“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)
“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia
Nyenzo Hii Ni Kwa Ajili ya Nani?
Nyenzo hii ni kwa ajili ya kila mtu binafsi na familia katika Kanisa. Imetengenezwa ili kukusaidia wewe kujifunza injili—iwe peke yako au na familia yako. Kama hukuwa kila mara unajifunza injili siku za nyuma, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuanza. Kama tayari una mazoea mazuri ya kujifunza injili, nyenzo hii inaweza kukusaidia kuwa na uzoefu mwingi wa maana.
Je, Ni Kwa Namna Gani Ninapaswa Kuitumia Nyenzo Hii?
Tumia nyenzo hii katika njia ambayo ina manufaa kwako. Unaweza kuona ina manufaa kama mwongozo au msaada wa kujifunza maandiko kwako binafsi na familia. Unaweza pia kuitumia kwa jioni ya familia nyumbani. Mihutasari huonyesha kanuni muhimu zinazopatikana ndani ya Agano Jipya, hupendekeza mawazo ya kujifunza na shughuli kwa ajili ya watu binafsi na familia, na hutoa sehemu za kuandika mawazo yako.
Wewe na familia yako yawezekana kuwa tayari mnajifunza injili kila mara. Labda mna lengo la kusoma Kitabu cha Mormoni. Au labda unasoma kitabu kingine cha maandiko kwa ajili ya darasa la seminari au chuo. Njoo, Unifuate hakikusudiwi kuchukua nafasi au kushindana na mambo mazuri unayofanya. Kwaweza kukawa na njia za kujifunza kutoka kwenye Agano Jipya kila mara na bado ukaweza kufikia malengo yako mengine ya kusoma maandiko. Kwa mfano, unaweza kuendelea kusoma Kitabu cha Mormoni kwa kujifunza maandiko kwako binafsi na kusoma Agano Jipya na familia yako (au kinyume chake). Au, unaposoma Agano Jipya, unaweza kuangalia vifungu vya Kitabu cha Mormoni ambavyo vinaimarisha kile unachojifunza. Fuata mwongozo wa Roho ili kuamua jinsi ya kuanza kujifunza kwako mwenyewe neno la Mungu.
Ni Kwa Jinsi Gani Nyenzo Hii Inahusiana na Kile Kinachotokea Kanisani?
Mihutasari katika nyenzo hii imepangwa kulingana na ratiba ya kusoma kila wiki. Masomo yanayofundishwa katika madarasa ya watoto wa Msingi na Shule ya Jumapili hufuata ratiba sawa na hiyo. Ili kusaidia juhudi zako za kujifunza na kuishi injili nyumbani, walimu wako watakupatia fursa za kuelezea uzoefu wako, mawazo, na maswali kuhusu vifungu vya maandiko ambavyo umekuwa ukijifunza wakati wa wiki.
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili hujumuisha mihutasari kwa kila wiki ya mwaka isipokuwa Jumapili mbili ambapo mkutano mkuu unafanyika. Wakati mikutano ya kawaida ya kanisa haifanyiki kwa sababu ya mkutano wa kigingi au sababu nyingine yoyote, unaalikwa kuendelea kujifunza Agano Jipya nyumbani. Madarasa yako ya Kanisani yanaweza kuruka somo lililopangwa kwa tarehe hizo au kuunganisha masomo mawili ili kuendana na ratiba.
Je, Ninahitajika kufuata Ratiba?
Ratiba itakusaidia kuendana na vitu vilivyofundishwa katika madarasa ya Jumapili, lakini usijisikie kufungwa nayo; ratiba ni mwongozo tu wa kukusaidia kujipima mwenyewe. Kitu cha muhimu ni kwamba unajifunza injili wewe binafsi na kama familia.