Julai 15–21. Matendo ya Mitume 10–15: ‘ Neno la Bwana Likazidi na Kuenea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
Julai 15–21. Matendo ya Mitume 10–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Julai 15–21
Matendo ya Mitume 10–15
“Neno la Bwana Likazidi na Kuenea”
Anza maandalizi yako kwa ajili ya kufundisha kwa kusoma Matendo ya Mitume 10–15 Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kukusaidia kuelewa hizi sura, na huu muhtasari unaweza kukupa mawazo ya kufundishia.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojifunza na kupata uzoefu, ungeweza kuwataka kushiriki vitu wanavyofanya ili kuonyesha kwamba wanamwamini Yesu Kristo.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Mungu wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote.
Mafundisho ya msingi ambayo hata watoto wadogo wanaweza kuelewa ni kwamba kila mmoja ni mtoto wa Mungu na kwamba Yeye anawapenda watoto wake wote.
Shughuli Yamkini
-
Onyesha picha Kristo na Watoto kutoka Ulimwenguni kote (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 116) unaposoma Matendo ya Mitume 10:34–35. Eleza kwamba wakati wa Petro baadhi ya watu waliamini kwamba Mungu aliwapenda baadhi tu ya makundi ya watu, lakini Petro alijifunza kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote, na anawataka wote kujifunza injili.
-
Waalike wanafunzi kuchora picha yao wenyewe. Shiriki ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wao na watoto Wake wote, bila kujali wanaonekana vipi au wapi wanakotoka.
-
Imba wimbo kuhusu kuwapenda wengine pamoja na watoto—kwa mfano, “Nitatembea pamoja Nawe (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 140–41 ). Waalike kushiriki njia ambazo wanaweza kuonyesha upendo kwa kila mtu—hata wale ambao ni tofauti nao—kama vile Yesu alivyofanya.
-
Waombe wazazi wa kila mtoto kabla ya muda kushiriki tabia chache nzuri za watoto wao. Shiriki majibu yao darasani, na shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anampenda kila mmoja wao.
-
Onyesha kila mtoto mmoja mmoja na sema, “Baba wa Mbinguni anampenda [jina].” Waruhusu watoto wachukue zamu kuonyeshana wao kwa wao na kusema msemo huu.
Mimi ni Mkristo kwa sababu ninamwamini na kumfuata Yesu Kristo.
Watoto unaowafundisha wanaweza kujua kwamba waumini wa Kanisa mara kwa mara huitwa Wamormoni kwa sababu tunaamini katika Kitabu cha Mormoni, lakini je, wanajua kwamba sisi pia ni Wakristo kwa sababu tunamwamini Yesu Kristo?
Shughuli Yamkini
-
Soma Matendo ya Mitume 11:26 kwa watoto. Eleza kwamba mtu anayeamini katika na kumfuata Yesu Kristo anaitwa Mkristo, kwa hiyo sisi ni Wakristo.
-
Imbeni “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77) pamoja na watoto. Je, tunapaswa kufanya vipi Kanisani, shuleni, na nyumbani kwa sababu sisi ni wafuasi wa Yesu Kristo na ni wa Kanisa Lake?
-
Waache watoto wapake rangi beji kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii na waivae nyumbani.
Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala.
Hadithi ya malaika akimfungua Petro kutoka gerezani inafundisha kwa nguvu kwamba Baba wa Mbinguni anajibu sala.
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto waigize hadithi ya Petro akiwekwa huru kutoka gerezani katika Matendo ya Mitume12:1–17 unapofanya muhtasari wa hadithi hii. Je, ni kwa jinsi gani Baba wa Mbinguni alijibu sala za wale waliokuwa wanasali kwa ajili ya Petro?
-
Imba wimbo kuhusu sala—kama vile, “Tunainamisha Vichwa Vyetu.” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 25)—na onyesha matendo ili kuwasaidia watoto kujifunza jinsi ya kusali. Waalike watoto kushiriki mifano ya vitu wanavyoweza kumshukuru Baba wa Mbinguni na kumwomba Yeye katika sala.
-
Onyesha picha za watu wakisali (ona, kwa mfano, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 111 na 112) unaposhiriki uzoefu wako wakati Baba wa Mbinguni alipojibu sala zako.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Matendo ya Mitume 10:34–35; 15:6–11
“Mungu hana upendeleo”.
