“Mei 6–12. Luka 12–17; Yohana 11: ‘Furahini Pamoja Nami, kwa Kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Mei 6–12. Luka 12–17: Yohana 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Mei 6–12.
Luka 12–17; Yohana 11
“Furahini Pamoja Nami, kwa Kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”
Soma kwa maombi Luka 12–17 na Yohana 11, ukitafuta jinsi unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kweli zilizopo katika sura hizi na kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wakumbushe watoto baadhi ya mafumbo na hadithi zilizopo katika Luka 12–17 na Yohana 11, na waalike kuchagua moja na kuchora picha yake.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Baba wa Mbinguni Anawataka wote warudi Kwake.
Waweza kuwepo baadhi ya watoto katika darasa lako wasiohudhuria kila mara. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto unaowafundisha kuwafikia hao wengine kwa upendo?
Shughuli za Yakini
-
Mpe sarafu mtoto mmoja, picha ya kondoo mtoto mwingine, na mtoto mwingine picha ya mwana mpotevu (LDS.org). Eleza hadithi za mafumbo tatu zinazopatikana katika Luka 15 na waalike watoto kuinua juu sarafu au picha picha zao wakati unaelezea. Unaweza kuwaalika watoto kuelezeana mafumbo mmoja na mwingine kwa maneno yao wenyewe.
-
Waombe watoto washiriki uzoefu wao wakati walimepoteza kitu. Eleza kuwa watu wanaweza kupotea kiroho wakati hawahisi upendo wa Mungu au wanapogeuka kutoka Kwake. Shuhudia kwamba haya mafumbo yanafundisha kwamba Mungu anataka sisi kuwasaidia watu waliopotea kurudi Kwake.
-
Waalike wanafunzi kufikiria watoto wengine ambao hawaji kwenye Msingi. Wasaidie kuandika maneno machache kuwaalika hawa watoto kuhudhuria Msingi au shughuli za Msingi. Kwa namna gani nyingine tunaweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwao?
Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Baba wa Mbinguni kwa kuwa mwenye shukrani kwa baraka zangu.
Ni kwa namna gani hadithi ya wakoma kumi inahimiza watoto kuwa wenye shukrani?
Shughuli za Yakini
-
Elezea hadithi ya wakoma kumi walioponywa na Yesu. Onyesha picha iliyopo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na waalike watoto kuhesabu hadi kumi katika vidole vyao. Halafu waulize kuweka chini vidole kumi kumuonyesha mkoma mmoja aliye mshukuru Yesu. Ni lini watoto walitoa shukrani zao kwa rafiki au mpendwa wao?
-
Alika kila mtoto kufanya kitu kinachoashiria shukrani zao kwacho na uulize watoto wengine kukisia kitu hicho ni nini. Waulize watoto kushiriki njia ambazo tunaweza kumwonyesha Baba wa Mbinguni kuwa tunashukuru kwa ajili ya baraka zetu.
Tunaamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
Martha, ambaye alikuwa dada wa Lazaro, alimwambia Yesu: “Ninaamini kwamba Wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu” (Yohana 11:27). Hadithi ya Mariamu, Martha, na Lazaro inaweza kuimarisha ushuhuda wa watoto juu ya Yesu Kristo.
Shughuli za Yakini
-
Fanya muhtasari hadithi ya Yesu akimfufua Lazaro kutoka kwa wafu (ona pia ”Sura 43:Yesu Kumfufua Lazaro” Hadithi za Agano Jipya, 107–9, au video inayofanana katika LDS.org) na onyesha tawi lililo kufa na tawi lililo hai. Shiriki ushuhuda wako kwamba kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo, watu wote watafufuliwa na kuishi milele.
-
Wasaidie watoto kukariri kirai ambacho Yesu alikisema kwa Martha: “Mimi Ndimi huo ufufuo, na uzima” (Yohana 11:25)). Elezea kwamba kwa sababu ya Ufufuko wa Mwokozi, tutawaona tena wapendwa wetu waliofariki.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Mimi ninaweza kumsaidia Yesu kumtafuta kondoo Wake aliyepotea.
