Njoo, Unifuate
Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18: ‘Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe’


“Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18: ‘Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Karamu ya Mwisho

Na Ilikuwa Usiku, na Benjamin McPherson

Juni 10–16.

Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18

“Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe”

Unaposoma matukio yaliyoelezewa katika Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; na Yohana 18, tilia maanani misukumo yoyote unayopokea, hasa ushawishi wa kufanya mabadiliko katika maisha yako.

Andika Misukumo Yako

Kulikuwa na mashahidi watatu tu wa mateso ya Kristo katika Bustani ya Gethsemane—na walilala kwa kipindi kirefu cha mateso hayo. Katika bustani ile na baadaye msalabani, Yesu alijichukulia juu Yake dhambi, maumivu, na mateso ya kila mtu aliyewahi kuishi, ingawa karibu wote waliokuwa hai kwa wakati huo hakuna hata mmoja aliyejua kilichokuwa kinatokea. Lakini wakati huo, matukio muhimu zaidi ya milele mara nyingi yalipita bila kutiliwa maanani na ulimwengu. Mungu Baba, hata hivyo, alijua. Yeye alisikia ombi la Mwanawe mwaminifu: “Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki: walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu” (Luka 22:42–43). Wakati hatukuwepo kimwili kushuhudia tendo hili la kujitolea na la unyenyekevu, katika hisia, wote tunaweza kuwa mashahidi wa Upatanisho wa Yesu Kristo. Kila tunapotubu na kupokea msamaha wa dhambi zetu na kila tunapohisi nguvu ya uimarisho ya Mwokozi, tunaweza kushuhudia juu ya kile kilichotokea katika Bustani ya Gethsemane.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 26:17–30; Marko 14:12–26; Luka 22:7–39

Sakramenti ni fursa ya kumkumbuka Mwokozi.

Je, unafanya nini ili kuwakumbuka watu ambao wamekuwa muhimu katika maisha yako? Wakati Mwokozi alipoanzisha sakramenti kwa wanafunzi Wake, Alisema, “Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Luka 22:19; ona pia 3 Nefi 18:7). Je, ni kwa jinsi gani mkate, maji, na vitu vingine vya ibada hii hukusaidia kumkumbuka Yeye na mateso Yake? Tafakari swali hili unaposoma kuhusu sakramenti ya kwanza. Pia, angalia masahihisho yanayopatikana katika Tafsiri ya Joseph Smith (ona marejeo na kiambatisho cha Biblia).

Chukua muda kutafakari uzoefu ulionao wakati wa sakramenti kila wiki. Je, unaweza kufanya nini ili kuifanya iwe na maana zaidi? Pengine unaweza kuandika mambo machache unayohisi kupata mwongozo kukumbuka kuhusu Mwokozi—mafundisho Yake, matendo Yake ya upendo, wakati ambapo ulijisikia kuwa karibu na Yeye hasa, au dhambi na maumivu Aliyojichukulia juu Yake kwa niaba yako.

Ona pia 3 Nefi 18:1–13; Mafundisho na Maagano 20:76–79; “Sakramenti,” Mada za Injili, topics.lds.org; “Daima Mkumbuke” (video, LDS.org).

Mathayo 26:36–46; Marko 14:32–42; Luka 22:40–46

Mwokozi aliteseka kwa ajili yangu katika Gethsemane.

Rais Russel M. Nelson alitualika “kuwekeza muda katika kujifunza kuhusu Mwokozi na dhabihu Yake ya kulipia dhambi” (“Kuleta Nguvu ya Yesu Kristo katika Maisha yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 40).

Fikiria wewe utafanya ili kukubali mwaliko wa Rais Nelson. Unaweza kuanza kwa kutafakari kwa maombi mateso ya Mwokozi katika Gethsemane, kama ilivyoelezewa katika mistari hii, na kuandika mawazo na maswali yanayokujia akilini.

