Njoo, Unifuate
Mei 13–19. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18: ‘Nimepungukiwa na Nini Tena?’


“Mei 13–19. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18: ‘Nimepungukiwa na Nini Tena?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Mei 13–19. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Vibarua katika shamba la mizabibu

Mei 13–19.

Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18

“Nimepungukiwa na Nini Tena?”

Soma na kutafakari Mathayo 19–20; Marko 10; na Luka 18, ukitilia maanani ushawishi unaopokea. Andika ushawishi huo, na azimia jinsi utakavyoutendea kazi.

Andika Misukumo Yako

Kama ungepata nafasi ya kumuuliza Mwokozi swali, lingekua swali gani? Wakati kijana mmoja tajiri alipokutana na Mwokozi kwa mara ya kwanza, alimuuliza, “nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?” (Mathayo 19:16). Jibu la Mwokozi lilionyesha yote shukrani kwa mambo mema ambayo kijana tayari amekwisha tenda na kumtia moyo kwa upendo ili afanye zaidi. Tunapotafakari uwezekano wa uzima wa milele, tunaweza pia kujiuliza kama kuna zaidi tunapaswa kufanya. Tunapouliza, katika njia yetu wenyewe, “Nimepungukiwa na Nini Tena?” (Mathayo 19:20), Bwana anaweza kutupatia majibu ambayo ni ya kibinafsi kama jibu Lake kwa kijana tajiri. Chochote Bwana anachotutaka tufanye, kufanyia kazi jibu Lake daima kutahitaji tumuamini Yeye zaidi kuliko wema wetu wenyewe (ona Luka 18:9–14) na kwamba “tuupokee ufalme wa Mungu kama mtoto vile mdogo” (Luka 18:17; ona pia 3 Nefi 9:22).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 19:1–9; Marko 10:1–12

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetawazwa na Mungu.

Majibizano kati ya Mwokozi na Mafarisayo ni moja kati ya matukio machache yaliyoandikwa ambapo Mwokozi alifundisha mahususi kuhusu ndoa. Baada ya kusoma Mathayo 19:1–9 na Marko 10:1–12, andika orodha ya kauli kadhaa ambazo unahisi ni muhtasari wa mtazamo wa Mwokozi juu ya ndoa. Kisha jifunze “Ndoa” katika Mada za Injili, topics.lds.org, na ongeza kauli zaidi kwenye orodha yako unapozigundua. Je, ni kwa jinsi gani ufahamu wako juu ya mpango wa Baba wa wokovu hukusaidia kuelewa kwa nini ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetawazwa na Mungu?

wana ndoa wazee wakiwa mbele ya hekalu

Ndoa ya milele ni sehemu ya mpango wa Mungu.

Unaweza kuwafahamu watu ambao hawakubaliani au wanaopinga viwango vya Bwana kuhusu ndoa. Kwa msaada wa ufafanuzi wa jinsi ya kuwa na maongezi ya heshima na wao, tazama filamu ya “Everyday Example: When Beliefs Are Questioned” (LDS.org).

Mathayo 19:3–9; Marko 10:2–12

Je, Yesu alifundisha kwamba talaka kamwe haikubaliki au kwamba watu waliotalikiana wasiingie tena kwenye ndoa?

Katika hotuba juu ya talaka, Mzee Dallin H. Oaks alifundisha kwamba Baba wa Mbinguni hukusudia kwamba uhusiano wa ndoa uwe wa milele. Hata hivyo, Mungu pia huelewa kwamba “kwa sababu ya ugumu wa mioyo [yetu]” (Mathayo 19:8), ikijumuisha chaguzi duni na ubinafsi wa mmoja wa wenza au wote, talaka wakati mwingine ni muhimu.

Mzee Oaks alieleza kwamba Bwana “huruhusu watu waliotalikiana kuingia tena kwenye ndoa bila doa la ukosefu wa maadili ulioainishwa katika sheria ya juu. Isipokuwa muumini mtalikiwa amefanya uvunjaji mkubwa wa sheria, anaweza kustahili kibali cha hekaluni chini ya viwango vya ustahili vinavyotumika kwa waumini wengine” (“Talaka,” Ensign au Liahona, Mei 2007, 70).

Ona pia “Talaka,” Mada za Injili, topics.lds.org.

