Njoo, Unifuate
Mei 6–12. Luka 12–17; Yohana 11: ‘Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea’


“Mei 6–12. Luka 12–17; Yohana 11: ‘Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Mei 6–12. Luka 12–17; Yohana 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019

Picha
mtu akimkumbatia mwanaye

Mwana Mpotevu, na Liz Lemon Swindle

Mei 6–12.

Luka 12–17; Yohana 11

“Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”

Unaposoma Luka 12–17 na Yohana 11, kwa maombi tafuta kile Baba wa Mbinguni anataka ujue na ufanye. Kujifunza kwako kwa sura hizi kunaweza kufungua moyo wako kwa jumbe zilizokusudiwa tu kwa ajili yako.

Andika Misukumo Yako

Katika hali nyingi, 99 kati ya 100 wangeweza kufikiriwa kuwa bora sana—lakini siyo wakati idadi kama hizo husimamia watoto wapendwa wa Mungu (ona M&M 18:10). Kama ni hivyo, hata nafsi moja hustahili kwa ukamilifu, kutafutwa “mpaka [sisi] tuipate” (Luka 15:4), kama Mwokozi alivyofundisha katika fumbo la kondoo aliyepotea. Kisha kushangilia kunaweza kuanza, kwani “kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda, ambao hawana haja ya kutubu” (Luka 15:7). Kama hilo linaonekana si sawa, itasaidia kukumbuka kwamba, katika ukweli, hakuna yeyote ambaye “haitaji toba.” Sote tunahitaji kuokolewa. Na wote tunaweza kushiriki katika kuokoa, kufurahi pamoja juu ya kila nafsi inayookolewa (ona M&M 18:15–16).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Luka 12; 14–16

Ninapaswa kuweka moyo wangu kwenye mambo ya muhimu ya milele kuliko kwenye mambo ya ulimwengu huu.

Kwa nini Mungu angesema “Mpumbavu wewe” kwa mchapakazi, mwenye mafanikio ambaye alijenga maghala makubwa na kuyajaza matunda ya kazi zake? (ona Luka 12:16–21). Katika sura hizi katika Luka, Mwokozi hufundisha mifano kadhaa inayoweza kutusaidia sisi kuinua mtazamo wetu kupita ulimwengu kwenda umilele. Baadhi ya mifano hii imeorodheshwa hapa. Ni kwa jinsi gani unaweza kufanyia muhtasari ujumbe wa kila mmoja? Unafikiri Bwana anakuambia nini?

Ona pia Mathayo 6:19–34; 2 Nefi 9:30; Mafundisho na Maagano 25:10.

luka 15

Baba wa Mbinguni hufurahia wakati wale waliopotea wanapopatikana.

Umewahi kujiuliza jinsi Baba wa Mbinguni anavyohisi kuhusu wale waliotenda dhambi au kwa upande mwingine “kupotea”? Mafarisayo na waandishi walimkosoa Yesu hata kwa kuchangamana na watu kama hao. Katika kujibu, Yesu aliwaambia mifano mitatu, inayopatikana katika Luka 15—mifano ya kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea, na mwana mpotevu.

Unaposoma mifano hii, fikiria kuweka orodha ya mifanano na tofauti kati yao. Kwa mfano, unaweza kutafuta kile kilichopotea na kwa nini, jinsi kilivyopatikana, na jinsi watu walivyofanya wakati kilipopatikana. Ni jumbe gani Yesu alikuwa nazo kwa wale walio “potea”—ikijumuisha wale ambao hawadhani wamepotea? Ni jumbe gani alikuwa nazo kwa watu wanaowatafuta wale waliopotea?

Ndiyo, daima ni vizuri kutokuwa mpotevu. Kuhusu Luka 15:7, Mzee James E. Talmage aliandika, “hakuna uthibitisho wa hitimisho kwamba mwenye dhambi anayetubu anapewa umuhimu wa kwanza juu ya nafsi njema ambayo ilikataa dhambi” (Yesu Kristo [1916], 461). Kwa hali yoyote, sote tunatenda dhambi na tunahitaji kuokolewa, na ujumbe wa faraja wa mafumbo ya Mwokozi ni kwamba kila mmoja wetu anaweza kutubu na kurudi katika haki, kwani Mungu hutamani kwamba hata nafsi moja isipotee.

Ona pia Mafundisho na Maagano 18:10–16; Jeffrey R. Holland, “Mpotevu Mwingine,” Ensign, Mei 2002, 62–64.

