“Julai 1–7 Matendo ya Mitume 1–5: ‘Nanyi Mtakuwa Mashahidi Wangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Julai 1–7 Matendo ya Mitume 1–5.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Julai 1–7
Matendo ya Mitume 1–5
“Nanyi Mtakuwa Mashahidi Wangu”
Anza maandalizi yako kwa kusoma Matendo ya Mitume 1–5. Kwa maombi tafuta kuelewa mahitaji ya watoto unaowafundisha . Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unaweza pia kusaidia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Andika Mimi ni Nani? ubaoni. Toa kauli kadha kuhusu Petro na waulize watoto nani kauli hizo zinamhusu. Kitu gani kingine wanachokijua kuhusu Petro?
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake kupitia manabii na mitume.
Kujifunza kuhusu jinsi Mwokozi alivyoliongoza Kanisa lake la kale kupitia Mitume kunaweza kuwasaidia watoto kupata shuhuda za manabii na mitume wa leo.
Shughuli za Yakini
-
Onyesha picha iliyojaa ukurasa mzima kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waulize watoto kwa nini wanafikiri watu wanaangalia mbinguni. Fanya muhtasari wa maelezo kutoka Matendo ya Mitume 1:1–11. (Ona pia “Sura ya 55: Mitume Wanaongoza Kanisa.” Hadithi za Agano Jipya, 145-47, au video zinazofanana (LDS.org.)
-
Wakati darasa linaangalia picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia, mwalike mtoto aonyeshe picha ya Mitume wa sasa. Nani anaongoza Kanisa wakati Kristo hayupo duniani? Ni kwa jinsi gani wanaliongoza Kanisa?
-
Cheza mchezo wa kuoanisha na seti mbili za picha za Urais wa kwanza unaoishi na Mitume Kumi na Wawili. Wakati mchezo unafanywa, shiriki jina la Mtume au Rais na kitu fulani kumhusu yeye.
-
Nyuma ya picha ya Yesu, bandika picha ndogo ndogo za vitu nabii anaweza kufundisha kuhusu, kama ubatizo au hekalu. Ruhusu kila mtoto kuchukua zamu kuangalia mojawapo ya picha na kuwaambia darasa zima, “Nabii anatufundisha kuhusu [mada kwenye picha].”
Baba wa Mbinguni anaweza kuwabariki wengine kupitia kwangu.
Unaweza kufanya nini kuwasaidia watoto kutambua njia wanazoweza kubariki wale wanaowazunguka? Wasaidie kujifunza kutoka mfano wa Petro na Yohana wakimponya mtu dhaifu.
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto kufanya matendo ambayo yanaendana na hadithi katika Matendo ya Mitume 3:1–10, kama vile kunyoosha mikono yao kwa ajili ya pesa na kuruka kwa furaha. Ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alimbariki mtu ambaye hakuweza kutembea?
-
Leta mfuko wenye picha ambazo zinaelezea njia ambazo tunaweza kuwabariki na kuwahudumia wengine. Waache watoto wachukue zamu kuchagua picha kutoka kwenye mfuko na kushiriki jinsi wanavyoweza kuwabariki wengine katika njia hiyo.
-
Waalike watoto kushiriki muda waliposaidia mtu fulani.
Naweza kuwa Mwaminifu
Wakristo wa mwanzoni walitekeleza aina ya sheria ya kuweka wakfu kusaidia kuwatunza maskini. Wale waliomiliki ardhi waliiuza na kutoa pesa kwa mitume igawanywe miongoni mwa Watakatifu kulingana na mahitaji yao. Anania na Safira hawakuwa waaminifu kuhusu mchango wao, wakifikiri wangeweza kuwadanganya watumishi wa Bwana.
Shughuli za Yakini
-
Wasaidie watoto kuigiza hadithi ya Anania na Safira. Eleza kwamba ingawa hatutakufa tutakaposema uongo, hadithi hii inaonyesha jinsi gani ilivyo muhimu kuwa mwaminifu kwa Baba wa Mbinguni.
-
Imbeni pamoja wimbo kuhusu uaminifu, kama vile “I Believe in Being Honest” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 149). Wasaidie watoto kuelewa kwamba sehemu ya kuwa mwaminifu ina maana siku zote kusema ukweli na sio kuchukuwa vitu ambavyo ni mali ya mtu mwingine.
