Njoo, Unifuate
Juni 17–23. Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19: ‘Imekwisha’


“Juni 17–23. Mathayo 27; Marko 15: Luka 23; Yohana 19: ‘Imekwesha’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 17–23. Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Kristo mbele ya Pilato

Ecce Homo, na Antonio Ciseri

Juni 17–23

Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19

“Imekwisha”

Anza maandalizi yako kwa kusoma Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19. Kwa maombi tafuta kuelewa mahitaji ya watoto.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Mwache kila mtoto ashike picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia. Wakati wakishikilia picha, kila mtoto anaweza kushiriki kitu anachojua kuhusu jinsi Yesu alikufa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 27:11–66; Luka 23; Yohana 19

Kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yangu, naweza kufufuka.

Watoto wadogo wanaweza kuchukizwa na matukio ya kusulubiwa kwa Yesu. “Sura 52: Majaribu ya Yesu” na “Sura 53: Yesu Anasulubiwa,” Hadithi za Agano Jipya, 133–38, au video zinazoambatana (LDS.org) zinatoa mfano mzuri kwa jinsi gani ungeweza kushiriki kiusahihi hadithi hii nao.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia unaposimulia kuhusu shitaka la Yesu, Kusulubiwa, na mazishi (ona pia Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba. 57 na 58). Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusiana na matukio haya. Sisitiza kwamba katika siku ya tatu, Yesu alifufuka, ikimaanisha alirudi tena uzimani.

  • Waombe watoto kutaja baadhi ya vitu wazazi wao huwafanyia ambavyo hawawezi kujifanyia wao wenyewe. Onyesha picha ya Mwokozi. Eleza kwamba kwa sababu ya Yesu, tunaweza kufufuka—kitu ambacho hatuwezi kujifanyia sisi binafsi.

  • Onyesha picha ya mtu fulani unayemjua aliyefariki. Shiriki ushuhuda wako kwamba kwa sababu ya Yesu huyo mtu ataishi tena.

Picha
mazishi ya Kristo

Mazishi, na Carl Heinrich Bloch

Mathayo 27:26-37; Luka 23:34

Ninaweza kuwasamehe wengine kama Yesu alivyofanya.

Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa jinsi ya kuwasamehe wale wasio wakarimu, kama Yesu Alivyofanya?

Shughuli za Yakini

  • Elezea ni kwa jinsi gani askari hawakuwa na huruma kwa Yesu (ona Mathayo 27:26–37), na kisha soma Luka 23:34. Elezea kwamba tunapowasamehe wengine, tunaachana na hisia mbaya dhidi yao na kuonyesha upendo.

  • Shiriki matukio ambayo mtu anasema au anafanya kitu kibaya. Waalike watoto kuonyesha ni kwa jinsi gani wangeweza kumsamehe mtu huyo.

  • Andika maneno au virai kutoka “Nisaidie, Baba , yangu.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 99, katika ubao. Waalike watoto kuimba wimbo huu mara kadhaa, wakifuta baadhi ya maneno kila mara hadi watakapojifunza wimbo wote. Kulingana na wimbo huu, ni nani tunapaswa kumsamehe? Ni nani anaweza kutusadia wakati kusamehe ni vigumu?

  • Pekua toleo la hivi karibuni la Friend au Liahona ili kutafuta hadithi kuhusu mtoto aliyemsamehe mtu fulani. Shiriki hadithi hii na watoto.

Luka 23:32–33, 39-43

Kwa sababu Yesu aliteseka na alikufa kwa ajili yangu, Ninaweza kutubu na kusamehewa.

Ingawa watoto chini ya umri wa miaka nane bado hawawajibiki, ni muhimu kwao kuanza kujifunza jinsi ya kutubu dhidi ya chaguzi zisizofaa wanazofanya.

Shughuli za Yakini

  • Fanya muhtasari Luka 23:32–33, 39–43, na uonyeshe wezi wawili katika picha 57 katika Kitabu cha Sanaa za Injili. Eleza kwamba wakati mwizi wa kwanza akimkejeli Yesu, mwizi wa pili alikiri kwamba amefanya kitu kibaya—alikuwa anaanza kutubu.

  • Wasomee Mafundisho na Maagano 19:16 watoto. Kwa nini Yesu Aliteseka kwa ajili yetu?

  • Onyesha video “Baiskeli inayong’aa” (LDS.org). Elezea kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu wanaweza kutusaidia kuepukana na dhambi zetu na makosa na kupokea msamaha.

