Njoo, Unifuate
Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21: ‘Amefufuka’


“Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21: ‘Amefufuka’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21: ‘Amefufuka’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Yesu akiongea na Petro

Lisha Kondoo Wangu, na Kamille Corry

Juni 24–30.

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21

“Amefufuka”

Kwa maombi soma Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; na Yohana 20–21, ukikumbuka furaha uliyonayo kwa sababu ya Ufufuko wa Kristo. Tafakari jinsi unavyoweza kutoa ushuhuda wako wa tukio hili kwa wengine.

Andika Misukumo Yako

Kwa waangalizi wengi, kifo cha Yesu wa Nazareti kingeliweza kuonekana kama mwisho wa mzaha kwa maisha ya kusifika. Je, huyu siye mtu aliyemfufua Lazaro kutoka kwa wafu? Je, sisi Yeye alistahamili vitisho vya mauaji kutoka kwa Mafarisayo kila mara? Alionyesha nguvu ya kuponya upofu, ukoma, na kupooza. Hata pepo na bahari zilimtii Yeye. Na sasa alikuwa hapa, akining’inia msalabani, akitangaza, “Imekwisha” (Yohana 19:30). Yaweza kuwa kulikuweko na mshangao wa dhati katika maneno ya kejeli “Aliokoa wengine; hawezi kujiokoa mwenyewe” (Mathayo 27:42). Lakini tunajua kwamba kifo cha Yesu haikuwa mwisho wa yote. Tunajua kwamba ukimya wa kaburi ulikuwa wa muda na kwamba kazi ya Kristo ya kuokoa ilikuwa ndiyo kwanza imeanza. Leo anapatikana si “miongoni mwa wafu” bali miongoni mwa walio hai (Luka 24:5). Mafundisho Yake yasingezimwa, kwani wanafunzi wake waaminifu wangeihubiri injili kwa “mataifa yote,” wakiamini ahadi Yake kwamba atakuwa “pamoja [nao] daima, hata ukamilifu wa dahari” (Mathayo 28:19–20).

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20

Kwa sababu Yesu alifufuka, mimi pia nitafufuka.

Katika vifungu hivi, utasoma kuhusu moja ya matukio muhimu sana katika historia ya mwanadamu: Ufufuko wa Yesu Kristo. Unaposoma, jiweke katika nafasi ya watu walioshuhudia matukio yaliyozunguka Ufufuko. Je, mashahidi hawa yawezekana walijisikiaje? Je, wewe unajisikiaje unaposoma kuhusu Ufufuko wa Mwokozi? Fikiria jinsi gani ulivyokuathiri—mtazamo wako wa maisha, mahusiano yako na wengine, imani yako katika Kristo, na imani yako katika kweli zingine za injili.

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Ufufuko”; “Ufufuko,” Mada za Injili, topics.lds.org.

Luka 24:13–35

Tunaweza kumualika Mwokozi ku “kaa nasi.”

Tukio la wale wafuasi wawili waliokuwa wakisafiri ambao walikutana na Mwokozi aliyefufuka linaweza kuwa sambamba na njia yako ya ufuasi. Je, ni uhusiano gani unaouona kati ya tukio hili na uzoefu wako kama mfuasi wa Kristo? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kutembea Naye leo na kumualika “kukaa” kidogo zaidi? (Luka 24:29). Je, ni kwa jinsi gani unatambua uwepo Wake katika maisha yako? Ni kwa njia zipi Roho Mtakatifu ameshuhudia juu ya uungu wa Yesu Kristo kwako?

Luka 24:36–43; Yohana 20

Je, Yesu Kristo ana mwili?

Kupitia matukio ya Bwana aliyefufuka wakati akijitokeza kwa Mariamu Magdalena na muingiliano wake baadaye na wanafunzi Wake, tunajifunza kwamba Ufufuko wa Yesu ulikuwa halisi na wa kimwili. Na mwili Wake uliofufuka, uliotukuka, Alitembea, alizungumza, na kula na wafuasi Wake. Maandiko mengine pia hushuhudia kwamba Yesu Kristo ana mwili wa nyama na mifupa: Wafilipi 3:20–21; 3 Nefi 11:13–15; Mafundisho na Maagano 110:2–3; 130:1, 22.

Yohana 20:19–29

“Wa heri wale wasioona, wakasadiki.”

