Njoo, Unifuate
Julai 15–21. Matendo ya Mitume 10–15: ‘Neno la Bwana Likazidi na Kuenea’


“Julai 15–21. Matendo ya Mitume 10–15: ‘Neno la Bwana Likazidi na Kuenea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Julai 15–21. Julai 15–21,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Kornelio akizungumza na Petro

Julai 15–21

Matendo ya Mitume 10–15

“Neno la Bwana Likazidi na Kuenea”

Soma Matendo ya Mitume 10–15 kwa umakini, ukitoa muda kwa Roho kukushawishi kwa mawazo na hisia. Je, kuna nini cha kujifunza wewe katika sura hizi?

Andika Misukumo Yako

Wakati wa huduma Yake ya duniani, mafundisho ya Yesu Kristo mara nyingi yalitoa changamoto kwa tamaduni na imani za watu walizozishikilia kwa muda mrefu; hii haikwisha baada ya kupaa Kwake mbinguni—hata hivyo, Yeye aliendelea kuliongoza Kanisa Lake kwa ufunuo. Kwa mfano, wakati wa uhai wa Yesu Kristo wanafunzi Wake waliihubiri injili kwa Wayahudi wenzao tu. Lakini punde baada ya Mwokozi kufa na Petro kuwa nabii wa Kanisa, Yesu Kristo alimfunulia Petro kwamba muda ulikuwa umefika kwa injili kuhubiriwa kwa wasio Wayahudi. Wazo la kushiriki injili na Wayunani halionekani la kushangaza leo, hivyo, ni somo gani sisi tunajifunza katika hadithi hii? Pengine somo moja ni kwamba mabadiliko ya sera na utendaji—katika Kanisa la zamani na la sasa—huja kwa ufunuo kutoka kwa Bwana kwenda kwa viongozi Wake aliowachagua (Amosi 3:7; M&M 1:38). Muendelezo wa ufunuo ni sifa muhimu ya Kanisa la kweli na lililo hai la Yesu Kristo. Kama Petro, ni lazima tuwe radhi kukubali muendelezo wa ufunuo na kuishi “kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” (Luka 4:4), ikijumuisha “yale yote [Mungu] ameyafunua, na ambayo sasa anayafunua” na ‘mambo mengi makuu na muhimu’ Atakayofunua “yahusuyo ufalme wa Mungu” (Makala ya Imani 1:9).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Matendo ya Mitume 10

“Mungu hana upendeleo.”

Kwa vizazi kadhaa, Wayahudi walikuwa wameamini kwamba kuwa wa “uzao wa Ibrahimu,” au warithi halisi wa Ibrahimu, ilimaanisha kwamba mtu alikuwa amekubaliwa (ameteuliwa) na Mungu (ona Luka 3:8). Mtu mwingine yeyote alichukuliwa kama Myunani “mchafu” ambaye hakukubaliwa na Mungu. Katika Matendo ya Mitume 10, Bwana alimfundisha nini Petro kuhusu nani “anakubaliwa na Yeye”? (Matendo ya Mitume 10:35). Ni ushahidi gani unapata katika sura hii kwamba Kornelio aliishi maisha ya haki ambayo yalikubalika kwa Bwana? Kwa nini ni muhimu kujua kwamba “Mungu hana upendeleo” (mstari wa 34), ikimaanisha kwamba watu wote wanaweza kupokea baraka ya injili kama wakiishi injili? (ona 1 Nefi 17:35).

Kama Wayahudi walivyowadharau wale ambao hawakuwa wa ukoo wa Ibrahimu, je, umewahi kujikuta ukiwaza mawazo yasiyo mema au yasiyo ya kweli kuhusu mtu ambaye yuko tofauti na wewe? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kushinda mazoea haya? Inaweza kuwa ya kuvutia kujaribu shughuli rahisi kwa siku chache zijazo: Wakati wowote unapojumuika na mtu, jaribu kufikiria mwenyewe, “Mtu huyu ni mtoto wa Mungu.” Unapofanya hivi, ni mabadiliko yapi unagundua katika jinsi ya kuwafikiria na kujumuika na wengine?

Ona pia D. Todd Christofferson, “Kaeni katika Pendo Langu,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 48–51; 1 Samuel 16:7; “Ufunuo wa Petro Kupeleka Injili kwa Wayunani” (filamu, LDS.org).

Matendo ya Mitume 10; 11:1–1815

Baba wa Mbinguni hunifundisha mstari juu ya mstari kwa njia ya ufunuo.

