Njoo, Unifuate
Mei 27–Juni 2. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’


“Mei 27–Juni 2. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya (2019)

“Mei 27–Juni 2. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Ujio wa Pili

Ujio wa Pili, na Harry Anderson

Mei 27–Juni 2.

Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21

“Mwana wa Adamu Atakuja”

Unaposoma Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; na Luka 21, unaweza kujiuliza, “ni ujumbe gani sura hizi unazo kwa ajili yangu mimi? kwa ajili ya familia yangu? kwa ajili ya wito wangu?”

Andika Misukumo Yako

Wanafunzi wa Yesu lazima waliona unabii Wake kuwa wa kushtusha: hekalu kuu la Yerusalemu, kitovu cha mambo ya kiroho na kiutamaduni cha Wayahudi, lingeharibiwa kabisa kiasi kwamba “kusingesalia … jiwe juu ya jiwe.” Kiuhalisia wanafunzi walitaka kujua zaidi. “Je, mambo haya yatakuwa lini?” waliuliza. “Na ni nini dalili ya kuja kwako” (Joseph Smith—Mathayo 1:2–4). Majibu ya Mwokozi yalifunua kwamba angamizo kuu litakalokuja kwa Yerusalemu—unabii uliotimizwa mnamo BK 70—kwa kiasi fulani lingekuwa dogo ikilinganishwa na dalili za kuja Kwake katika siku za mwisho. Vitu ambavyo huonekana thabiti hata kuliko hekalu katika Yerusalemu vitathibitisha kuwa vya muda mfupi—jua, mwezi, nyota, mataifa, na bahari. Hata “nguvu za mbingu zitatikiswa” (Joseph Smith—Mathayo 1:33). Kama tuko macho kiroho, ghasia hii inaweza kutufundisha kuweka imani yetu katika kitu ambacho kweli ni cha kudumu. Kama Yesu alivyoahidi, “Mbingu na dunia zitapita; lakini maneno yangu hayatapita. … Na ye yote mwenye kuyahifadhi katika hazina maneno yangu, hatadanganyika” (Joseph Smith—Mathayo 1:35, 37).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Joseph Smith—Mathayo

Joseph Smith—Mathayo ni nini?

Joseph Smith—Mathayo, iliyopo ndani ya Lulu ya Thamani Kuu, ni dondoo kutoka Tafsiri ya Joseph Smith ya Biblia. Ina masahihisho kwenye mstari wa mwisho wa Mathayo 23 na Mathayo 24 yote (ona Kamusi ya Biblia, “Tafsiri ya Joseph Smith”). Masahihisho ya Joseph Smith yenye mwongozo wa kiungu hurejesha kweli za thamani ambazo zilikuwa zimepotea. Mstari wa 12–21 wa Joseph Smith—Mathayo inahusu maangamizo ya kale ya Yerusalemu; mstari wa 21–55 ina unabii kuhusu siku za mwisho.

Joseph Smith—Mathayo1:21–37; Marko 13:21–37; Luka 21:25–38

Unabii kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi unaweza kunisaidia kuukabili wakati ujao kwa imani.

Inaweza kuwa ya kutia wasiwasi kusoma kuhusu matukio kuelekea Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Lakini Yesu alipotoa unabii wa matukio haya, Aliwaambia wanafunzi Wake “msifadhaike” (Joseph Smith—Mathayo 1:23). Je, ni kwa jinsi gani unaweza “kutofadhaika” unaposikia kuhusu matetemeko, vita, uongo, na njaa? Fikiria swali hili unaposoma mistari hii. Wekea alama au andika ushauri wowote wa hakikisho jipya unaopata.

Ona pia Mafundisho na Maagano 29:14–21; 38:30; 45:16–52; 88:86–94; “Ujio wa Pili wa Yesu Kristo,” Mada za Injili, topics.lds.org.

Joseph Smith—Mathayo 1:26–27, 38–55; Mathayo 25:1–13; Luka 21:29–36

Lazima niwe tayari daima kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi.

Mungu hajafunua “siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu” (Mathayo 25:13). Lakini hataki siku hiyo ije kwetu “ghafla” (Luka 21:34), hivyo ametupatia ushauri kuhusu jinsi ya kujiandaa.

Unaposoma mistari hii, tambulisha mafumbo na mifanano mingine ambayo Mwokozi aliitumia kutufundisha kuwa daima tujiandae kwa Ujio wa Pili Wake. Je, unajifunza nini kutoka kwayo? Je, unashawishika kufanya nini?