Watoto waweza kutojua kwamba kuna wengine katika darasa ambao hawahudhurii Msingi. Unawezaje kuwahamasisha kuwafikia hawa watoto wengine?
Shughuli za Yakini
-
Acha kila mtoto asome kimoyomoyo fumbo la kondoo aliyepotea au fumbo la sarafu iliyopotea, ipatikanayo katika Luka 15:1–10, na ushiriki kile walichojifunza.
-
Andika majina haya katika ubao: baba, mwana mkubwa, na mwana mdogo. Onyesha video “Mwana mpotevu” (LDS.org) na simamisha mara kadhaa ili watoto waandike katika ubao baadhi ya hisia za watu walioorodheshwa.
-
Muombe mtoto kutoka katika chumba wakati wengine wakiificha sarafu au karatasi yenye kondoo. Muite mtoto arudi na kutafuta sarafu au kondoo. Wakumbushe watoto kwamba watu wanaweza kupoteza baraka za injili. Waalike wafikirie njia wanazoweza kutumia kuwafikia hao wengine. Imba pamoja na watoto “Kipenzi kwa Moyo wa Mchungaji.” Wimbo, na. 221, na shuhudia furaha inayokuja pale watu wanamrudia Mungu.
-
Elezea kwamba Yesu alitumia kondoo aliyepotea, sarafu iliyopotea, na mwana mpotevu kuwakilisha watu walio “potea” kwa sababu hawana baraka za injili. Waalike watoto wafikirie juu ya watu wanaowafahamu wasiokuja kanisani. Ni kitu gani wanaweza kufanya kuwasaidia watu hawa kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwao?
Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Baba wa Mbinguni kwa kuwa mwenye shukrani kwa ajili ya baraka zangu.
Hadithi ya wakoma kumi inaweza kuwa njia nzuri kuwahamasisha watoto kumshukuru Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka zao.
Shughuli za Yakini
-
Someni pamoja tukio la wakoma kumi. Ni kwa namna gani mkoma aliyetoa shukrani alibarikiwa kwa ajili ya shukrani zake? Kwa nini ni muhimu kumshukuru Mungu kwa baraka zetu?
-
Waalike watoto kuorodhesha vitu wanavyoshukuru kwa ajili yavyo ambavyo vinaanza na kila herufi ya jina lao.
-
Waulize watoto kuandika ujumbe wa-ahsante kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya baraka alizowapa. Wanaweza kutundika jumbe hizo katika vitanda vyao kuwakumbusha kushukuru wanaposali.
Tunaamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
Unawezaje kutumia hadithi ya Mariamu, Martha, na Lazaro kuwasaidia watoto kujua, kama Martha alivyojua, kwamba Yesu ni “Kristo, Mwana wa Mungu”? Yohana 11:27.
Shughuli za Yakini
-
Andika ubaoni baadhi ya kauli zilizozungumziwa na watu katika Yohana 11. Waalike watoto kukisia nani alisema kila kauli, na waulize kupekua Yohana 11 kuhakikisha makisio yao. Wangehisi vipi kama wangelikuwa Yesu, Martha, Mariamu, au Lazaro? Ni kwa jinsi gani kuamini katika Yesu kunatusaidia wakati tuna huzuni au hofu?
-
Soma ushuhuda wa Martha, unaopatikana katika Yohana 11:20–27. Waombe watoto watafute maneno na virai ambavyo vinaonyesha Martha alikuwa na imani. Tunaweza kufanya nini ili kuwa na imani wakati ni vigumu?
-
Wasaidie watoto kukariri Yohana 11:25. Elezea kwamba kila mtu atafufuliwa, lakini ni watenda haki tu watapokea uzima wa milele na kuishi pamoja Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo tena.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wapatie watoto karatasi au daftari dogo ambalo wanaweza kuandikia au kuchora vitu ambavyo wanashukuru katika wiki yote.