Wakati Petro alipoona ono lililoelezwa katika Matendo ya Mitume 10, mwanzo alihangaika kulielewa na “aliona shaka ndani ya nafsi yake [ono] lilimaanisha nini” (mstari wa 17). Lakini bado Bwana alimpa Petro uelewa mkubwa pale Petro alipoutafuta. Unaposoma Matendo ya Mitume 10, 11, na 15, gundua ni kwa jinsi gani uelewa wa Petro juu ya ono lake uliongezeka baada ya muda. Ni kwa jinsi gani umetafuta na kupata uelewa mkubwa kutoka kwa Mungu ulipokuwa na maswali?

Matendo ya Mitume 10, 11, na 15 husimulia nyakati ambazo Bwana aliwaongoza watumishi Wake kupitia ufunuo. Inaweza kusaidia kuandika kile unachopata kuhusiana na ufunuo unaposoma sura hizi. Je, ni kwa jinsi gani Roho huongea nawe?

Ona pia “Ufunuo,” Mada za Injili, topics.lds.org; Ronald A. Rasband, “Acha Roho Mtakatifu Aongoze,” Ensign au Liahona, Mei 2017, 93–96; “Mkutano wa Yerusalemu” (filamu, LDS.org).

Matendo ya Mitume 11:26

Mimi ni Mkristo kwa sababu ninamwamini na kumfuata Yesu Kristo.

Ni nini cha kipekee kuhusu mtu anayeitwa Mkristo? (ona Matendo ya Mitume 11:26). Inamaanisha nini kwako kujulikana kama Mkristo au kujichukulia juu yako jina la Yesu Kristo? (ona M&M 20:77). Fikiria umuhimu wa majina. Kwa mfano, jina la familia yako linamaanisha nini kwako? Kwa nini jina la Kanisa leo ni muhimu? (ona M&M 115:4).

Ona pia Mosia 5:7–15; Alma 46:13–15; 3 Nefi 27:3–8; M. Russell Ballard, “Umuhimu wa Jina,” Ensign au Liahona, Nov. 2011, 79–82.

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Matendo ya Mitume 10:17, 20

Je, tumewahi kupata uzoefu wa kiroho na baadaye kutia shaka kile tulichojisikia au kujifunza? Ni ushauri gani tunaweza kutoa ambao unaweza kutusaidia kushinda shaka zetu? (Ona Ronald A. Rasband, “Ili Usisahau,” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 113–15.)

Matendo ya Mitume 12:1–17

Wakati Petro alipotupwa gerezani, waumini wa Kanisa walikusanyika pamoja na kuomba kwa ajili yake. Je, kuna mtu yeyote familia yako anahisi kushawishiwa kumuombea, kama vile kiongozi wa Kanisa au mpendwa wenu? Inamaanisha nini “kuomba kwa juhudi”? (Matendo ya Mitume 12:5).

Picha
Petro anaokolewa kutoka gerezani

Petro anaokolewa kutoka gerezani, na A. L. Noakes

Matendo ya Mitume 14

Mnaposoma sura hii pamoja, baadhi ya wanafamilia wanaweza kuandika baraka walizopata wafuasi na Kanisa, wakati huo wanafamilia wengine wanaweza kuona upinzani au majaribu waliyopata wafuasi. Kwa nini Mungu huruhusu mambo magumu kuwapata wenye haki?

Matendo ya Mitume 15:1–21

Mistari hii huelezea kutokuelewana ndani ya Kanisa kuhusiana na kama waongofu wa kiyunani (watu wasio Wayahudi) wanapaswa kutahiriwa kama ishara ya agano lao. Kutokuelewana kulisuluhishwa baada ya Mitume kukutana pamoja kufikiria mada hiyo na kisha kupokea jibu lenye mwongozo wa kiungu. Huu unaweza kuwa wakati mzuri kufundisha familia yako kwamba mpangilio huo ndio utumikao leo. Kama familia, chagueni swali kuhusu injili ambalo mnataka kulitafutia jibu pamoja. Tafuteni pamoja utambuzi katika maandiko na katika mafundisho ya manabii na mitume wa siku hizi. ( Mwongozo wa Mada na kielezo cha mada ndani ya majarida ya Kanisa ya toleo la mkutano mkuu vinaweza kusaidia.)

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Chora picha. Picha zinaweza kuwasaidia wanafamilia kupata taswira ya mafundisho na hadithi. Mnaweza kusoma mistari michache, na kisha toa muda kwa wanafamilia kuchora kitu kinachohusiana na kile mlichosoma. Kwa mfano, wanafamilia wanaweza kufurahia kuchora picha za ono la Petro katika Matendo ya Mitume 10.

Picha
Kornelio na Petro

Ono la kimiujiza la akida Kornelio na safari ya kukutana na Petro huonyesha kwamba “Mungu hana upendeleo” (Matendo ya Mitume 10:34).

Chapisha