Picha
Mwanamke akitafuta sarafu

Kipande cha Fedha Kilichopotea, na James Tissot

Luka 16:1–12

Ni nini Kristo alikuwa akifundisha katika fumbo la mkadamu dhalimu?

Mzee James E. Talmage alielezea somo moja tunaloweza kujifunza kutoka kwenye fumbo hili: “Kuwa mwenye bidii; kwani siku ambayo unaweza kutumia utajiri wako wa duniani karibuni itapita. Chukua funzo hata kutoka kwa wasio waaminifu na waovu; kama wana busara ya kujiandaa kwa ajili ya wakati ujao wanaoweza tu kuufikiria, jinsi gani zaidi unapaswa wewe, ambaye unaamini katika milele ijayo, kujiandaa kwa ajili hiyo! Kama hujajifunza hekima na busara katika matumizi ya ‘utajiri usio wa utiifu,’ jinsi gani unaweza kuaminiwa na utajiri zaidi wa kudumu?” (Yesu Kristo, 464).

Luka 5:11–19

Shukrani kwa ajili ya baraka zangu kutanisogeza karibu na Mungu.

Kama ungekuwa mmoja wa wenye ukoma kumi, unafikiri ungerudi kumshukuru Mwokozi? Ni baraka gani za ziada mkoma mwenye shukrani alipokea kwa sababu alitoa shukrani? Ni kwa jinsi gani kutoa shukrani kunakuathiri kiroho? Itakusaidia kuanza kuandika kile unachoshukuru katika shajara yako, kama Rais Henry B. Eyring alivyoelezea katika ujumbe huu “Ee Kumbuka, Kumbuka” (Ensign au Liahona, Nov. 2007, 66–69).

Yohana 11:1–46

Yesu Kristo ni Ufufuo na Uzima.

Muujiza wa kumfufua Lazaro kutoka wafu ulikuwa ni ushuhuda wa nguvu na dhahiri kwamba Yesu alikuwa kweli Mwana wa Mungu na Masiya aliyeahidiwa. Ni maneno gani, vifungu, au utondoti katika Yohana 11:1–46 huimarisha imani yako kwamba Yesu Kristo ni “ufufuo, na uzima”? Ni kwa jinsi gani maarifa haya hushawishi maisha yako na chaguzi zako?

Picha
ikoni ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Luka 15:1–10

Je, wanafamilia wako wanaelewa jinsi ilivyo kupoteza kitu—au kupotea? Kuzungumza kuhusu uzoefu wao kunaweza kuanzisha majadiliano kuhusu mafumbo ya kondoo aliyepotea na shilingi iliyopotea. Au mnaweza kucheza mchezo ambapo mmoja anajificha na wanafamilia wengine wanajaribu kumtafuta. Ni kwa jinsi gani shughuli hii hutusaidia kuelewa mafumbo haya?

Luka 15:11–32

Ni kwa insi gani tunaweza kuwa kama baba katika hadithi hii tunapokuwa na mpendwa aliyepotea? Nini tunaweza kujifunza kutoka kwa uzoefu wa kijana mkubwa kinachoweza kutusaidia kuwa zaidi kama Kristo? Ni kwa njia zipi baba katika fumbo hili ni kama Baba yetu wa Mbinguni?

Luka 5:11–19

Kuwasaidia wanafamilia kutumia hili tukio la wakoma kumi, unaweza kuwaalika kuandika ujumbe wa siri wa shukrani na kuuweka kote katika nyumba. Mnaweza pia kuimba pamoja “Hesabu Baraka Zako,” Nyimbo za Kanisa, namba. 241, na kujadili baraka ambazo familia yako imepokea.

Yohana 11:1–46

Wanafamilia wanaweza kuangalia filamu “Lazaro Anafufuliwa kutoka Wafu” (LDS.org) na kushiriki shuhuda zao za Yesu Kristo.

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia hadithi na mifano kufundisha kanuni za injili. Mwokozi mara nyingi alifundisha kuhusu kanuni za injili kwa kutumia hadithi na mafumbo. Fikiria mifano na hadithi kutoka maisha yako mwenyewe ambazo zinaweza kufanya kanuni za injili kuwa hai kwa familia yako (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22).

Picha
mtu akipiga magoti kwa shukrani mbele ya Yesu

Wako Wapi wale Kenda, na Liz Lemon Swindle

Chapisha