Njoo, Unifuate
Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21: ‘Amefufuka’


“Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16: Luka 24; Yohana 20–21: ‘Amefufuka’ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Yesu akiongea na Petro

Lisha Kondoo Wangu, na Kamille Corry

Juni 24–30

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21

“Amefufuka”

Anza maandalizi yako kwa kusoma Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana20–21. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unaweza kukusaidia kuchagua kanuni katika sura hizi ambazo zitafaa kwa watoto katika darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuona picha kunaweza kuwasaidia watoto kukumbuka vitu walivyojifunza nyumbani au katika mazingira mengine. Labda unaweza kuonyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. na waombe watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu hadithi iliyoonyeshwa katika picha.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20:1–23

Nitaishi tena baada ya kufa, kama tu Yesu Alivyofanya.

Upatanisho wa Yesu Kristo, ikiwa ni pamoja na Ufufuo Wake, ni tukio muhimu zaidi katika historia, na ni msingi wa imani ya Kikristo. Unaposoma kuhusu Ufufuo, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kujenga imani yao katika Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Simulia hadithi ya Ufufuo wa Yesu Kristo kwa maneno yako mwenyewe. Waombe watoto kuchukua zamu kurudia kukusimulia hadithi. Unaweza kutumia “Sura ya 54: Yesu Amefufuka,” Hadithi za Agano Jipya, 139–44, au video zinazoambatana (LDS.org). Elezea kwamba Yesu Alipokufa, Roho Yake iliacha mwili Wake. Alipofufuka, Roho Yake na mwili Wake viliungana tena.

  • Waalike waumini wa kata kadhaa kuigiza kama askari, malaika, Mariamu Magdalena, Petro, Yohana, wanafunzi, na Tomaso na uelezee ni kitu gani walishuhudia baada ya Ufufuko wa Yesu.

  • Onyesha video “Nini kinatokea baada ya kufa kwetu?” (LDS.org), na uelezee kuhusu mtu fulani unayemjua aliyefariki. Toa ushuhuda wako kwamba kila mtu atafufuka siku moja. Waalike watoto kushiriki shuhuda zao.

  • Fikiria kuimba kwa pamoja “Je! Kweli Yesu Aliishi tena?” na “Atakapokuja tena.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64, 82. Waombe watoto wafikirie jinsi itakavyokuwa kumuona Yesu Aliyefufuka. Waache washiriki mawazo yao na darasa.

Yohana 20:24–29

Ninaweza kuwa na imani katika Yesu Kristo ijapokuwa siwezi kumuona.

Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa imani ni nini na jinsi wanavyoweza kuonyesha imani katika Mwokozi.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha Yesu Akimkaribia Tomaso (LDS.org) unaposimulia uzoefu wa Tomaso katika Yohana 20:24–29. Rudia hadithi baadae katika somo, lakini wakati huu waombe watoto kutoa baadhi ya maelezo.

  • Onyesha sanduku likiwa na kitu ndani ambacho watoto hawawezi kuona, na uelezee kitu hicho kwa watoto. Waulize kama wanaamini kitu hicho kipo kweli ndani ya sanduku na kwa nini. Kisha waonyeshe kitu hicho, na kueleza kwamba imani ni kuamini katika vitu tusivyoweza kuviona. Imani muhimu zaidi tunayoweza kuwa nayo ni imani katika Yesu Kristo.

Picha
Yesu akionyesha mikono kwa Mitume

Tazameni Mikono Yangu, na Jeff Ward

Yohana 21:15–17

Ninaweza kuonyesha upendo kwa Yesu kwa kuwatumikia wengine.

Ni kwa jinsi kwa gani unaweza kuwashawishi watoto kuwapenda na kuwasaidia wale wanaowazunguka?

Shughuli za Yakini

  • Soma Yohana 21:15–17, au Onyesha video “Lisha Kondoo Wangu” (LDS.org). Yesu hakutaka Petro kutumia muda wake wote akivua samaki. Badala yake, Alihitaji Petro ashiriki injili na kualika kila mtu kumjia Yeye. Mpe kila mtoto kondoo wa karatasi, na waombe kuiandika kitu ambacho wanaweza kufanya ili kulisha kondoo wa Yesu.