-
Tumia vikaragosi vya mfuko wa karatasi kuigiza hali rahisi ambapo mtu anakuwa mwaminifu au sio mwaminifu. Waombe watoto kusimama kama mtu alikuwa mwaminifu au kukaa sakafuni kama mtu alikuwa sio mwaminifu.
Fundisha Mafundisho ya injili
Watoto Wakubwa
Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake kupitia manabii na mitume.
Watoto unaowafundisha wanaweza kuelewa kwamba Kanisa la Mwokozi leo linaongozwa na manabii na mitume, kama ilivyokuwa nyakati za kale.
Shughuli Yamkini
-
Andika ubaoni Jinsi gani Yesu Kristo anaongoza Kanisa wakati hayupo duniani? Waalike watoto kutafuta majibu ya swali unaposoma maneno ya Mwokozi kwa Mitume katika Matendo ya Mitume 1:8
-
Someni pamoja Matendo ya Mitume 1:22–26. Kama darasa, tambueni jinsi Mitume walivyompatia wito Mtume mpya.
-
Kabla ya wakati, muombe mtoto na mzazi wake kusoma kuhusu Mtume aliyeitwa hivi karibuni (pengine kwenye LDS.org). Mwalike mtoto kushiriki kile ambacho yeye alijifunza pamoja na darasa na, kama inawezekana, kile ambacho Mtume alisema kuhusu wito wake katika ujumbe wake kwenye mkutano wake mkuu wa kwanza.
Baba wa Mbinguni huwabariki wengine kupitia kwangu, hata kama mimi sio tajiri.
Unawezaje kuwafundisha watoto kwamba wanaweza kuwabariki wengine, hata kama hawana “fedha na dhahabu”? (Matendo ya Mitume 3:6). Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto waone fursa za kumhudumia Mungu kwa kuwahudumia wengine?
Shughuli Yamkini
-
Muombe mtoto asome Matendo ya Mitume 3:1–10 wakati watoto wengine wanaigiza hadithi nzima. (Kwa msaada, ona pia “Sura ya 56: Petro Anamponya Mtu,” Hadithi za Agano Jipya, 148–49, au video zinazoambatana katika LDS.org.) Unaweza pia kuonyesha video ”Petro na Yohana Wanamponya Mtu Mlemavu Tangu Kuzaliwa” (LDS.org). Katika njia gani baraka aliyopewa mtu huyu ilikuwa kubwa kuliko pesa alizoomba?
-
Pitisha mfuko wa sarafu. Watoto wanaposhikilia mfuko, waulize wanaweza kununua nini na hizo pesa. Kisha rudisha mfuko wa sarafu na waulize watoto baraka gani hawawezi kununua. Waalike kushiriki jinsi wanavyoweza kumhudumia mtu fulani bila kutumia pesa (Matendo ya Mitume 3:6).
Roho Mtakatifu hushuhudia kwenye moyo wangu juu ya ukweli wa injili.
Wakati watoto wanapojifunza kutambua jinsi Roho Mtakatifu huzungumza nao, watakuwa wamevutiwa kusikiliza na kutenda juu ya mwongozo wa kiungu wanaopokea.
Shughuli Yamkini
-
Someni pamoja Matendo ya Mitume 2:36–37. Unajisikiaje wakati Roho Mtakatifu anapotuambia kitu katika mioyo yetu?.
-
Kama darasa, tengeneza bango lenye maneno Tutafanya nini? juu yake. Onyesha bango kila wiki, na ongeza njia watoto wanaweza kufanya juu ya kile wanachojifunza katika kila somo la wiki.
-
Waalike watoto kutafuta vitu vizuri ambavyo watu walifanya baada ya kubatizwa katika Matendo ya Mitume 2:41–47. Je, ni vitu gani vizuri tunaweza kufanya ili kuonyesha tunashukuru kwa kipawa cha Roho Mtakatifu tulichopokea wakati tulipobatizwa?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Watie moyo watoto kupanga njia moja wanayoweza kumhudumia Baba wa Mbinguni kwa kumsaidia mwana familia wao wiki hii.