“Julai 8–14. Matendo ya Mitume 6–9: ‘Ungependa Mimi Nifanye Nini?’“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Julai 8–14. Matendo ya Mitume 6–9.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Julai 8–14
Matendo ya Mitume 6–9
“Ungependa Mimi Nifanye Nini?”
Anza kwa kusoma Matendo ya Mitume 6–9. Muhtasari wa wiki hii kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaweza kukusaidia kuelewa sura hizi. Shughuli kwa watoto wadogo katika muhtasari huu zinaweza kutoholewa kwa ajili ya watoto wakubwa, na kinyume chake.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Andika baadhi ya majina ya watu kutoka Matendo ya Mitume 6–9 ubaoni—pengine Sauli au Stefano. Waalike watoto kushiriki chochote wanachokijua kuhusu mmojawapo wa watu hawa.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Ninaweza kumfuata Yesu Kristo kwa kusimamia haki.
Watoto wanaweza kujifunza nini kutoka kwa Stefano kuhusu kuwa mfuasi wa Yesu Kristo?
Shughuli Yamkini
-
Wasaidie watoto kufanya matendo yanayoendana na wimbo kuhusu kuchagua yaliyo mema, kama vile “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159). Tumia Matendo ya Mitume 7:51–60 kuwaeleza watoto jinsi Stefano alivyofundisha kuhusu Yesu Kristo, ingawa kwa kufanya hivyo kuliwafanya viongozi wa Kiyahudi wakasirike sana (ona pia “Sura ya 57: Watu Waovu Wanamuua Stefano,” Hadithi za Agano Jipya, 150-51, au video inayofanana kwenye LDS.org). Je, ni kwa jinsi gani Stefano alisimama kwa ajili ya haki?
-
Wape watoto matukio kadhaa ya watoto ambao wanatakiwa kufanya uchaguzi kati ya jema na ovu. Uliza watoto je wangelifanya nini ili kusimama kwa ajili ya haki.
Roho Mtakatifu ananipa mwongozo wa kiungu wa kuhubiri injili kwa wengine.
Filipo alifuata ushawishi wa Roho na kumsaidia Muethiopia ambaye alikuwa akijitahidi sana kuelewa maandiko. Ni masomo gani katika hadithi hii yana msisimko kwa watoto unaowafundisha?
Shughuli Yamkini
-
Weka viti viwili pamoja kuumba kibandawazi. Waalike watoto wawili kukaa katika kibandawazi, mmoja kumwakilisha Filipo na mwingine mtu wa Ethiopia. Kisha eleza hadithi ya jinsi Filipo alivyofundisha injili kwa mtu kutoka Ethiopia.
-
Umewahi wakati wowote kumhisi Roho Mtakatifu akikuambia uhubiri injili kwa mtu fulani, kunakofanana na tukio la Filipo alilolipata katika Matendo ya Mitume 8:29? Shiriki uzoefu wako pamoja na watoto.
Ninapofanya makosa, Baba wa Mbinguni ananialika nitubu na nibadilike.
Wakati Yesu alipomwambia Sauli kuacha kutesa Kanisa la Bwana, Sauli mara moja alitubu na kubadilika. Ni kwa jinsi gani maelezo haya yanaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutamani kubadilika kwa haraka wakati wanapofanya kosa?
Shughuli Yamkini
-
Fanya muhtasari wa kuongoka kwa Sauli katika Matendo ya Mitume 9:1–20 (ona pia ”Sura ya 59: Sauli anajifunza kuhusuYesu.” Hadithi za Agano Jipya, 154-55. au video inayofanana katika LDS.org).
-
Orodhesha au lete picha za vitu ambavyo vinabadilika, kama vile kiluwiluwi, ambacho kinabadilika kuwa chura, au miti wakati wa misimu tofauti. Ni kwa jinsi gani Sauli alibadilika wakati Yesu Kristo alipomtembelea?
-
Chora barabara yenye njia panda ubaoni. Waalike watoto kutaja sehemu wangependa kutembelea na ziandike juu ya barabara moja. Je, nini kingetokea kama tungeshika barabara isiyo sahihi? Je, ni kwa jinsi gani toba ni kama kurudi kwenye barabara sahihi?
-
Waombe watoto kurudia kile Sauli alichosema kwa Bwana: “Ungependa mimi nifanye nini?” Je, Bwana anatutaka sisi tufanye nini?
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Nitakuwa shahidi wa Yesu Kristo.
Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kujifunza kutokana na mfano wa Stefano wa kusimama kama shahidi wa Yesu Kristo?