  • Waombe watoto kadhaa mapema kushiriki vitu wanavyofanya kuwapenda na kuwatumikia wengine, au njia ambazo wengine waliwatumikia wao.

  • Andika jina la kila mtoto katika darasa lako katika kipande cha karatasi kilicho katwa katika umbo la kondoo, na kusambaza kondoo hawa kote chumbani. (Jumuisha majina ya watoto wasiohudhuria kila mara.) Waalike watoto kukusanya kondoo kwa kumtafuta mmoja mwenye jina lao juu yake. Ni nini tunaweza kufanya kutumikia kondoo yeyote aliyepotea tumjuaye?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20:1–23

Kwa sababu Yesu alifufuka, watu wote watafufuliwa.

Ni kawaida kwa watoto kujiuliza kinachotokea baada ya kufa. Fikiria jinsi unavyoweza kufundisha juu ya Ufufuo kwa njia ambayo itajenga imani yao.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufumba macho yao na kufikiri kwamba wameketi kando ya kaburi la Yesu wakati unaposoma Yohana 20:1–17 au fupisha hadithi ya Ufufuo Wake (ona pia “Sura 54: Yesu Amefufuka.” Hadithi za Agano Jipya, 139–44, au video inayoambatana katika LDS.org). Ingekuwaje kumuona Mwokozi aliyefufuliwa?

  • Muombe kila mtoto kujifunza uzoefu wa mtu fulani aliyemuona Mwokozi aliyefufuka na shiriki na wana darasa wengine wote kile mtu huyo alijifunza.

  • Tazama moja au zaidi ya video hizi pamoja na watoto: “Yesu Amelazwa katika Kaburi,” “Yesu Amefufuka,” “Kristo Ametokea katika barabara ya kuelekea Emau,” na “Bwana Aliyefufuka Awatokea Mitume” (LDS.org).

Yohana 20:24–29

Ninaweza kuwa na imani katika Yesu Kristo ijapokuwa siwezi kumuona.

Watoto unawafundisha wanafanya nini ili kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo? Unawezaje kuwasaidia?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wachache wachukue zamu kusoma mistari katika Yohana 20:24–29. (Ona pia video “Wamebarikiwa Wale Wasioona, na Lakini Wameamini,” LDS.org.)

  • Andika kila neno katika kirai “Wamebarikiwa Wale Wasioona, na Lakini Wameamini” katika vipande tofauti vya karatasi. Waalike watoto wayapange maneno katika utaratibu. Waalike wao washiriki uzoefu ambao walihisi upendo wa Mwokozi hata kama hawakumuona Yeye.

  • Waalike watoto wachore picha za vitu wanavyoweza kufanya kuimarisha imani yao. Wanapochora, shiriki kile ulichofanya kuimarisha imani yako katika Yesu Kristo.

Yohana 21:1–17

Ninaweza kuonyesha upendo wangu kwa Yesu kwa kulisha kondoo Wake.

Watoto wanaweza kuwashawishi kwa kiasi kikubwa wale wanaowazunguka. Unawezaje kuwahamasisha wao kuimarisha wengine katika injili?

Shughuli za Yakini

  • Kabla ya kusoma Yohana 21:1–17 kwa pamoja, waulize watoto kama wameshawahi kuenda kuvua hapo awali. Ilikuwaje? Uliza kama kuna mmoja alishawahi kuvua “samaki wengi” (Yohana 21:6).

  • Soma Yohana 21:15–17, lakini weka majina ya watoto badala ya jina la Simioni. Kondoo wa Yesu ni kina nani? Je, tunawezaje kulisha kondoo Wake?

  • Shiriki vitafunwa rahisi na watoto. Wanapokula, waulize ni kwa namna gani kushiriki injili na mtu ni kama kuwalisha wao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kufundisha familia zao kuhusu wiki ya mwisho ya Maisha ya Mwokozi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia Mialiko ya Kutenda. Unapowaalika watoto kutenda katika kile wanachojifunza, fuatilia katika mwaliko wako wakati wa darasa lijalo. Hii inaonyesha watoto kuwa unajali kuhusu jinsi gani injili inabariki maisha yao. Wanaposhiriki uzoefu wao, wataimarishwa na watasaidiana kuishi injili.

Picha
ukurasa wa shughuli: Kila mtu atafufuliwa

Chapisha