Watoto unaowafundisha wanahitaji kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote, bila kujali wanaonekanaje, wanatoka wapi, au ni chaguzi gani wanafanya.
Shughuli Yamkini
-
Waulize watoto kama wanaweza kusema mtu fulani yuko hivi kwa kuwaangalia tu au kubahatisha wapi wanakotoka. Kulingana na Matendo ya Mitume 10:35, ni kwa jinsi gani Mungu anaamua kama mtu fulani “anakubalika kwake”?
-
Soma Matendo ya Mitume 10:34–35; 15:6–11. Pamoja na watoto. Eleza kwamba katika wakati wa Petro, Wayahudi waliamini kwamba Mungu hakuwakubali watu ambao hawakuwa Wayahudi (watu hawa waliitwa Wayunani). Lakini Mungu alimfundisha Petro kwamba Mungu anawapenda watoto Wake wote, Wayahudi na Wayunani. Imbeni pamoja “Mimi ni Mtoto wa Mungu,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3. Waalike wanafunzi kubadili majina ya kila mmoja wao na maneno kama mie au mimi.
-
Waalike watoto kushiriki kitu cha kipekee kuhusu mtu mwingine katika darasa. Eleza kwamba maelezo “Mungu hana upendeleo” humaanisha kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote, na kwa sababu anawapenda, Anataka Watoto Wake wote kuisikia injili.
Mkristo ni mtu anayeamini katika Yesu Kristo na kumfuata.
Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba maneno na matendo yao yanaonyesha kwamba wao ni Wakristo?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto wasome Matendo ya Mitume 11:26; 3 Nefi 27:3–8; na Mafundisho na Maagano 115:4. Andika Mkristo ubaoni na sisitiza sehemu ambayo inasema “Kristo.” Waombe watoto kuelezea wanafikiri inamaanisha nini kuwa Mkristo.
-
Waombe watoto kutaja makundi tofauti ambayo wao wamo, kama vile famila zao au darasa la msingi. Waalike kushiriki sababu za kwa nini wao wanashukuru kuwa Wakristo na kustahili kuwa katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaonyesha wengine kuwa sisi ni Wakristo?
-
Onyesha vitu kadhaa au picha ambazo zinawakilisha kweli za kipekee kwa Kanisa la Yesu Kristo, kama vile picha ya baraka ya ukuhani. Muombe mtoto achague mojawapo ya vitu au picha na aeleze jinsi ilivyo baraka katika Kanisa letu. Eleza kwamba wakati Wakristo ulimwenguni kote wako kwenye Makanisa tofauti, sisi tupo katika Kanisa lile lile ambalo Yesu Kristo alilianzisha duniani.
-
Onyesha video “True Christianity” (LDS.org). Waalike watoto kuchora vitu wanavyoweza kufanya ili kuwa Wakristo wa kweli.
Wakati ninaposali kwa imani, Baba wa Mbinguni atajibu.
Tafakari nyakati ambapo Baba wa Mbinguni amejibu sala zako. Unawezaje kutumia uzoefu huu kuwafundisha watoto kwamba Baba wa Mbinguni atasikia na kujibu sala zao katika njia yake mwenyewe na kwa muda wake?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto waigize hadithi ya malaika akimwachilia huru Petro kutoka gerezani katika Matendo ya Mitume 12:1–17 wakati unarudia hadithi katika maneno yako mwenyewe.
-
Waulize watoto wanafikiri inamaanisha nini “sala ilifanywa kwa juhudi” (Matendo ya Mitume 12:5). Je, ni kwa jinsi gani sala za watu zilijibiwa? Waalike watoto kushiriki uzoefu wao ambapo Baba wa Mbinguni alijibu sala binafsi au ya familia yao. Ungeweza pia kushiriki uzoefu wako ambao Yeye alijibu sala yako katika njia ambayo ilikuwa tofauti kutokana na kile ulichotegemea au ulichotaka. Shuhudia kwamba Mungu anatupenda, na atajibu sala zetu katika njia na mpangilio ambao ni mzuri sana kwa ajili yetu.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wape watoto picha au kitu cha kuonyesha katika nyumba zao kama kumbukumbu ya wanafamilia kusali pamoja.