Mathayo 19:16–22; Marko 10:17–22; Luka 18:18–23

Kama nikimwomba Bwana, atanifundisha ninachopaswa kufanya ili kuurithi uzima wa milele.

Hadithi ya kijana tajiri inaweza kutoa msito hata kwa mfuasi mwaminifu, wa maisha yote. Unaposoma Marko 10:17–22, unapata ushahidi gani wa uaminifu na unyoofu wa kijana ?

Kama kijana tajiri, sisi sote si wakamilifu na tuna upungufu, hivyo kama wafuasi yatupasa kuuliza, “Nimepungukiwa na nini tena?”—na tunapaswa tujiulize swali hili maisha yetu yote. Tambua kwamba jibu linatolewa kwa upendo kutoka kwa Mmoja anayetutazama kwa jinsi tulivyo hasa (ona Marko 10:21). Je, unaweza kufanya nini ili kujiandaa kumwomba Bwana kujua kile unachopungukiwa—na kukubali jibu Lake?

Ona pia Larry R. Lawrence, “Nimepungukiwa Nini Tena?” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 33–35; S. Mark Palmer, “Kisha Yesu Akamtazama Akampenda,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 114–16.

Mathayo 20:1–16

Kila mmoja anaweza kupokea baraka ya uzima wa milele, bila kujali lini wamepokea injili.

Je, unaweza kutoa maelezo ya uzoefu wa mkulima yeyote katika shamba la mizabibu? Ni mafunzo gani unapata kwa ajili yako katika kifungu hiki? Ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Wakulima katika Shamba la Mizabibu” (Ensign au Liahona, Mei 2012, 31–33) unaweza kukusaidia kuona njia mpya za kutumia mfano huu. Je, ni ushawishi gani wa ziada Roho anaokupatia?

ikoni ya kujifunza kwa familia.

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Mathayo 19:1–9; Marko 10:1–12

Je, familia yako itanufaika kwa kujadili mafundisho ya Mungu kuhusu ndoa na familia? Kama ndivyo, mnaweza kusoma “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (Ensign au Liahona, Nov. 2010, 129). Je, ni kwa jinsi gani mafundisho katika tangazo husaidia kuondoa mkanganyiko na uongo katika ujumbe wa ulimwengu kuhusu ndoa na familia?

Marko 10:23–27

Je, nini tofauti kati ya kuwa na utajiri na kuamini katika utajiri? (ona Marko 10:23–24). Unaposoma mstari wa 27, unaweza kutaka kuonyesha Tafsiri ya Joseph Smith: “Kwa watu wanaoamini katika utajiri, haiwezekani; lakini sivyo kwa watu wanaomwamini Mungu na kuacha vyote kwa ajili yangu, kwani kama hao mambo yote haya yanawezekana” (katika Marko 10:27, tanbihi a).

Mathayo 20:1–16

Ili kuonyesha kanuni zilizopo katika Mathayo 20:1–16, unaweza kufanya shindano rahisi, kama vile mbio fupi, na kuahidi kwamba mshindi atapata zawadi. Baada ya kila mtu kumaliza shindano, mzawadie kila mmoja zawadi inayofanana, ukianzia na aliyemaliza mwisho na kumalizia na aliyemaliza wa kwanza. Je, hii inatufundisha nini kuhusu anayepokea baraka ya uzima wa milele katika mpango wa Baba wa Mbinguni?

Mathayo 20:25–27; Marko 10:42–45

Je, nini maana ya kifungu hiki “Na mtu yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu”? (Mathayo 20:27). Je, ni kwa jinsi gani Yesu Kristo alionyesha mfano wa kanuni hii? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano Wake katika familia zetu, kata au tawi letu, na maeneo yanayotuzunguka?

Luka 18:1–14

Je, tunajifunza nini kuhusu sala kutoka kwenye mifano hii miwili katika mistari hii?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi.

Tafuta muda ambao unafaa kwako. Ni rahisi mara kwa mara kujifunza pale unapoweza kusoma maandiko bila kubugudhiwa. Tafuta muda ambao unafaa kwako, na fanya kwa uwezo wako wote kuwa na msimamo wa kujifunza katika muda ule kila siku.

Kristo na kijana tajiri

Kristo na Kijana Tajiri Mtawala, na Heinrich Hofmann