Njoo, Unifuate
Aprili 29–Mei 5. Yohana 7–10: ‘Mimi Ndimi Mchungaji Mwema’


Aprili 29–Mei 5. Yohana 7–10: ‘Mimi Ndimi Mchungaji Mwema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

Aprili 29–Mei 5. Yohana 7–10.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Kristo na mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi

Yeye Asiye na Dhambi, na Liz Lemon Swindle

Aprili 29–Mei 5

Yohana 7–10

“Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”

Unaposoma Yohana 7–10, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Mawazo mengi ya watoto wakubwa katika toleo hili yanaweza pia kuchukuliwa kwa ajili ya watoto wadogo au kinyume chake.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Alika watoto washiriki kitu walifanya wiki iliyopita kuwa kama Msamaria mwema.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Yohana 7:14–17

Kuzishika amri kutanisaidia kujua ni za kweli.

Yesu alifundisha kwamba tunaweza kupata ushuhuda wa kweli alizoshiriki tunapoziishi. Unawezaje kutumia simulizi hii kuwafundisha watoto kwamba amani tunayojisikia wakati tunatii amri inatusaidia kujua ni za kweli?

Shughuli za Yakini

  • Fanya muhtasari Yohana 7:17 katika maneno ambayo watoto wataelewa. Wasaidie kujua kwamba kutii amri hutusaidia kuhisi tu karibu na Yesu Kristo, labda kwa kuimba kwa pamoja “Tii Amri” au “Chagua Njia Sahihi” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47, 160–61. Waombe watoto wasikilize ni jinsi gani tutabarikiwa tunapotii amri.

  • Shiriki uzoefu ulipojifunza amri ilitoka kwa Mungu kwa sababu uliishi, kama vile kulipa zaka au kumsamehe mtu fulani aliyekuwa sio mkarimu. Waalike watoto kufikiria juu ya uzoefu waliopata walipotii amri. Waulize, “Ulijisikiaje ulipotii?”

  • Chagua baadhi ya amri na uchore seti mbili za picha rahisi zinazowakilisha kila amri. Zilaze picha zote kwa kuangalia chini katika ardhi na waalike watoto kuchukua zamu kuoanisha amri pamoja. Shuhudia juu ya umuhimu wa amri na jinsi kuzifuata kumeimarisha ushuhuda wako.

Yohana 8:29

Yesu alimtii Baba Yake.

Yesu Kristo daima Alifanya vitu vilivyompendeza Baba Yake wa Mbinguni. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kutafuta njia za kufuata mfano Wake?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kurudia kile Yesu Alisema kuhusu Baba wa Mbinguni katika Yohana 8:29: “Nafanya siku zote yale yampendezayo.” Waombe washiriki vitu Yesu Alifanya vilivyomfanya Baba wa Mbinguni Afurahi. Waonyeshe baadhi ya picha kutoka katika Kitabu cha Sanaa ya Injili kuwapa wao mawazo.

  • Waulize watoto ni nini huwafanya kuwa na furaha. Kisha waulize ni nini ambacho wanaweza kufanya wiki hii kumfanya mwanafamilia au rafiki afurahie. Waalike watoto kuchora picha zao binafsi wakifanya hizo shughuli, wazipeleke nyumbani na ili kuwakumbusha.

  • Mwalike mzazi wa mmoja wa watoto kushiriki uzoefu ambapo mtoto alifanya kitu ambacho kilimfanya mzazi afurahi. Mwache mtoto ashiriki jinsi alivyojihisi.

Yohana 10:1–18

Yesu ananijua na ananipenda.

Fumbo la mchungaji mwema linaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Yesu anawapenda na Anawajua wao ni akina nani.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto wachore picha inayowakilisha kitu fulani katika fumbo la mchungaji mwema, kama kondoo, jambazi, au mbwa mwitu. Wasomee Yohana 10:1–18 watoto, na uwaombe washikilie juu picha zao wanapokusikia ukisoma kuhusu walichokichora. Elezea kwamba kama tu “mchungaji mwema” anavyotuongoza na kupenda kundi lake, Yesu anatupenda na kutuongoza sote kurudi Kwake. Mvalishe mmoja wa watoto kama mchungaji, na waache watoto washiriki ni jinsi gani Yesu yu kama mchungaji kwetu.

  • Onyesha picha ya Yesu na wanakondoo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Tunajuaje kwamba Yesu Kristo anawapenda wanakondoo? Tunawezaje kuelezea kwamba wanakondoo wanampenda Yesu?