Mathayo 25:14–30

Baba wa Mbinguni anategemea nitumie zawadi Zake kwa busara.

Katika wakati wa Mwokozi, “talanta” ilimaanisha pesa. Lakini fumbo la Mwokozi la talanta linaweza kutufundisha kuhusu jinsi anavyotaka sisi tutumie kila baraka Aliyotupatia. Bwana anatarajia sisi tuboreshe kile ambacho Ametupatia. Unaposoma mfano huu, tengeneza orodha ya baadhi ya baraka na fursa ambazo Baba wa Mbinguni amekupatia. Je, Yeye anatarajia ufanye na baraka hizi? Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuzitumia zawadi hizi kwa busara zaidi? Je, ni kwa jinsi gani talanta zako zimekuzwa ulipomtumikia Bwana?

Mathayo 25:31–46

Ninapowatumikia wengine, Ninamtumikia Mungu.

Kama umewahi kujiuliza ni kwa jinsi gani Bwana atayahukumu maisha yako, soma fumbo la kondoo na mbuzi. Je, ni nini kitakuwa na umuhimu zaidi utakaposimama mbele ya Kristo?

Ona pia Mosia 2:17.

Marko 12:18–27

Je, ndoa zitaendelea baada ya Ufufuko?

Tunajifunza kutoka ufunuo wa siku za mwisho kwamba maelezo ya Yesu “Watakapofufuka kutoka kwa wafu, hawaoi, wala hawaolewi” humaanisha wale ambao hawajaingia kwenye agano la ndoa ya selestia (ona M&M 132:15–16). Ndoa ya selestia, ambapo “mwanamume [huoa] mke… kwa agano jipya na lisilo na mwisho,” itadumu “milele yote” kama mume na mke ni wakweli katika maagano yao (M&M 132:19).

Picha
ikoni ya kujifunza kwa familia

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Kwa Familia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

Joseph Smith—Mathayo

Ili kusaidia familia yako kutafiti sura hii, waalike kutafuta mafundisho ya Mwokozi kuhusu jinsi tunavyoweza kujiandaa kwa Ujio wa Pili Wake (ona, kwa mfano, mstari wa 22–23, 29–30, 37, 46–48). Je, familia yako inaweza kufanya nini ili kufuata ushauri huu?

Joseph Smith—Mathayo 1:22, 37

Je, inamaanisha nini kuyahifadhi katika hazina maneno ya Mungu? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya hili kama familia? Je, ni kwa jinsi gani kufanya hivyo kutatusaidia kuepuka kudanganywa?

Mathayo 25:1–13

Unaweza kutumia picha ya wanawali kumi ambayo huambatana na muhtasari huu kujadili Mathayo 25:1–13. Je, ni maelezo gani ya kina wanafamilia huona katika picha hii ambayo yameelezewa katika mistari hii?

Je, wanafamilia watafurahia kutafuta kote nyumbani karatasi zenye matone ya mafuta ambazo umeficha? Unaweza kushikisha matone kwenye vitu vinavyowakilisha mambo ambayo wanafamilia wanaweza kufanya ili kuimarisha shuhuda zao na kujitayarisha kwa Ujio wa Pili, kama vile maandiko, nguo za kanisani, au picha ya hekalu.

Marko 12:38–44; Luka 21:1–4

Je, wanafamilia wanaweza kujifunza nini kutoka katika mfano wa mjane? Je, Mwokozi aliwafundisha nini wanafunzi Wake kuhusu matoleo? Onyesha karatasi ya matoleo ya zaka, na jadili matoleo ya familia yako kwa Bwana na jinsi gani matoleo haya husaidia kujenga ufalme wa Mungu. Je, kuna matoleo familia yako inatoa ambayo hayawezi kuandikwa kwenye karatasi ya zaka?

Picha
Senti ya Mjane.

Senti ya Mjane, na Sandra Rast

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Andaa Mazingira yako. “Mazingira yetu kwa kiasi kikubwa yanaweza kuathiri uwezo wetu wa kujifunza na kuhisi kweli” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 15). Jaribu kutafuta mahali pa kujifunza maandiko ambapo pataalika ushawishi wa Roho Mtakatifu. Muziki wenye kuinua na picha vinaweza pia kumwalika Roho Mtakatifu.

Picha
Wanawali Kumi

Watano kati Yao Walikuwa wenye Busara, na Walter Rane

Chapisha