Kwa ajili ya kujifunza kwa kina zaidi juu ya Mwokozi na Upatanisho Wake, jaribu kutafuta maandiko mengine kwa ajili ya majibu ya maswali kama haya:

Unapojifunza kuhusu kile kilichotokea Gethsemane, inaweza kuwa ya kuvutia kujua kwamba Gethsemane ilikuwa bustani ya miti ya mzeituni na ilijumuisha mtambo wa kusindika mizeituni, uliotumika kusaga mizeituni na kutoa mafuta yaliyotumika kwa ajili ya kuwashia na kwa chakula vile vile kuponya (ona Luka 10:34). Mchakato wa kutumia uzito wa juu kutenga mafuta ya mzeituni unaweza kuwakilisha uzito wa dhambi na maumivu ambao Mwokozi alibeba kwa ajili yetu (ona D. Todd Christofferson, “Kaeni katika Pendo Langu”,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 50–51).

Marko 14:27–31, 66–72; Luka 22:31–32

Uongofu ni mchakato unaoendelea.

Fikiria kuhusu uzoefu Petro alikuwa nao na Mwokozi—miujiza aliyoshuhudia na mafundisho aliyojifunza. Je, ni kwa nini sasa Mwokozi alimwambia Petro, “Nawe utakapoongoka, waimarishe ndugu zako”? (Luka 22:32; mlazo umeongezwa). Je, Mzee David A. Bednar alifundisha nini ndiyo ilikuwa tofauti kati ya kuwa na ushuhuda na kuongoka kweli? (ona “Kuongoka kwa Bwana,” Ensign au Liahona, Nov. 2012, 106–9). Unaposoma kuhusu uzoefu wa Petro katika Marko 14:27–31, 66–72, fikiria kuhusu uongofu wako wewe mwenyewe. Je, unaweza kujifunza nini kutoka kwa Petro? Unapoendelea kusoma Agano Jipya, ni ushahidi gani unaopata juu ya uongofu wa Petro na wa juhudi zake katika kuwaimarisha wengine? Je, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu kulileta matokeo gani katika uongofu wake? (ona Yohana 15:26–27; Matendo ya Mitume 1:8; 2:1–4).

ikoni ya kujifunza kwa familia

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unapoendelea kusoma kuhusu wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Mathayo 26:17–30; Marko 14:12–26; Luka 22:7–39

Je, uzoefu wa familia yako wakati wa sakramenti kila wiki ni nini? Kusoma kuhusu sakramenti ya kwanza kunaweza kuleta mwongozo wa majadiliano kuhusu umuhimu wa sakramenti na njia wanafamilia wanazoweza kufanya ili kuabudu kwao kuwe na maana zaidi. Fikiria kuonyesha picha Kupitisha Sakramenti (Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 108) na kushiriki mawazo pamoja kuhusu kile mnaweza kufanya kabla, wakati wa, na baada ya sakramenti.

Luka 10:40–46

Wakati familia yako inaposoma mistari hii, wanaweza kushiriki kile walichojifunza wakati wanaposoma maandiko yaliyopendekezwa katika sehemu ya kujifunza maandiko binafsi “Mwokozi aliteseka kwa ajili yangu katika Gethsemane.”

Luka 10:50–51

Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu kutokana na uzoefu huu?

Kristo akiponya sikio la mtumwa

Mwe Radhi Kwa Hili, na Walter Rane

Mathayo 26:36–46; Marko 14:32–42; Luka 22:40–46

Je, tunajifunza nini kutoka kwenye maneno ya Mwokozi katika mistari hii?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Jifunze maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho. Soma kile manabii na mitume wa siku za mwisho wamefundisha kuhusu kweli unazopata ndani ya maandiko. Kwa mfano, katika toleo la mkutano mkuu wa hivi karibuni la Ensign au Liahona, unaweza kutafuta kielezo cha mada cha “Upatanisho” (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21).

Kristo katika Gethsemane

Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe, na Walter Rane