi.

Shughuli za Yakini

  • Soma Luka 19:1–10, ukitua kila mistari michache kujadili nini tunajifunza kuhusu Zakayo. Ni nini Zakayo alifanya ili aweze kumwona Yesu? Ni kwa jinsi gani alijibu wakati Yesu alimuuliza kushuka toka mtini? Waombe watoto washiriki sababu moja kwa nini wangependa kumwona Yesu. Kama Mwokozi angekuja kwenye mji wako, nini ungefanya kujiandaa?

  • Waalike watoto kufikiria juu ya watu wanaowafahamu ambao, kama Zakayo, wanaweza kuwa wanamtafuta Mwokozi. Waulize watoto nini wangefanya kusaidia mtu mwingine kujifunza kuhusu Mwokozi.

  • Waalike watoto kushiriki uzoefu wakati walihisi kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo aliwafahamu na kuwapenda.

Mathayo 21:12–14

Hekalu ni mahali patakatifu ambapo lazima nipaheshimu.

Ni kwa jinsi gani tukio la Mwokozi akisafisha hekalu linakusaidia kuwafundisha watoto kuhusu utakatifu wa mahekalu?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kusoma Mathayo 21:12–14. Onyesha picha Yesu Akisafisha Hekalu (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 51), na waulize ni mstari gani ulioneshwa katika picha. Waombe wachore picha juu ya vile hekalu lingelionekana kabla na baada ya Yesu kulisafisha.

  • Waalike watoto kushiriki jinsi walivyojisikia wakati walikwenda ndani ya hekalu, walitembelea ardhi ya hekalu, au walipoangalia picha za mahekalu. Ni nini kiliwasaidia kujua kuwa hekalu ni mahali patakatifu?

  • Alika kijana mmoja au zaidi kuja katika darasa na kuongea kuhusu jinsi walivyojiandaa kuingia hekaluni. Kama wamewahi kuwa hekaluni, waombe kuongea jinsi walivyohisi wakati walipokuwa kule.

  • Kata picha ya hekalu katika vipande vya chamsha bongo, na mpe kila mtoto kipande kimoja. Waombe watoto kuandika nyuma ya kipande cha chamsha bongo kitu kimoja wanaweza kufanya kujiandaa kuingia hekaluni. Pale kila mtoto anaposhiriki wazo, ongeza kipande chake kwenye chamsha bongo.

Mathayo 23:25–28

Nahitaji kuwa mwenye haki katika matendo yangu na tamaa zangu.

Yesu alifundisha waandishi na Mafarisayo kuhusu umuhimu juu wa kuishi kikweli injili—siyo kujifanya kuwa mwenye haki. Ni nini kingeweza kuwasaidia watoto kuelewa ukweli huu?

Shughuli za Yakini

  • Unaposoma Matayo 23:25–28 pamoja na watoto, fikiria kushiriki maana hii ya unafiki kutoka kwenye Kamusi ya Biblia: “mmoja ambaye anajifanya kuwa mshika dini wakati siyo.” Kwa nini ni vibaya kuwa mnafiki?

  • Onyesha watoto kikombe ambacho ni kisafi nje lakini kichafu ndani kuwasaidia kuonyesha mfano katika Mathayo 23:25. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuhakikisha tuwa safi na tusio na doa kwa ndani?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kuchagua kanuni au shughuli kutoka darasani za kushiriki na familia zao nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie wazazi wa watoto. Wazazi ni walimu muhimu zaidi wa injili kwa watoto wao—wanalo jukumu kubwa na nguvu kubwa zaidi kuwashawishi watoto wao (ona Kumbukumbu la Torati 6:6–7). Unapofundisha watoto Kanisani, kwa maombi tafuta njia za kuwasaidia wazazi wao katika jukumu lao muhimu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25).

ukurasa wa shughuli: hekalu ni takatifu