“Mei 27 –Juni 2 Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’’’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Mei 27 –Juni 2 Joseph Smith— Mathayo 1: Mathayo 25: Marko 12–13; Luka 21,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Mei 27–Juni 2
Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21
”Mwana wa Adamu Atakuja”
Tafakari ni kitu gani watoto unaowafundisha wanahitaji kujifunza kuhusu Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; na Luka 21. Jihisi huru kutohoa mawazo kwa watoto wakubwa katika muhtasari huu kwa watoto wadogo au kinyume chake.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Onyesha picha inayohusiana na moja kati ya hadithi katika somo la wiki hii (kama vile picha ya wanawali kumi kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia). Waombe watoto washiriki kile wanachokijua kuhusiana na hadithi hii.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Kabla Yesu hajaja tena, injili itahubiriwa duniani kote.
Yesu alisema kwamba kabla hajaja tena, injili itahubiriwa duniani kote. Watoto wanaweza kusaidia kutimiza unabii huu kwa kushiriki injili.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha ramani, tufe, au picha ya dunia (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 3) wasaidie watoto kusema, “Injili hii … Itahubiriwa duniani kote” (Joseph Smith—Mathayo 1:31). Kwa nini Mungu anataka watoto Wake wote kusikia Injili Yake?
-
Waalike watoto kutembea papo hapo mnapoimba pamoja “Ninataka kuwa Mmisionari Sasa” na “Nimeitwa Kuhudumu” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 168, 174. Waalike wamisionari wanaohudumu au wale waliorudi hivi karibuni kushiriki uzoefu wao katika kushiriki injili na kuwasaidia watoto kufikiria juu ya njia wanazoweza kushiriki injili.
Ninaweza kutumia zawadi alizonipatia Mungu.
Watoto wadogo wanatambua zawadi zao na uwezo wao. Wasaidie kuelewa kwamba zawadi hizi na uwezo huja kutoka kwa Baba wa Mbinguni.
Shughuli za Yakini
-
Leta sarafu kadhaa za kutumia unapoelezea fumbo wa talanta, lipatikanalo katika Mathayo 25:14–30. Unaweza kuwauliza watoto watatu kuwakilisha watumishi watatu. Eleza kwamba katika siku ya Yesu, talanta ilijulikana kama pesa, lakini leo talanta inaweza kumaanisha zawadi zetu na uwezo wetu.
-
Waombe watoto wataje njia wazazi wao, ndugu, walimu, au marafiki wamewasaidia wao. Watu hawa wana uwezo gani unaowasaidia kutumikia wengine?
-
Andika maneno machache ya kukumbuka kwa watoto ukimwambia kila mmoja wao kuhusu zawadi au uwezo uliouona kwao. Kunja kila karatasi yenye maneno ya kukumbuka kama zawadi na uwaalike watoto kufungua “zawadi” zao. Wahimize kuboresha zawadi zao na kuzitumia kuwatumikia wengine.
Yesu ananitaka niwatumikie wengine.
Tunamtumikia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa kuwatumikia watu wanaotuzunguka. Hata watoto wadogo wanaweza kuwatumikia wengine.
Shughuli za Yakini
-
Fanya muhtasari fumbo katika Mathayo 25:34–46. Wasaidie watoto kuelewa kwamba wakati tunapowatumikia wengine, tunamtumikia Yesu.
-
Shikilia juu picha ya mtoto katika darasa lako na picha ya Yesu iliyofichwa nyuma yake. Nini tunaweza kufanya kumtumikia mtoto huyu? Ondoa picha ya mtoto na elezea kwamba wakati tunatumikiana, tunamtumikia Yesu.
-
Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe wakiwatumikia wengine katika njia Mwokozi ameeleza katika Mathayo 25:35–36. Waombe watoto wengine kukisia nini hawa wanachora.
-
Waalike watoto kushiriki uzoefu wakati mtu alionyesha huduma kama ya Kristo kwao au familia zao.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Kabla Yesu hajaja tena, injili itahubiriwa katika ulimwengu wote.
Watoto unaowafundisha wanaweza kusaidia kuhubiri injili katika ulimwengu kabla ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kushiriki baraka walizopokea au watakazopokea kwa sababu wao ni waumini wa Kanisa la Kristo. Someni pamoja Joseph Smith—Mathayo 1:31, na uwaulize watoto jinsi injili itakavyowabariki watoto wa Mungu ulimwenguni kote.
-
Waonyeshe watoto ramani ya dunia au ya nchi yako na wasaidie kutambua baadhi ya sehemu ambapo mwanafamilia au rafiki alihubiri injili kwenye misheni.
-
Waalike watoto wachache waje wakiwa wamejiandaa kushiriki ni kwa jinsi gani wanafamilia wao au mababu zao walijulishwa injili. Kama inawezekana, muulize mtu fulani katika kata aliyehudumu misheni kushiriki uzoefu wa kushiriki injili.
-
Muulize mtoto aandike jina la mtu fulani anayeweza kumuambia kuhusu injili au kumualika kanisani. Pia, waombe watoto kuorodhesha vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa wamisionari sasa.
Ninawajibika kwa uongofu wangu binafsi kwa injili.
Fumbo la wanawali kumi hufundisha kwamba hatuwezi kuazima uongofu wetu kwa injili kutoka kwa wengine. Ni kwa jinsi gani unawasaidia watoto kuchukua jukumu la uongofu wao binafsi?
Shughuli za Yakini
-
Muombe mtoto na mmoja wa wazazi wake kuja wamejiandaa kushiriki ni kwa jinsi gani walijifunza kuhusu fumbo la wanawali kumi nyumbani wiki hii.
-
Chora taa ya mafuta katika ubao, na iandike ushuhuda. Mpe kila mtoto kipande cha karatasi kilichoundwa kama tone la mafuta, na muulize kila mtoto aandike juu yake kitu atakachofanya kuwa muongofu zaidi katika injili. Bandika vipande vyao kwenye ubao kuzunguka taa.
-
Waalike watoto kukusaidia kutengeneza orodha ya vitu vya kufanya ili kujiandaa kwa ajili ya mgeni rasmi. Ni kwa jinsi gani vitu hivi vinalingana au vinatofautiana na njia tunazoweza kujiandaa kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi?
-
Kwenye vipande vitano vya karatasi, andika vitu ambavyo haviwezi kuazimwa. Kwenye vipande vingine vitano, andika vitu vinavyoweza kuazimwa. Changanya vipande, na waombe watoto wavipange katika makundi haya mawili. Someni pamoja Mathayo 25:1–13. Kwa nini ni muhimu kutokutegemea wengine kwa ajili ya uongofu wetu wa injili?
Katika Hukumu ya Mwisho, tutampa Bwana simulizi za maisha yetu.
Baada ya ufufuo, Mungu atatuhukumu kulingana na utiifu wetu katika amri Zake na kukubali dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi. Fumbo la talanta na fumbo la kondoo na mbuzi linatufundisha kuhusu hii Hukumu ya Mwisho.
Shughuli za Yakini
-
Alika nusu ya darasa isome Mathayo 25:14–30 na nusu ingine kusoma Mathayo 25:31–46. Omba makundi yaigize mafumbo kwa darasa.
-
Waalike watoto wasome Mathayo 25:35–36 katika jozi na kutengeneza orodha ya vitu wanaweza kufanya kuonyesha upendo wao kwa Yesu Kristo.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waombe watoto kushiriki na familia zao njia wanazoweza kuwa wamisionari bora na kuongea na familia zao kuhusu watu wanaoweza kushiriki nao injili.