Shughuli Yamkini
-
Soma Matendo ya Mitume 6:5–15 na 7:51–60 pamoja na watoto. Je, ni kwa jinsi gani Stefano alikuwa shahidi wa Yesu Kristo? Alika mmoja au watoto zaidi wajifanye kuwa Stefano na kushiriki kile wanachoamini na kwa nini.
-
Waalike watoto kuchukua zamu kusoma Matendo ya Mitume 6:3–10, wakitafuta sifa Stefano alizokuwa nazo ambazo zilimsaidia kuhudumu.
-
Waombe watoto kukusaidia kufikiria juu ya hali ambazo wanaweza kusimama kama mashahidi wa Yesu Kristo na injili Yake. Wasaidie kuigiza baadhi ya hali hizi. Waombe watoto kusoma Mosia 18:9. Toa angalizo kwamba kuwa shahidi wa Yesu Kristo ni pamoja na ahadi tunazofanya wakati wa ubatizo.
-
Andika majina Stefano na Filipo ubaoni. Chini ya jina la Stefano, andika njia tunazoweza kuwa mifano kwa wengine. Chini ya jina la Filipo, andika njia tunazoweza kushiriki injili pamoja na wengine. Ni kwa jinsi gani kuwa mfano wa mfuasi wa Yesu Kristo kunatusaidia kushiriki injili?
Ukuhani ni zawadi ya thamani kuu kutoka kwa Mungu.
Shetani anajenga ujumbe kwamba vitu vya dunia vinatuletea furaha. Unawezaje kutumia hadithi ya Simoni kuwasaidia watoto kuthamini vitu vya kiroho kama vile ukuhani na baraka zake?
Shughuli Yamkini
-
Fanya muhtasari wa hadithi ya Simoni, inayopatikana katika Matendo ya Mitume 8:5-24 (ona pia ”Sura 58: Simoni na Ukuhani.” Hadithi za Agano Jipya, 152-53. au video inayofanana katika LDS.org). Kwa nini hatuwezi kuupokea ukuhani kwa kuununua? Ni kwa jinsi gani kwa kweli mtu hupokea ukuhani? (Ona Makala ya Imani 1:5).
-
Wape watoto mfano wa pesa, na onyesha picha za vitu ambavyo vinaweza kununuliwa kwa pesa. Waulize watoto kiasi gani cha mfano wao wa pesa watatoa kwa ajili ya vitu hivi. Kisha onyesha picha za sakramenti, hekalu (ikiwakilisha baraka za hekalu), ubatizo, na baraka zingine tunazopokea kupitia ukuhani. Eleza kwamba vipawa hivi kutoka kwa Mungu ni vyathamani kuu na haviwezi kununuliwa na pesa.
Ninapofanya makosa, Baba wa Mbinguni ananialika nitubu na nibadilike.
Wakati Yesu alipomwambia Sauli kuacha kutesa Kanisa la Bwana, Sauli mara moja alitubu na kubadilika. Ni kwa jinsi gani maelezo haya yanaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutamani kubadilika kwa haraka wakati wanapofanya kosa?
Shughuli Yamkini
-
Waalike wanafunzi kukunja kipande cha karatasi kiwe nusu. Waombe waandike Kabla kwenye nusu moja na Baada kwenye nusu nyingine. Soma pamoja na watoto Matendo ya Mitume 8:1–3; 9:1–2; na 9:17–22, kutafuta maneno au virai ambayo vinamwelezea Sauli kabla na baada ya kumwona Bwana.
-
Mwalike mshiriki wa kata kushiriki na watoto hadithi yake ya kuongoka na jinsi gani kuwa muumini wa Kanisa kumebadilisha maisha yake, kama maisha ya Sauli yalivyobadilika.
-
Chora “barabara kwenda Dameski ubaoni. Waalike watoto kusoma Matendo ya Mitume 9:6, 11, 18, 20–22, wakitafuta kile Sauli alichofanya ili kutubu na kumgeukia Kristo, na andika vitendo hivi kwa kuambaa na barabara. Tunajifunza nini kutoka kwa Sauli kuhusu jinsi tunavyoweza kuwa zaidi kama Kristo?
-
Waalike watoto kuchora sehemu waliyoipenda ya maelezo ya kuongoka kwa Sauli na kushiriki mchoro wao pamoja na washiriki wa darasa.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Watie moyo watoto waeleze familia zao shughuli waliyoipenda kutoka darasani leo na iliwafundisha nini wao.