  • Wasaidie watoto kukamilisha ukurasa wa shughuli ya wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Yohana 7:14–17

Kuzishika amri kutanisaidia kujua ni za kweli.

Wewe na watoto unaowafundisha mnaweza kuwa na uzoefu katika kuishi kweli za injili na kujifunza kuwa ni za kweli. Unawezaje kujenga juu ya uzoefu huo unapofundisha?

Shughuli za Yakini

  • Andika kila mstari wa Yohana 7:14–17 katika vipande tofauti vya karatasi na vionyeshe katika utaratibu usio na utaratibu. Waombe watoto waziweke katika utaratibu sahihi na kuangalia Yohana 7:14–17 kuona kama ziko sahihi. Waalike watoto kugawanyika katika jozi na kushiriki uelewa wao wa kila mstari na mwenzake. Ni kwa jinsi gani utii kwa amri ya Mungu umewasaidia kujua amri ni za kweli?

  • Shiriki mifano kutoka katika maandiko ukionyesha jinsi gani watu walibarikiwa kwa kuishi kweli za injili, kama vile (ona Danieli 6) au Nefi (ona 1 Nefi 3–4).

  • Siku chache kabla ya darasa, mwalike mmoja wa watoto kuandika kuhusu wakati ambapo alipata ushuhuda wa amri kwa kuiishi. Wakati wa darasa, muulize mtoto huyo kushiriki alichoandika.

Yohana 8:31–36

Kweli inaweza kutufanya kuwa huru.

Watoto wanapokua wakubwa, watawakuta watu wanaoamini kwamba kuishi injili ni kizuizi. Unawezaje kutumia Yohana 8:31–36 kupinga madai hayo?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kusoma Yohana 8:31–36 na kushiriki kile wanafikiria kinamaanisha kuwa mtumwa wa dhambi. Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Yesu hutusaidia kuwa huru?

  • Muombe mtoto kukusaidia kukufunga kamba, skafu, au tai kuzunguka kifundo cha mikono yako ili kuonyesha jinsi tunavyokuwa tumefungwa na dhambi wakati tukizitenda kila mara bila kutubu.

  • Onyesha kufuli ili kuwakilisha dhambi na ufunguo kuwakilisha jinsi ukweli wa Injili unaweza kutufanya kuwa huru. Kwa mfano, kujua kuhusu Upatanisho wa Mwokozi kunaweza kutupa uhuru wa kutubu na kusamehewa dhambi zetu. Au kujua kuhusu Neno la Hekima kunaweza kutupa uhuru kuepukana na mazoea mabaya.

Picha
Yesu Akifundisha Hekaluni

Yesu Alifundisha, “Kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32).

Yohana 10:1–18

Yesu ni kama mchungaji kwetu.

Unaposoma fumbo la mchungaji mwema, tafuta kweli zinazofundisha kuhusu uhusiano wetu na Mwokozi. Ni kwa jinsi gani kujua kweli hizi hubariki watoto?

Shughuli za Yakini

  • Andika mchungaji mwema na kibarua katika ubao. Eleza kwamba kibarua ni mtu anayekodiwa kufanya kazi kwa pesa. Waombe watoto kuorodhesha tofauti wanazozipata katika Yohana 10:1–18 kati ya mchungaji mwema na kibarua. Kwa nini ungehitaji kumfuata mchungaji mwema kuliko kibarua?

  • Chora au onyesha picha ya mlango. Someni pamoja Yohana 10:7–9, na waulize watoto ni kwa jinsi gani Yesu ni kama mlango. Kulingana na mstari 9, ni baraka gani zinazokuja kwa wale wanao “ingia katika” mlango? Tunawezaje kuingia katika mlango ambao Yesu Kristo Ametupatia?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kufikiria juu ya amri wanazoweza kutii kikamilifu zaidi. Waombe kujaribu kutii amri wakati wa wiki ijayo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali yaliyo na mwongozo. Uliza maswali yanayoalika watoto unaowafundisha kuenda zaidi ya kutoa taarifa ya mambo. Badala yake, wahimize kushiriki shuhuda zao za kweli za injili. Kwa mfano, kama unajadili amri, unaweza kuwauliza watoto kushiriki ni kwa jinsi gani kutii amri kumewabariki.

Picha
ukurasa wa shughuli: Yesu ananifahamu na ananipenda.

Chapisha