Njoo, Unifuate
Nyenzo za Ziada


“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Nyenzo za ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

familia ikitazama kompyuta ya tableti

Nyenzo za Ziada

Nyenzo hizi zote zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye LDS.org.

Magazeti ya Kanisa

Magazeti ya The Friend, New Era, Ensign, na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuelezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Kwa nyongeza ya matoleo ya chapa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi ya kusikiliza na video ya nyimbo nyingi za Kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.lds.org na katika LDS Music app.

Hadithi za Agano Jipya

Hadithi za Agano Jipya (2005) zinaweza kuwasaidia watoto kujifunza mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Agano Jipya. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika Gospel Library app na kwenye medialibrary.lds.org.

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo

Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo hutoa historia ya nyuma na mawazo ya kimafundisho kwa kanuni na matukio yanayopatikana katika maandiko.

Maktaba ya Vyombo vya Habari

Kazi ya sanaa, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kukusaidia wewe na familia yako kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazopatikana katika Agano Jipya. Tembelea medialibrary.lds.org ili kuvinjari mkusanyo wa nyenzo za vyombo vya habari vya Kanisa, ikijumuisha video za hadithi za Biblia, ambazo huelezea matukio katika Agano Jipya.

Mada za Injili

Kwenye topics.lds.org unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo za kusaidia, kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa kwa kina majibu ya maswali ya injili.

Kweli kwa Imani

Kama unahitaji msaada zaidi kuelewa kanuni muhimu za injili, fikiria kuangalia kwenye Kweli kwa Imani (2004). Nyenzo hii ina orodha ya kialfabeti ya mada za injili zilizoelezewa kwa maneno rahisi.