Njoo, Unifuate
Juni 3–9 Yohana 13–17: ‘Kaeni katika Pendo Langu’


“Juni 3–9. Yohana 13–17: ‘Kaeni katika Pendo Langu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 3–9. Yohana 13–17,“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Karamu ya Mwisho

Kwa Ukumbusho Wangu, by Walter Rane

Juni 3–9

Yohana 13–17

“Kaeni katika Pendo Langu”

Sali ili kujua mahitaji ya watoto unaowafundisha unaposoma Yohana 13–17. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unaweza kukusaidia kuelewa mafundisho na kukupa mawazo ya kufundishia watoto katika darasa lako.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia watoto kushiriki kile wanajifunza nyumbani, pitisha moyo wa karatasi na alika kila mtoto kushiriki kitu ambacho yeye ufanya kuonyesha upendo kwa wengine wakati ni zamu yake kushika moyo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Yohana 13:1–17

Yesu ananitaka niwatumikie wengine.

Hadithi ya Yesu akiosha miguu ya Mitume Wake ni mfano wa huduma ya unyenyekevu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto kufuata mfano wa Yesu?

Shughuli za Yakini

  • Tumia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia kusaidia kueleza hadithi katika Yohana 13:1–17. Waalike watoto kuonyesha utondoti kutoka kwenye hadithi ambao hupo kwenye picha.

  • Onyesha picha za Yesu akiwatumikia wengine (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili au magazeti ya Kanisa kwa mawazo). Acha watoto wachukue zamu kushikilia picha unapowasimulia hadithi zilizooneshwa (waache wasaidie kusimulia hadithi kama wanaweza).

  • Waulize watoto jinsi wanahisi wakati mtu anawasaidia. Waache watoto wachore picha za jinsi wanavyoweza kufuata mfano wa Yesu kwa kuwatumikia wengine.

Yohana 13:34–35; 14:15

Ninaonyesha upendo wangu kwa Yesu kwa kushika amri Zake.

Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba utiifu wao ni ishara kwamba wanampenda Yesu Kristo?

Shughuli za Yakini

  • Mpe kila mtoto moyo wa karatasi ili aupambe. Waalike wainue juu mioyo yao kila wakati wanapoimba neno “upendo” katika “Yesu Alisema Mpenda Kila Mtu” na “Pendaneni,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 61, 136.

  • Wasaidie watoto kukariri Yohana 14:15 kwa kushikilia juu mioyo yao ya karatasi wanaposema, “kama unanipenda,” na picha ya vidonge vya jiwe wanaposema, “Shika amri zangu.”

  • Waalike watoto kuchukua zamu wakiigiza aina ya kitendo wangefanya kwa mtu fulani kuonyesha upendo wao kwa Yesu. Acha watoto wengine kukisia kile wanachokifanya.

  • Malizia ukurasa wa shughuli ya wiki hii pamoja na watoto.

Yohana 2:26–27; 15:26; 16:13–14

Roho Mtakatifu hunisaidia kujihisi nipo karibu na Yesu.

Ingawa watoto unaowafundisha bado hawajapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, wanaweza kujifunza sasa jinsi nguvu ya Roho Mtakatifu hufanya kazi katika maisha yao.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha Karamu ya Mwisho (Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 54). Waeleze watoto kwamba katika Karamu ya Mwisho, Yesu Aliwafundisha Wanafunzi Wake kuhusu Roho Mtakatifu.

  • Waalike watoto waweke mikono yao katika mioyo yao na kwenye vichwa vyao. Fungua maandiko kwenye Mafundisho na Maagano 8:2, na uelezee kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuongea nasi “katika akili [zetu] na mioyo [yetu],” au kupitia mawazo yetu na hisia.

  • Zima taa na ushikilie picha juu. Kisha mlika picha kwa tochi. Waulize watoto ni kwa jinsi gani tochi ni kama Roho Mtakatifu.

  • Pamoja na watoto, imbeni “Roho Mtakatifu.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 105, kwa “sauti nyororo ya utulivu.” Waalike wao wasikilize vitu ambavyo Roho Mtakatifu anafanya.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Yohana 13:34–35; 14:15; 15:10–14

Ninaonyesha upendo wangu kwa Yesu kwa kushika amri Zake.