Inaweza kuwa vigumu kuamini kwamba jambo ni la kweli bila kuona ushahidi halisi. Wewe wakati mwingine unaweza kujiona kama Tomaso, ambaye alisema, “Mimi nisipoziona … Mimi sisadiki hata kidogo” (Yohana 20:25). Katika kujibu, Mwokozi alimwambia Tomaso, “Wa heri wale wasioona, wakasadiki” (Yohana 20:29). Je, ni kwa jinsi gani umebarikiwa kwa kuamini katika mambo ya kiroho ambayo hujayaona? Je, ni kitu gani kinachokusaidia wewe kuwa na imani katika Mwokozi hata wakati humuoni? Je, ni kweli zipi zingine unazoamini hata bila ushahidi halisi? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuendelea kuimarisha imani yako katika “vitu visivyoonekana, ambavyo ni vya kweli”? (Alma 32:21; ona pia Etheri 12:6). Fikiria kuandika katika shajara uzoefu huo ambao umekusaidia kuamini katika Yesu Kristo, au mwelezee mtu unayemjua.

Yohana 21:1–17

Mwokozi hunialika kuwalisha kondoo Wake.

Inaweza kuwa ya kuvutia kulinganisha mchangamano wa Mwokozi na Mitume Wake katika Yohana 21 na mara ya kwanza Alipowaamuru kuacha nyavu zao, ulioandikwa katika Luka 5:1–11. Je, ni mifanano na tofauti zipi unazipata? Je, ni umaizi gani unapata kuhusu ufuasi?

Fikiria jinsi gani maneno ya Mwokozi kwa Petro katika Yohana 21:15–17 yanaweza kutumika kwako. Je, kuna kitu kinachokurudisha nyuma kwenye kuwahudumia kondoo wa Bwana? Je, jibu lako lingeweza kuwaje kama Bwana angekuuliza “Je, wanipenda?” Tafakari jinsi unavyoweza kuonyesha upendo wako kwa Bwana.

Ona pia Jeffrey R. Holland, “Amri Kuu ya Kwanza,” Ensign au Liahona, Nov. 2012, 83–85.

ikoni ya kujifunza kwa familia

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unapomaliza kusoma Injili na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Mathayo 28:6

Kwa nini maneno “Hayuko hapa: kwani amefufuka” ni baadhi ya maneno yenye tumaini na umuhimu kuliko yote yaliyowahi kusemwa?

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21

Familia yako inaposoma sura hizi, kuwa na usikivu kwa wale watu waliojihusisha na Yesu katika kila tukio. Kwa mfano, kwa upande mmoja unaweza kuzingatia watu waliomtembelea Mwokozi kaburini. Kwa upande mwingine, unaweza kwa makini kujifunza matendo ya Mitume au wale wafuasi katika njia ya Emau.

Kristo na wafuasi wawili

Barabara ya kwenda Emau, na John McNaughton

Mathayo 28:16–20; Marko 16:14–20; Luka 24:44–53

Kama familia, jadili kazi ambayo Kristo alikuwa akiwataka Mitume Wake waifanye. Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kusaidia kutekeleza kazi hii? Je, unaweza kuelezea wakati ambapo ulihisi “Bwana akitenda kazi pamoja [nawe]” ili kukusaidia kutimiza malengo Yake? (Marko 16:20).

Yohana 21:15–17

Fikiria kusoma mistari hii wakati mkila pamoja. Hii inaweza kuongeza maana kwenye maneno ya Mwokozi “lisha kondoo wangu.” Kufuatia kile ambacho Yesu alifundisha kuhusu kondoo katika Agano Jipya (ona, kwa mfano, Mathayo 9:35–36; 10:5–6; 25:31–46; Luka 15:4–7; Yohana 10:1–16), kwa nini kulisha kondoo ni sitiari nzuri ya kuwapa lishe na kuwatunza watoto wa Mungu? Je, sitiari hii hufundisha nini kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu wanavyojisikia kuhusu sisi?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Tumia Muziki Kumwalika Roho Mtakatifu na kujifunza mafundisho. Kusikiliza au kuimba nyimbo za kanisa kama vile “Amefufuka!” au “Kristo Bwana Kafufuka Leo,” Nyimbo za kanisa, namba. 199, 200, kunaweza kumwalika Roho Mtakatifu na kukusaidia kujifunza kuhusu Ufufuko wa Mwokozi.

Yesu akimtokea Mariamu kaburini

Mwanamke, Kwa nini Unalia? Na Simon Dewey