Njoo, Unifuate
Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18: ‘Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe’


Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18: ‘Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Karamu ya Mwisho

Na Ikawa Usiku, na Benjamin McPherson

Juni 10–16

Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18

“Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe”

Unaposoma Mathayo 26; Marko 14; Luka, 22; na Yohana 18, angalia kanuni ambazo unahisi watoto wanahitaji kuzielewa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha za matukio kwenye sura hizi, kama vile Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 54, 55, na 56, na alika watoto waseme kile kinachotendeka kwenye picha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Marko 14:22–25; Luka 22:19–20

Sakramenti hunisaidia kufikiria juu ya Yesu.

Wasaidie watoto kuelewa kwamba kupokea sakramenti ni nafasi ya kufikiria kuhusu Yesu.

Shughuli za Yakini

  • Fanya muhtasari tukio la Yesu akianzisha sakramenti. Unaweza kutumia “Sura ya 49: Sakramenti ya Kwanza,” Hadithi za Agano Jipya, 124–26, au video zinazoambatana (LDS.org). Ona pia video “Sakramenti” (LDS.org). Wasaidie watoto kuelewa kwamba tunamkumbuka Yesu wakati wa sakramenti.

  • Waulize watoto kama wanafahamu ni nini mkate na maji ya sakramenti vinawakilisha. Elezea kwamba ishara hizi zinatusaidia kukumbuka kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu na kufufuka kutoka kwa wafu. Onyesha kipande cha mkate na kikombe cha maji wakati unawasaidia watoto kukariri maneno “Katika kumkumbuka [Yeye]” (Luka 22:19).

  • Waombe watoto wafunge macho yao na kufikiria juu ya mtu wanayempenda, na kisha waalike kukusimulia kumhusu mtu huyo. Waombe kufunga macho yao tena, na kufikiria juu ya Mwokozi, na kushiriki vitu wanafahamu kumhusu Yeye. Wahimize wafikirie kumhusu Yesu wakati wa sakramenti kila wiki.

  • Waalike watoto kuonyesha nini wanaweza kufanya kumkumbuka Yesu na kuwa na staha wakati wa sakramenti.

  • Wasaidie watoto kutengeneza kijitabu kilichoelezewa kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Pendekeza kwamba wakitumie kuwasaidia kufikiria kuhusu Yesu wakati wa sakramenti.

  • Wasaidie watoto kutafuta baadhi ya magazeti ya Kanisa kwa ajili ya picha za Yesu na kuunda muunganiko wanaoweza kuuangalia wakati wa sakramenti.

Mathayo 26:36–46

Yesu aliumia kwa ajili yangu kwa sababu Ananipenda.

Fikiria jinsi unaweza kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Yesu unapojadili tukio la mateso Yake katika Gethsemane.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufikiri juu ya wakati ambapo walihisi huzuni au kuumia. Kama ni sahihi, waalike watoto wachache kushiriki. Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Elezea kwamba Yesu, katika njia ambayo hatuelewi kikamilifu, alihisi maumivu yote na huzuni ambayo kila mmoja amewahi kuhisi. Hii ina maana kwamba Anaweza kutusaidia kujisikia vizuri wakati tunapohisi huzuni, maumivu, au kuchukizwa.

  • Imba “Ninahisi Upendo wa Mwokozi Wangu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 74–75, pamoja na watoto. Waalike kushiriki njia ambazo wamehisi upendo wa Yesu.

Picha
Kristo aliomba katika Gethsemane

Kristo Anasali katika Bustani ya Gethsemane, na Hermann Clementz

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Marko 14:22–24

Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu Kristo na dhabihu Yake kwa ajili yangu.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuwa na uzoefu wa maana zaidi kwa sakramenti?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuchukua zamu kusoma mistari katika Marko 14:22–24 (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Marko 14:20–24 [katika kiambatisho cha Biblia na Mafundisho na Maagano 20:75–79. Ni maneno gani na mawazo gani yanafanana katika hivi vifungu viwili?

  • Waulize watoto wanafanya nini kuwasaidia kufikiria juu ya Yesu wakati wa sakramenti. Wasaidie kutafuta maandiko au maneno kutoka katika nyimbo za sakramenti ambayo wanaweza kusoma wakati wa sakramenti, na kisha kuorodhesha katika kadi ambayo watoto wanaweza kurejea wakati mwingine wanapopokea sakramenti. Imba nyimbo chache kati ya hizi pamoja na watoto (ona Nyimbo, na. 169–97).

  • Andika vifungu muhimu kutoka katika sala ya sakramenti katika ubao, na wasaidie watoto kukariri. Virai hivi vinamaanisha nini? Kwa nini tunashukuru kwamba tunafanya upya maagano yetu ya ubatizo kila wiki?