Unaposoma vifungu hivi katika kujifunza binafsi, fikiria kuhusu watoto unaowafundisha. Watabarikiwaje wanapoelewa kwamba utiifu wao ni ishara ya upendo wao kwa Mwokozi?

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kukariri Yohana 13:34–35. Njia moja ya kufanya hivi ni kuimba “Pendaneni.” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37, na wasaidie watoto kujifunza matendo ya kuendana nao.

  • Waalike watoto kuandika katika ubao njia Yesu Ameonyesha Anatupenda sisi. Unaweza kuonyesha picha kutoka katika maisha ya Mwokozi kuwasaidia (kwa mawazo, ona Kitabu cha Sanaa za Injili). Tunawezaje kuonyesha upendo kwa wengine kama Alivyofanya? Mwalike kila mtoto kusimama na kushiriki njia moja “atapendana” (Yohana 13:34).

  • Mwalike mtoto asome Yohana 14:15. Acha watoto wachukue zamu kuchora picha zinazomwakilisha mtu akishika amri, wakati watoto wengine wote wakikisia kile mtoto huyu anachora. Kwa mifano ya maagano, ona Kwa Nguvu ya Vijana. Ni kwa jinsi gani kushika amri hizi humwonyesha Mwokozi kwamba tunampenda Yeye?

Yohana 14:26; 15:26; 16:13

Roho Mtakatifu huongoza, hufariji, na kushuhudia ukweli.

Sasa kwamba wengi wa watoto wamepokea kipawa cha Roho Mtakatifu, tunawezaje kuwasaidia kuelewa vyema kazi za Roho Mtakatifu?

Shughuli za Yakini

  • Wapatie watoto mistari ifuatayo wasome katika jozi: Yohana 14:26; 15:26; na 16:13. Waombe watoto watafute maneno ambayo yanawafundisha kile Roho Mtakatifu hufanya. Andika maneno hayo ubaoni.

  • Shiriki uzoefu wakati Roho Mtakatifu alikuongoza, alikufariji, alikuonya, au kukushuhudia ukweli. Waalike watoto kushiriki uzoefu wowote waliowahi kuwa nao na Roho Mtakatifu. Waligunduaje ushawishi wa Roho Mtakatifu?

  • Mwalike kila mtoto kuchora sura yake katika mfuko wa karatasi. Mlika kwa tochi, ikiwakilisha Roho Mtakatifu, katika mifuko. Kisha weka vitu katika mifuko vitakavyozuia mwanga, kama vile kitambaa cha mkononi au kitambaa kilichofumwa, kuwafundisha kwamba chaguo zetu mbaya zinaweza kuzuia ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Waache watoto watoe kitambaa cha mkononi au kilichofumwa kutoka katika mifuko yao kuwakilisha toba.

Yohana 15:1–8; 17:3

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wananitaka niwafahamu Wao.

Utabariki maisha ya watoto milele kwa kuwasaidia kuja kumjua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Shughuli za Yakini

  • Onyesha mmea wakati watoto wanachukua zamu kusoma mistari katika Yohana 15:1–8. Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo ni kama mzabibu? Je, sisi tunakuwaje kama matawi? Ni nini tunaweza kufanya ili tubaki karibu na Bwana?

  • Soma kwa sauti Yohana 17:3. Waulize watoto ni kitu gani wanachokifanya kumjua Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Shiriki ni kwa jinsi gani umekuja kuwajua Wao.

Yesu Akiwa na mtoto katika pajani

Kristo alifundisha, “Kaeni ndani Yangu” (Yohana 15:4).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kumuuliza mwana familia ni kitu gani wanaweza kufanya kumhudumia. Wakati wa darasa la wiki ijayo, wapatie watoto muda wa kushiriki kile walichofanya.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tohoa shughuli. Kama unafundisha watoto wadogo, unaweza kupata mawazo ya ziada ambayo unaweza kutumia kwa darasa lako katika sehemu ya muhtasari huu kwa watoto wakubwa. Vivyo hivyo, shughuli kwa watoto wadogo zinaweza kutumiwa kufundisha watoto wakubwa.

ukurasa wa shughuli: kushika amri.