  • Waache watoto waweke alama za chaki katika ubao kuwakilisha chaguzi mbaya. Kisha waombe wafute ubao kuwakilisha toba. Onyesha picha ya Mwokozi, na shuhudia kwamba tunaweza kutubu kwa sababu Yake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 27:11–66; Luka 23; Yohana 19

Yesu alikufa kwa ajili yangu kwa sababu Ananipenda.

Kwa nini unashukuru kwamba Yesu Kristo Alikufa kwa ajili yako? Fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa dhabihu ya Mwokozi kwao.

Shughuli za Yakini

  • Orodhesha matukio muhimu kutoka Mathayo 27:11–66 (kwa msaada katika kufanya hili, ona “Sura 52: Majaribu ya Yesu” na “Sura 53: Yesu Kasulubiwa.” Hadithi za Agano Jipya, 133–38). Waalike watoto kusoma mistari hii na kuweka matukio katika utaratibu sahihi.

  • Onyesha video “Yesu anahukumiwa mbele ya Pilato” na “Yesu Anapigwa na Kusulubiwa” (LDS.org). (Ona pia “Upatanisho,” LDS.org.) Kwa nini Yesu Alikuwa tayari kuteseka kwa ajili yetu?

  • Muombe mtoto asome Mathayo 27:54, na waalike watoto kushiriki vitu kuhusu Yesu vinavyowasaidia kufahamu kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu.

  • Waulize watoto kile wanachojifunza juu ya kusulibiwa kutoka “Tazama Mwokozi Mkuu Amekufa” Nyimbo, na. 191, au nyimbo nyingine ya sakramenti.

Mathayo 27:26-37; Luka 23:34

Ninaweza kuwasamehe wengine kama Yesu alivyofanya.

Inaweza kuwa vigumu kuwasamehe wengine. Watoto unaowafundisha watabarikiwa wanapofuata mfano wa Mwokozi na kusamehe kila mtu.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuchukua zamu kusoma kuhusu askari wakiwa hawana huruma kwa Yesu katika Mathayo 27:26–37 na Yesu akiwasamehe katika Luka 23:34. (Tazama umaizi unaotolewa na Tafsiri ya Joseph Smith katika Luka 23:34, tanbihi c.) Tunajifunza nini kutoka katika mfano wa Yesu?

  • Andika katika ubao Je, unaweza kufanya nini kumsamehe mtu asiye na huruma kwako? Waache watoto wachukue zamu kuandika mawazo katika ubao, kama vile Sali kuwa na hisia zenye upendo kwa mtu huyo au Fikiria kitu fulani kizuri kuhusiana na mtu.

  • Waalike watoto kuchora picha za hali ambazo mtu hajawa mkarimu na jinsi ya kumsamehe mtu huyo. Waache washiriki michoro yao na darasa.

Luka 23:32–33, 39-43

Kwa sababu Yesu aliteseka na alikufa kwa ajili yangu, Ninaweza kutubu na kusamehewa.

Somo hili ni wakati mzuri wa kushuhudia kwamba kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza kutubu dhambi zetu na kusamehewa.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike mtoto asome Luka 23:32–33, 39-43. Elezea kwamba watu wawili waliosulubiwa na Yesu walikuwa wezi. Mmoja wa wezi alionyeshaje kwamba alikuwa anaanza kutubu?

  • Maneno: “Ninaweza samehewa wakati ninatubu kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo.” Wapatie watoto vidokezo vya kuwasaidia kujaza mapengo.

  • Mwalike mtoto kushikilia mfuko, na kuujaza kwa mawe madogo wakati watoto wengine wanataja chaguzi zisizofaa mtu anaweza kufanya. Wasaidie watoto kulinganisha mfuko na mzigo wa kiroho tunaobeba pale tutendapo dhambi. Ni kwa jinsi gani toba ni kama kuchukua miamba kutoka kwenye mfuko?

  • Tumia makala “Unaweza kutubu na Kusamehe” (Friend, Aug. 2015, 10) kufundisha watoto jinsi ya kutubu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kufikiria mtu wanayehitaji kumsamehe na kuamua juu ya jambo moja watakalofanya ili kumuonyesha mtu huyo kwamba wamemsamehe.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jifunze kutambua ufunuo. Ufunuo mara nyingi huja “mstari juu ya mstari” (2 Nefi 28:30), wala sio yote kwa wakati mmoja. Unapoomba na kutafakari maandiko na muhtasari huu, utapata mawazo na misukumo inaweza kuja wakati wowote na popote—unaposafiri kwenda kazini, unapofanya kazi za nyumbani, au unapokuwa pamoja na familia na marafiki.

Picha
ukurasa wa shughuli: Nitafufuliwa

Chapisha