  • Mwalike mtu mwenye ukuhani wa Haruni kuwaambia watoto kuhusu uzoefu wake katika kuandaa, kubariki, au kupitisha Sakramenti. Ni kitu gani kilimsaidia yeye kujiandaa kufanya hivi? Anajisikiaje anapofanya hivyo? Ni kwa jinsi gani mkate na maji vinamkumbusha kuhusu Mwokozi?

  • Waombe watoto ambao wameshabatizwa kushiriki nini wanakumbuka kuhusu ubatizo wao. Walihisi vipi? Ni maagano gani waliyafanya? (Ona Mosia 18:8–10.) Waambie kwamba kila wiki wakati wanapokea sakramenti, inaweza kuwa kama kubatizwa tena—tunaweza kusamehewa dhambi zetu, na kuweka upya maagano yetu.

Mathayo 26:36–42

Katika Gethsemane, Yesu Kristo alijichukulia Yeye mwenyewe dhambi zangu na maumivu.

Kujua kuhusu kile Yesu alifanya kwa ajili yetu katika Gethsemane kunaweza kuwasaidia watoto kutubu kwa Ajili ya dhambi zao na kumrudia Mwokozi wakati wanapopitia majaribu magumu.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wasome Mathayo 26:36–42, wakiangalia maneno au virai ambayo vinaeleza jinsi Yesu alihisi katika Gethsemane. Ni nini Yesu alipitia ambacho kilimfanya kujisikia hivi? Wape watoto nafasi kushiriki hisia zao kuhusu Yesu na dhabihu Yake kwa ajili yetu.

  • Waalike watoto washiriki wakati ambapo walikuwa na huzuni au maumivu. Waulize kama wanamjua yeyote ambaye amehisi kitu kama hicho. Elezea kwamba katika Gethsemane, Yesu alihisi maumivu yote na huzuni ambayo kila mtu aliwahi kuhisi. Alifanya hivi ili Yeye aweze kutufariji sisi wakati tunahitaji (ona Alma 7:11–12).

  • Mpe mtoto fimbo ambayo ni ndefu kuliko upana wa mlango wa darasa, na muombe kuishika kimlalo na ajaribu kutembea kupita mlango. Elezea kwamba fimbo inawakilisha dhambi zetu, ambazo zinatuzuia kuingia ufalme wa Mungu. Ondoa fimbo kuonyesha kwamba Yesu alijichukulia Yeye mwenyewe dhambi zetu ili kwamba tuweze kusamehewa tunapotubu.

Luka 22:39–44

Ninaweza kufuata mfano wa Yesu kwa kuwa mtiifu kwa Baba wa Mbinguni.

Yesu alionyesha utiifu kwa Baba wakati Alisema, “Walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke” (Luka 22:4). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kujifunza kutoka mfano wa Yesu?

Shughuli za Yakini

  • Kariri pamoja na watoto kirai “Walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke” (Luka 22:42) na jadili kile inamaanisha. Nini tunachoweza kufanya ili kutii mapenzi ya Baba wa Mbinguni?

  • Wasaidie watoto kutambua baadhi ya amri walizotii. Uliza: Baraka gani ulizopokea kwa kuwa mtiifu kwa Baba wa Mbinguni, hata ilipokuwa vigumu? Waalike kushiriki uzoefu na shuhuda zao.

Luka 22:41–43

Ninaweza kupokea msaada ninaposali.

Wakati Yesu alisali katika Gethsemane, malaika alimtokea kumuimarisha. Je, watoto unaowafundisha wanaelewa kwamba wao pia wanaweza kuomba nguvu kwa Baba wa Mbinguni ?

Shughuli za Yakini

  • Simulia hadithi ya Luka 22:41–43 kwa watoto (pengine kwa kutumia “Sura ya 51: Yesu Anateseka katika Bustani ya Gethsemane,” Hadithi za Agano Jipya, 129–32, au video zinazoambata kwenye LDS.org). Elezea kwamba wakati Yesu aliomba, Baba wa Mbinguni alimtuma malaika kumuimarisha. Nani Baba wa Mbinguni anamtuma kutuimarisha?

  • Onyesha picha ya malaika akimfariji Kristo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia, na ushiriki uzoefu ambapo ulihisi kuimarishwa na Baba wa Mbinguni.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao nini watafanya wakati wa sakramenti kumkumbuka Yesu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda darasani kwako. Ushuhuda unaweza kuwa rahisi kama “Ninajua kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wenu” au “Ninahisi vizuri ndani ninapojifunza kuhusu Yesu Kristo.”

Picha
ukurasa wa shughuli: sakramenti

Chapisha